Sunday, June 1, 2014

UFUNGUO WA TOBA PART 2

Asalaam Aleiykum

Pokea Funguo kwenye Viganja vyako huku ukiitikia Aamin itokayo Moyoni tena kwa nguvu, kaa ukumbuke karibuni utaingia kwenye Madarsa ya Ramadhan yenye kulea Roho, Na wewe hutaki ubakie kwenye giza ukiendelea kupapasa, Na fanya Ihsan moja ukiipata Funguo yenyewe basi (Share) na wenzio, wape faida na wao waepukane na Madhnmbi wapate Toba, Na kila mmoja wao atoacha kwa ajili ya kumfundisha au kumuonesha Funguo hii ya Toba na wapi yalipoandikwa mafunzo haya, basi na wewe una ujira wako kwa tendo hilo.
Sasa tunaanza kuutafuta Ufunguo, Ukichunguza kwa makini utaona wingi wa Madhanmbi yako ni yale kwa yale, na yenye alama za kujirejea rejea, umepata kujiuliza kwanini, ushawahi kushangaa kwanini kwenye Quraan kuna kauli naambiwa nisikaribie, nijiepushe, niinamishe macho, kwani kuna kitu gani kinatokea, tukitaka kujua kitu gani kinatokezea itabidi turudi mwanzo wa aya tuliyoitaja hapo mwanzoni ya sura ya (Qalam).
Kaapa Mwenye enzi Mungu kwa kitu alichokiumba yeye Mwenyewe kwa ubora wa neema yake, na kiapo cha Mwenye enzi Mungu sisi Wanaadamu inatupasa kukirejesha kwake Mwenyewe na kusema "Ametukuka Mbora Mwenye kuumba", Kasema Mwenye enzi Mungu "Naapa kwa Akili na kile kiandikacho hiyo Akili"(Kusudio ni huo utendaji wake kazi) Sasa Funguo yenyewe ni hiyo Akili na matumizi yake uamuzi unao wewe, na hiyo ndio (Freedom)ukitaka kufungua mlango wa kushoto au wa kulia hiyari ni yako Mwenyewe. 
Sasa nini kinatokea iwapo utafungua(Kutumia)mmoja katika Milango hiyo, kabla ya kuendelea naomba kwanza nikujulishe kitu, kuna vitu vingi vimetajwa kwenye Quraan, lakini nachagua viwili hivi kwa kuwa vimekamatana na kuona na kusikia, "Unaambiwa Angusha macho yako na Uhifadhi tupu yako  (قُل لِّلۡمُؤۡمِنِينَ يَغُضُّواْ مِنۡ أَبۡصَـٰرِهِمۡ وَيَحۡفَظُواْ فُرُوجَهُمۡ‌ۚ)   " la kwanza, na la pili "Unaambiwa jiepushe na mambo ya kipuuzi"(وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ )
Sasa kwanini makatazo hayo muhimu matatu yakasisitizwa, lazima ipo sababu Quraan haiwezi kusisitiza kitu cha kukunyimeni Raha, Na sababu kubwa yenyewe ni hiyo Akili yako, ina tabia au (System)yakuandika mambo mengi yenye kuona na kusikia, Na Kiumbe ukisha andika siri yake lazima ukisome ulichoandika, ukiandika (sex) utaisoma mpaka utaitenda, na ukiandika tu inaandikwa kwenye (Book)lako walo shika (Malaika) na ikisha huku kwenye akili yako maandiko hayo yanakua yanajirejea mchana kutwa mpaka ulale, na hivyo ndivyo ifanyavyo Akili yako, haina kazi nyengine ila kukusomea yote uloandika, funga macho uitizame Akili yako inakusomea nini, (kama ntakutokea ghafla utanionea haya) Inachapa kazi Akili yako kwa kukusomea Biashara, Uongo ulosikia, Dhuluma ulopanga, na kusikiliza mambo ya kipuuzi, unaandika kila siku mambo Million, yale unayoyatenda ikiwa (Thawabu) wewe chunguza hayarejei tena ukakumbuka lakini ikiwa (Dhanmbi) inaongezeka utamu kama (Kiporo) yanarejea tena na tena, mpaka unakua Mteja (Addicted) kwa vile huna nguvu ya kuyazuia, mambo ya kawaida tu kichwani unayapanga ukiyarejea tena na kuyapangua nini habari yetu sisi kwenye utamu wa dhanmbi, vipi wewe utakwenda (Beyond) Dhanmbi ufikie Mlango wa Toba, ndio maana mkaletewa basi Alfajiri hebu anzeni na Quraan, pengine mtazingatia acha Quraan ikurejee itakua Shahid wako na kila ikirejea unaandikiwa (Thawabu)"إِنَّ قُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِ كَانَ مَشۡہُودً۬ا ".
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment