Asalaam Aleiykum
Aya imeanza vizuri sana kwa kukueleza kuwa mwezi huu wa Ramadhan imeteremshwa hii Quraan, Unakumbushwa kwamba na wewe pia umeteremshwa na hii Ramadhan umetermshiwa iwe zawadi yako kutoka kwa Mollah wako, ili iwe nini? iwe huu Mualiko wako kila mwaka kumkumbuka Mollah wako alokuumba, Umeteremshiwa muongozo na hoja zilizo wazi kabisa zenye upambanuzi usiokua na shaka.
Hapa leo kazi yangu mimi kutoa huo ufafanuzi, ila nataka ukumbuke ufafanuzi ni wangu huna haja ya kuukubali, unaweza kubakia na kitambaa chako cha machoni na kuukataa ufafanuzi huu, Ufafanuzi wenyewe ni kuhusiana Baina ya Roho yako na hicho (Kiwiliwili)(Body) ilobeba hiyo Roho.
Wanazuoni wameugawa huu Mwezi wa Ramadhan kwenye mafungu matatu, (Kumi la mwanzo)Rehma na (Kumi la Pili)Maghfira na (kumi la tatu) kuepushwa na Moto, Na upambanuzi huo ni sahihi kabisa, kwani kinacho tokea katika mwezi huu ndio hicho hicho walichokieleza, Nini kinatokea?,
Katika kumi la mwanzo kama kweli utaifunga Ramadhan ipasavyo na kwa Imani ya ukweli kinatokezea kile kile kinacho tokezea kwenye (Ndoa) (Al Ruum 21).( مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ )
Najua utashangaa, wengine watasema hee kwani nafunga ndoa na Ramadhan, (Hayo ni mawazo finyu), sio kosa lako ukidhani hivyo, taratibu utakuja kufahamu, na mimi nilikua hivyo hivyo mpaka (Something of Beyond happen) kufungua fahamu yako, Tunakaribia Mwezi wa Ramadhan pata faida hii ili ujue nini kinatokea, tuko kwenye ufafanuzi na upambanuzi basi tuliza jicho na sikio, Kwenye (Ndoa) una ruzukiwa Mapenzi na watoto, na kwenye Ramadhan linatokea hili la Mapenzi kwa Mollah wako, Vipi?.
Unapoanza kufunga lazima ujue mambo mawili haya, unaunyima chakula mwili wako, kwa sababu hii (Body) inahitaji chakula, na ukiinyima chakula tu (Body) inaanza kushituka, unaipa (Shock) vipi mbona mambo yako hivi?, hapo moja kwa moja zinafunguka Rehma za kuhudumia Mwili ambapo (cells) zilo lala zinaanza kuamka, zinafanya marekebisho, zinatibu magonjwa Nk, Na kitu cha pili kinachotokezea (Mwili) ukinyimwa chakula(Automatic) unaipa Roho chakula chake nacho ni hayo mapenzi (Taqwa) vipi yanakua Mapenzi hayo? Ukimpenda Binaadamu mwenzako una (Share) unatoa huna kizuizi, hujali chochote, sasa mapenzi yenyewe katika mwezi huu yaangalie vizuri japo yamejificha, chakula unacho kwenye Friji, viporo vipo, maji baridi yapo na wewe una kiu kubwa, Mke au Mume yupo, vyote hivyo unaweza kuvifanya hakuna anokuzuia, lakini wewe kwa ajili ya mapenzi ya Mollah wako, jinsi ya Penzi lilivo kuzidi hata kusukutua unaogopa, wewe unaogopa kutizama mambo machafu, wewe unaogopa kufanya vitendo vya Haramu, wewe unaogopa kugombana au kugombanisha na sio kama kuna mlinzi au umelazimishwa, unafanya kwa hiyari yako na hayo ndio mapenzi na hiyo ndio Taqwa, ukiweza kufanya hivyo ukafikia (Stage) ya funga yako kukamilika, utaona wewe upo tafauti na mwili wako, tafauti na vitendo vyako, (Unaishi Kiroho) ukigundua hilo mapenzi yataanza ku (Shower)kuteremka, hutokubali tena kufutari peke yako, hutowacha maskini wateseke, utakua unampenda kila ajae kwako kwa mahitaji au kuwa karibu na wewe, na hapo utakua ushaupata utukufu wa Ramadhan na Taqwa yake. Mollah wetu tujaalie tuifunge kwa salama na tupate mapenzi yako yasokatika ndani ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment