Asalaam Aleiykum
Imekuaje mpaka ukafeli mtihani wako, Sababu ya mwanzo maskini hujui thamani ya Zawadi hii ya Uhai alokupa Mollah wako, Mollah wako kakuumba ikisha akataka ufanye mambo mawili tu, Nayo kama alivokuumba kwa Mapenzi yake na wewe umpende urejee kwake kwa njia ya Ibada ama tuseme (Taqwa) kumkumbuka yeye na kumtaja kwa kadir ya uwezo wako.
Na la pili kufata muongozo wake kwa kutii amri zake zote, Sasa jitizame nini wewe unafanya, unakwenda kinyume na hayo yote mawili na pahala hapo ndipo yanapoanzia matatizo yako yote ulo nayo sasa hivi mpaka kufikia kuiomba hiyo Toba. Mkasa huu wa Toba ulianzaje, Kwa kuwa Mwenye enzi Mungu kaumba kiumbe chake akakipa mtihani na huku anaujua udhaifu wake ndio akamuekea hili chaguo la Toba kama atataka, na kama ataendelea na Jeuri yake basi hilo ni shauri lake, Na mtihani wenyewe ni huu.
وَقُلۡنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
"Ewe Adam (a.s) kaa wewe na mkeo katika bustani hii (Ya Peponi) Na kuleni humo popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu, mkawa miongoni waliodhulumu"
Hatari kubwa inatokana na kujua, kila anojua mwanzo mpaka mwisho anadhulumu mpaka mwisho wake, jiangalie wewe ukijua peke yako ikawa wengine hawajui unakuwaje, unaanza na dhuluma ya kiburi, dharau inakuingia ndani kwa ndani kuhisi kumbe hawa hawajui kitu, kwanini ikawa hivyo sababu kubwa nikuwa Kiza ni kutokuwepo na Taa, lakini taa ikiwepo kiza hakikai, na kabla ya kuipata hiyo Taa ya kujua wewe ulikuwa sawa sawa na sisi wenzio tuliopo kizani, lakini baada ya kuipata Taa unadhani utakubali kuishi tena kizani, hiyo ndio maana ya kuingia kwenye dhuluma, ukipata kulila tunda tu ushaingia kwenye ujuzi na wala hutoki tena, na kwa sababu Taa ina athari zake, ndizo zinazokupoteza wewe,(Kama vile)utamchukua mtu wa kijijini kwa ghafla umtupe (Japan) anavokua huyo ndivo anavokua mtoto, Mtoto anakuaje? (Innocent)kila mtoto anaona maisha yake kama pepo, Na sote ukiambiwa uhadithie utoto wako unasema sie ilikua hivi ikawa vile, raha hizi na zile, lakini ukianza kupata Fahamu kwa njia ya (Baleghe) mambo yanabadilika kuanzia hapo, fujo yote inaanzia kutokea wakati huo.
Unatoka kwenye ujinga unaingia kwenye werevu, Na ukiingia tu unaanza kudhulumu nafsi yako na hapo unafukuzwa na wewe kwenye Neema ya Mwenye enzi Mungu, Nabii Adam a.s alipewa maneno ya kutubu baada ya kuonekana anasumbuka kwa majuto na kuhangaika, ikisha kwa kuwa kenda kinyume na amri ya Mwenye enzi Mungu akatolewa (Peponi) huo ni mfano chochote utakacho fanya lazima ukilipe, ndipo akatolewa peponi, kwa hiyo na wewe kumbuka kwanza (Kama ulivo kopesha ndivo utakavo lipwa).
Maneno alopewa Nabii Adam a.s yalikua yana kazi mbili ndani ya nafsi yake, moja ilikua ni kwa ajili ya kunyenyekea na kurudi kwa Mollah wake, na ya pili ni kutibu hiyo fahamu ilofanya kosa kwa kumkumbusha kama wewe mkosaji na umo kuomba Toba, na hivyo ndio mpaka leo tukawa ukifanya kosa unalijua hili kosa lakini unakuwa umezidiwa na nguvu ya hilo kosa.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment