Asalaam Aleiykum
Na kila ukikumbuka mwezi huu wa Ramadhan kumbuka ni mwezi wa Ibada, basi na wewe ifanye ya aina yoyote ya Ibada ujira wake anaujua Mollah wako, Na utakapo kuzidisha Ibada ghafla utaona tabia yako imebadilika, utaanza kupenda Ibada kuliko mambo ya kipuuzi, Utakua unamfikiri Mollah wako kila saa na dakika, na ikikutokezea hali kama hiyo, hapo utakua umeipata Raha ya Ramadhan na faida zake, Na ikiwa utakua na dalili hizo basi Mollah wako anakupa ahadi ikiwa utakua na matatizo yoyote yale, kama una dhiki, au huna cha kukila, matatizo haya na yale kama kweli una mapenzi na Mollah wako basi jikumbushe mwisho wa aya ya pili na aya ya tatu sura ya (Talaq) inasemaje " وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُ ۥ مَخۡرَجً۬ا " Na anayemuogopa(Kwa kumpenda)Mwenye enzi Mungu humfanyia
Njia ya Kuokoka(Kutokea)
"وَيَرۡزُقۡهُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَحۡتَسِبُۚ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُ ۥۤۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَـٰلِغُ أَمۡرِهِۦۚ قَدۡ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدۡرً۬ا"
Na humpa Riziki kwa Namna asiyotarajia, Na anayemtegemea Mwenye enzi Mungu humtoshea, kwa hakika Mwenye enzi Mungu anatimiza kusudio lake, Hakika Mwenye enzi Mungu amekiwekea kila kitu kipimo chake.
Ukifunga kikweli na kufanya Taqwa Mwenye enzi Mungu atajaalia utoke kwenye hizo Dhiki, matatizo, shida, Dhanmbi, na zawadi yako itakua kuruzukiwa kwa njia usizotarajia wewe mwenyewe. Hapo tena ndio utaigundua Raha ya Ramadhan kumbe ndio inakua hivi, hizi ndio Raha zenyewe za kufunga, Basi hata itakapokwisha hiyo Ramadhan siku ya sikukuu wewe unakua husheherekei kama wafanyavo wengine, wewe unakua una Raha na ufanyalo nikuongeza Fu-Raha, Furaha ndio (Freedom) Maisha yote Mwenye enzi Mungu kaumba furaha, yote yalosalia viumbe tunayafanya kwa mikono yetu, Kwa hiyo funga kwa Imani, Ifanye Ramadhan yako ya aina nyengine mwaka huu, ifanye iwe tafauti na zote zilopita, badilisha tabia yako ya miezi 11 uzifunge kwa kutozifanya mwezi huu, basi ukimaliza mwezi wa Ramadhan utakua Mtu mwengine kabisa ambaye alo jaa Furaha, Mchache wa Dhiki za Roho, na zaidi ya yote sasa wewe ni Mcha Mungu, na hiyo ndio Raha ya Ramadhan ambayo tunamuomba Mollah atujaalie tuifunge kwa salama na afya njema,Mollah awasamehe na kuwapa ujira unaostahiki kwa wale wasoweza kutimiza Ibada hii ya kufunga, awaruzuku Ucha Mungu kwa njia nyengine zenye mfano wa mwezi huu wa Ramadhan. Amin
No comments:
Post a Comment