Asalaam Aleiykum
Unatizamwa Mali uliyonayo unaweza kuitoa kwa ajili ya (Allah) si unautaka Ucha Mungu, basi toa uonekane (Share) na wenzio igawe kama wewe kidume cha kweli, hiyo Mali itakufanya uepukane na adhabu za hapa Ulimwenguni na huko akhera uendako. Ndio maana nikakwambia vigumu sana kuwa Mcha Mungu, kwa sababu ndani ya Nafsi yako unaamini ukitoa utafilisika, na unasahau kujiuliza swali muhimu nani kakupa?. Basi hapo tena unaamua kubaki na Mali yako na uko Radhi adhabu za Mwenye enzi Mungu zikufike lakini hutoi chochote.
Basi hebu jiulize kama kweli uko tayari na hizo adhabu, wakati jino tu likikuuma au ukucha tu ukikatika Mtaa mzima wanajua leo fulani anaumwa, nini habari yako wewe kuhusiana na hizo adhabu za Mwenye enzi Mungu ambaye alokupa hilo jino(Hapo nakuachia mwenyewe utafakari) Na neno la tatu likawa hizo Nafsi zenu (Jihad ya Nafsi) mwanzo nilikupeleka Porini kuna kitu nimetia ndani ya nafsi yako, ndani ya Akili yako, kama utakua mwerevu basi yule Simba atakupa darsa kubwa, Na hili la Nafsi ndio zito zaidi, ikiwa unataka Ucha Mungu(Wakiristo wanasema Born again) mie nasema sio (Born again) sababu (Born again) unakua hujui mambo sasa hivi mambo unayajua mie naita (Painful Death) kifo cha machungu.
Uamuzi wa jambo hilo unalo wewe, na mimi kwanini nikaita hivyo kwa sababu ya (investment) zako, Ushazoea kusema uongo inabidi uache mpaka ukutoke uongo wote, vipi mpaka ule uongo wa mtu(Kapiga simu ishapokelewa unasema mwambie sipo)sasa useme ukweli mpaka watoto washangae, kwanini nikasema mpaka watoto washangae, sababu wewe umekulia katika mazingira ya kudanganywa na kudanganya kwa hiyo umerithisha na watoto, unamwambia mtoto nikirudi ntakuletea kitu fulani na ukirudi humletei, na unakua mkali, kwa hiyo mtoto anashangaa na sasa mfanye ashangae tena kwa kupona maradhi maradhi hayo, ndio maana nikaita (Painful death).
Uache kwenda Barazani wakati wewe ushazoea kwenda barazani, unadhani itakua rahisi,kuziacha karata, kuacha mipira, kuacha siasa, kuacha kusema watu, kuacha kusikiliza mambo ya kipuuzi,na kutizama (mambo machafu kwenye TV) ukiweza kuacha hayo yote basi moja kwa moja unakua Mcha Mungu, kwani ukiacha hayo yote, basi hiyo Nafsi moja kwa moja inajazwa na (Presence of God)Makumbuko ya Mwenye enzi Mungu, sasa kwanini haiwezekani na kwanini ikawa vigumu, haiwezekani kwa sababu ya Imani yako bado ndogo sana, na kutokana na hilo inakua vigumu kwa wewe kuwa Mcha Mungu, huwezi kuacha mambo yako, unayathamini sana, huwezi kuchagua baina ya mambo yako na Mollah wako, daima unachagua mambo yako na kwa hilo inakua vigumu kuupata Ucha Mungu.
No comments:
Post a Comment