Sunday, May 11, 2014

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 5

Asalaam Aleiykum

"وَلَوۡلَآ إِذۡ دَخَلۡتَ جَنَّتَكَ قُلۡتَ مَا شَآءَ ٱللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِٱللَّهِ‌ۚ إِن تَرَنِ أَنَا۟ أَقَلَّ مِنكَ مَالاً۬ وَوَلَدً۬ا "
Na Lau ulipoingia katika Bustani (Shamba)yako ungesema, Hivi nilivyo navyo amenitakia Mwenye enzi Mungu, (Na)Nguvu hazipatikani ila kwa (Kupewa na)Mwenye enzi Mungu, kama unaniona mimi nina mali kidogo na watoto wachache kuliko wewe.
Hayo ndio maneno unayotakiwa kusema wakati wowote unapopata mali au kitu chochote cha kheri, huko ndiko ku(Surrender)kujua kila kitu kumbe kinasababishwa na yeye, na mimi shukurani zangu ni kushirikiana na kila kiumbe kusheherekea Neema hii alonijaalia Mollah wangu.
Vipi utasheherekea? Huna haja ya kujisifu wala kufanya chochote cha majivuno, wewe unazijua nyumba za Maskini zipi, unawajua nani na nani wasio na uwezo, nini ufanye? toka bila ya vishindo nunua Chips kuku piga hodi kaa nao ule nao, au huwezi hivyo bado mawimbi ya Kiburi yanakuyumbisha, basi nunu gunia la Mchele wapelekee, na kama Mauti au chochote kitakukuta siku hiyo utakwenda huko Akhera ukakutane na Mlima wako wa (Thawabu). Lakini wapi ndio kwanza tumebaki kwenye fikra za kumzungumza fulani mpaka leo hana uwezo, hajamaliza kibanda chake, fulani anahangaika na maisha, yule mjinga sana atatupata wapi sie Familia yetu kubwa, tuko wengi, ikisha kabila letu tukufu, hicho ndio Kiburi.
"فَعَسَىٰ رَبِّىٓ أَن يُؤۡتِيَنِ خَيۡرً۬ا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرۡسِلَ عَلَيۡہَا حُسۡبَانً۬ا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَتُصۡبِحَ صَعِيدً۬ا زَلَقًا"
Basi huwenda Mollah wangu akanipa kilicho bora kuliko Bustani(Shamba)yako, Na kupelekea hiyo Bustani yako kwa mapigo ya Radi kutoka Mbinguni na ikawa ardhi tupu inayotelezesha.
Siku zote wanyenyekevu wanataraji kutoka kwa Mollah wao, akiwapa sawa, na asipowapa kwao sawa, wanajua Mollah wao ana sababu zake za kutokuwapa, Na hutaraji watakachopewa na Mollah wao kitakua daima kina kheri na chenye kuridhisha. Na angalia sana hususan Matajiri wangapi kwa viburi vyao wanavopigwa na Radi za Mwenye enzi Mungu wakafilisika, wanasiasa wangapi kwa Radi hizo wakashindwa kunyanyuka tena, ikawa kila Mtu unalolifanya haliwi, kila unalolitenda hufanikiwi, usisahau wakati huu ulopewa unafanya jeuri na Kiburi, basi na wewe ngojea wakati wako ukifika kila kitu kitabadilika utabaki na hadith nyingi nilikua hivi nikawa vile, unaishi kwa mawazo ya zamani ya kiburi, wakati huu unohadithia ndio (Nature)yako unayotakiwa uwe muda wote unaoishi katika Ulimwengu huu.
"أَوۡ يُصۡبِحَ مَآؤُهَا غَوۡرً۬ا فَلَن تَسۡتَطِيعَ لَهُ ۥ طَلَبً۬ا "
Au Maji yake yakawa yenye kuzama hata usiweze kuyapata(Mazao au mimea)
Kumbuka huo ni mfano, na wewe unaishi katika mifano kama hiyo, Na hivi ndivyo siku zote inavotokea, kama unaringia Mali, basi unaoneshwa vipi urahisi wake kuangamizwa mara moja, kama unaringia Majumba mafuriko au moto yanaweza kuyaangamiza mara moja, magari yanaweza kuungua moto au kupata ajali ukabaki huna hata moja, Dhahabu zinaweza kuibiwa zote ukawa huna kitu, na mambo haya usidhani yanafanyika kwa kutaka wewe, laa yanaweza kufanyika mara moja au yakafanyika kidogo kidogo ikawa kiburi chako kinakwenda arijojo kama kishada.

No comments:

Post a Comment