Asalaam Aleiykum
وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصۡبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيۡهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيہَا وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِہَا وَيَقُولُ يَـٰلَيۡتَنِى لَمۡ أُشۡرِكۡ بِرَبِّىٓ أَحَدً۬ا
Basi matunda (Mali yake)yakamungunyika(Kuharibika)na akawa anapindua viganja vyake(Kwa masikitiko)kwa ajili ya alichogharimia(Yale mashamba)ikawa miti yake imeanguka juu ya chanja zake, na akawa anasema, laiti nisinge mshirikisha Mollah wangu na yoyote.
Ukianza kufilisika jambo la mwanzo unaanza kufanya ishara za kushangaa, na kushangaa huku kunatokea ndani na kuko kwa aina mbili, Ima utashangaa kwa macho au kwa kutumia mikono, ukawa unauliza huku unapindua viganja vyako nini kimetokea, mbona sifahamu, Na ukifahamu tu, ndio vichekesho vinaanzia hapo, unajua unafanya nini? unaanza kuwa eti Mnyenyekevu, ghafla unageuka kuwa (Humble)unataka ufahamike sasa wewe mtu mzuri, kumbe vile kiburi kimeshakuacha mkono.
"وَلَمۡ تَكُن لَّهُ ۥ فِئَةٌ۬ يَنصُرُونَهُ ۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا "
Wala hakua na Watu wa kumsaidia baada ya (Kumkosa)Mwenye enzi Mungu, wala mwenyewe kujisaidia.
Hivyo siku zote ndivyo inavotokea, Ukifilisika au ukianguka kivyovyote iwe kisiasa au kiofisi, watu wakishagundua sasa huna uwezo tena, huna cha kusomesha, kiburi kishakukimbia, utashitukia watu wote wametawanyika na umebaki peke yako, hakuna hata mtu mmoja atakae kupa msaada, hakuulizi mtu kitu, hata ukipita watu hawajui kapita nani, hapo tena unakua huna kiburi na wala huna kunyenyekevu.
Mwenye enzi Mungu kakutupa na sasa wewe mwenyewe huwezi kujisaidia, na hayo ndio malipo ya Kiburi katika Ulimwengu huu, ukiendekeza kiburi katika Ulimwengu huu na kuwanyanyasa wenzio, basi weka mbele kukutwa na mfano huu alokupigia Mwenye enzi Mungu.
"هُنَالِكَ ٱلۡوَلَـٰيَةُ لِلَّهِ ٱلۡحَقِّۚ هُوَ خَيۡرٌ۬ ثَوَابً۬ا وَخَيۡرٌ عُقۡبً۬ا "
Huko(Akhera na hapa Duniani)Ufalme ni wa Mwenye enzi Mungu(yeye)tu aliyoko daima, yeye ndio bora kwa malipo na (Ndiye)bora wa(kuleta)matokeo mazuri.
Napenda kukujulisha Ndugu yangu Mwenye enzi Mungu ndiye mtoaji hapa Ulimwenguni na huko Akhera, huna haja ya kufanya Kiburi, hukupata kwa uwezo wako, huna haja ya kujisifu, Na ukijitupa kwa Mollah wako basi utapata mazuri hapa Ulimwenguni na kesho Akhera. Mollah tujaalie tukishinde Kiburi ili tuwe Wanyenyekevu, kwani Mwenye Kiburi hawezi kuipata Pepo ya Mwenye Enzi Mungu. Amin.
No comments:
Post a Comment