Asalaam Aleiykum
Napenda uelewe hakuna kitu chenye uharibifu na sumu kubwa ilofatana na Madhara kama kitu Kiitwacho (Kiburi), Na kitu hichi Kiburi kinatawala kila sehemu ya maisha ya Mwanaadamu, Iwe kwenye Dini, Siasa au Elimu, Kwenye Utajiri na hata mpaka kwenye Umaskini sumu hii inafika na kumuangamiza Mja.
Na hichi Kiburi ni nyenzo yenye nguvu ambayo inamfanya mpaka Mja aikose Pepo aliyoandaliwa na Mollah wake, Kwani kutokana na Kiburi (Ego)huwezi kabisa kuwa (Humble)Mnyenyekevu. Na kutokana na hicho Kiburi yanapatikana hayo madhara makubwa, Nini Madhara? Neno hili madhara lina mahusiano ya karibu na neno Maradhi, utaona yamepishana kwa herufi moja tu, na Kiburi kinaishi kwenye herufi mbili hizo, Vipi? Mwenye Kiburi kwa Watu anapeleka Madhara, na kwake Mwenyewe anajipa Maradhi.
Kabla ya kuingia katika Darsa yetu ya leo wacha tujitizame japo kidogo jee tunavyo Viburi au tumeepukana nacho, Alama ya mwanzo ya kukujulisha wewe umeepukana na Kiburi ni (Unyenyekevu). Na ukijijua kwamba wewe ni Mnyenyekevu basi ujue Kiburi kishapenya kwa siri kwenye unyenyekevu wako, Kinachokufahamisha kwa yakini kuwa wewe huna Kiburi ni Unyenyekevu ambao unakuja (Automatic)vitu viwili hivi havikutani kabisa Ima una unyenyekevu au una kiburi, huwezi ukawa na vyote viwili, Na hiyo ndio sheria ya Ulimwengu huu ikiwa utatizama Miti, Majabali na Milima, Mbingu na Nyota zake, Wanyama vyote vina nyenyekea isipokua Mwanaadamu.
Sasa tuviangalie Viburi vyetu vya kila siku na bora tuanze kwa wale walopewa Elimu iwe ya Dini au Dunia, na hapa nitawachagua watu wawili kuwaangalia, (Doctor na Sheikh)wawili hawa wana Mahusiano ya karibu na viumbe wenzao. Sasa muhudhurie Daktari wakati yupo na Mgonjwa upate kuona Kiburi kinavo chukua (centre stage) unaweza kuingia ofisini kwake hata asikutizame usoni, wewe unamuhadithia maradhi yako makubwa umeshughulika unataka japo anyanyue uso, japo aone imani kwa hili kiumbe mwenzangu karibu atakufa, wacha nimtizame kwa jicho la huruma pengine kwa kufanya hivyo mie ntapata matumaini, (kwa sababu chunguza hata ukenda kutizama wagonjwa hhospital hali yako inavokua ukiingia ndani unakua na wewe tafrani unajua kwanini kwa sababu wagonjwa wanamuhitajia mzima ili wapate kunyonya nguvu za afya, ndio maana na wewe unajiona kama hujisikii sikii, wewe chunguza hilo mara nyengine ukenda kwenye chumba cha wagonjwa, na hiyo ndio inayomfanya Daktari wakati wote kanuna, kumbuka kununa sio Kiburi, na hivyo ndivyo watu wazamani walipokua wanasema usisimame unatunyonya Damu ikiwa wao wamekaa, ni kweli sababu (Energy)ya Mwanaadamu inamazoea ya (Levitation) kwa hiyo kama watu wamekaa na wewe umesimama unapata zaidi hiyo (Energy)ambayo inaoneka mpaka kwenye hizo Camera wanazoziita (Heating seeking Camera)na hizo ndio nguvu nilizokusudia).
Naam Basi Daktari wetu akiamua kukutizama basi huku anatafuna kalamu (Pen) Maskini Daktari anakosa bahati ya kupata (Transformation) na yeye akawa (Humble)mnyeyekevu na kugundua zawadi aliyoletewa na mgonjwa huyo. Na kuhusu wapili wetu huyu Shekhe, Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment