Asalaam Aleiykum
Tunaendelea na darsa yetu ya kiburi tukiwemo tunaogelea katika aya ya 36 ya sura ya (Kahf)
"وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآٮِٕمَةً۬ وَلَٮِٕن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّى لَأَجِدَنَّ خَيۡرً۬ا مِّنۡهَا مُنقَلَبً۬ا "
Wala sidhani kama Kiama kitatokea, Na kama (Kikitokea)Nikarudishwa kwa Mollah wangu, bila shaka nitakuta(Kaniandalia)kikao chema kuliko hiki (alichonipa hapa Ulimwenguni).
Hicho ndio Kiburi kinatafauti ya kiasi tu, anasema huyo alopewa wala sidhani kama kiama kitasimama, hiyo ndio kufuru ilochanganyika na jeuri ikalelewa na Kiburi, Sasa njoo kwetu sisi ikisha ujichunguze upo unakula Raha za aina yoyote au upo kwenye Madaraka Fulani na wewe pia unatumia maneno hayo hayo , ila tafauti yake wewe umekua Bingwa wa kupindua lughaunabadilisha kidogo, unasema sidhani kama nitakufa sasa hivi, labda mpaka niwe Mzee, wacha nile Raha, Na hata kama nitakufa si ninazo Sala zangu tano nishatanguliza, Na pia siku fulani nilimsaidia fulani, basi namie nikirudi huko Akhera nitapewa hiyo pepo ya Jumba la ghorofa.
Hivyo ndivyo tulivyo na Viburi vyetu, vinatusahaulisha wazee wetu, ndugu zetu, marafiki zetu walo lala hoi maskini hawana hata cha kukila majumbani kwao na waislam wenzetu na walimwengu kwa jumla.
"قَالَ لَهُ ۥ صَاحِبُهُ ۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ أَكَفَرۡتَ بِٱلَّذِى خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ۬ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٍ۬ ثُمَّ سَوَّٮٰكَ رَجُلاً۬ "
Mwenzake (Msokitu)akamwambia akiwa ana mjibu jee unamkufuru yule alokuumba kwa Udongo, ikisha kwa tone la manii, halafu akakufanya Mtu kamili.
Kumbuka Quraan ni mawaidha ya kukuzindua na kama bado umezama kwenye Kiburi huu ndio wakati muafaka wa kujiokoa, Na sisi tunakukumbusha jee umesahau kama wewe asili yako ni Udongo, jitizame vizuri ukitiwa (Vipodozi)ndipo dongo linavojitokeza, ikisha ukaumbwa kupitia mbegu ya uzazi, halafu tena ukafanywa Mtu mwengine kabisa uliye kamili, basi haya yote hayakukumbushi kitu ukajiona kumbe mimi ni dhaifu na wajibu wangu kuwa Mnyenyekevu, Na basi kama kweli ushakua Mtu kamili utaona unaanza kupata ishara za kuwacha Kiburi na unakuwa Binaadamu wa kawaida.
Na Kiburi kikiondoka unarejea kuwa Mtu kamili hutaki kufanya sura ya (Plastic) hutaki tena kucheka kwa kudanganya, humjali fulani atajua, fulani ataona, nani kasema wewe unaamua kuwa Mtu (Natural)Mtu kamili, kinyume cha hivyo wewe (Feki)wewe ni Kiburi kitupu, na kaa ukijua Kiburi ni Maradhi.
"لَّـٰكِنَّا۟ هُوَ ٱللَّهُ رَبِّى وَلَآ أُشۡرِكُ بِرَبِّىٓ أَحَدً۬ا "
Lakini (Mimi Namuamini)Mwenye enzi Mungu wangu ndiye Mollah wangu wala simshirikishi Mollah wangu na yoyote.
Mwanzo pametajwa maneno muhimu yanofaa kuzingatiwa kwa makini , Kasema Mnyenyekevu na hivi ndivo sote tunavotakiwa tuamini, kuwa Mwenye enzi Mungu kaumba kila kitu, Na vyote anavotupa vinatokana na yeye na pia kutokea kwake, Basi sio hilo tu hata mimi mwenyewe natokana na yeye Mollah wangu, kwa hiyo sina haja ya kumshirikisha na yoyote yule kwa sifa, kwa msaada wala kuogopa, kuanzia leo nawacha Kiburi changu, na najua chochote kinachotokea kwake hakuna mwengine mwenye uwezo wa kukizuia isipokua atake mwenyewe, na mimi sina jinsi ila kuwa mnyenyekevu kwake yeye Mollah wangu na viumbe vyake.
endelea part 5
No comments:
Post a Comment