Asalaam Aleiykum
Sasa wacha Tumgeukie Sheikh tumuangalie na Majuba yake vipi kiburi kinavo muhangaisha, Mkono wa kulia kashika Funguo zimeandikwa(Peponi) Mkono wa kushoto kakamata (Raba) ya kufutia Madhanmbi, hapo tena hana shaka ya kudhulumu wala kusema uongo, haogopi kula haramu wala kutoa Fatwa za uongo, na kibaya zaidi anauza na Dua, Dua Elfu kumi, au Yasini Pound ishirini hivi ndivo tulivyo sisi tunao vaa vilemba vya Ushekhe, Viburi vimetutawala tunasahau kuwa tunawatumikia Binaadamu wenzetu kwa ajili ya Mwenye Enzi Mungu.
Na Wafuasi wanaendelea kukipalilia Kiburi hicho kwa kumwagia Shekehe huyo sifa kemkem kwa dua zake na kazi zake zisizo mfano, Na wawili wengine Mwanasiasa na Tajiri hawa hawana hata dawa, sina haja hata ya kuwazungumza, Mnajua vipi Viburi vyao vinavyo mwagiwa maji na kupaliliwa, Na mambo hayo yote yanaletwa na watu wa nje, bila ya watu wa nje Kiburi kinakufa moja kwa moja, hakiwezi kusimama.
Tujitizame na maneno yetu unavoambiwa, "Eti watu watasemaje""Watu watakuonaje"Shughuli zote unajipamba wewe lakini kwa ajili ya kufurahisha Watu, Mwenye hufurahi na kama unataka kujijua kwanini ufurahi wacha aje mtu akwambie shati au kanzu yako ina doa au imechanika mbele ya halaiki ujione unavokua, hapo ndio utajua unafanya kila kitu kwa ajili ya watu, na kama watu hawajakusifu unaumia sana. Inafikia wakati mpaka kwenda msikitini inategemea watu watasemaje kama hawajaniona, kutokana na hali hiyo sote tumegeuka kuoneana chuki, kufanyiana uadui, kuoneana husda yote sababu ya Kiburi.
Na kawaida ya Kiburi ukiwa nacho kwa siri au dhahiri basi unaelekea kwenye njia ya kumkufuru na kumshirikisha Mollah wako bila hata ya wasiwasi.
Sasa leo tunaingia katika Darsa yetu ya Kiburi kwa aya zilizomo kwenye Sura ya (Al-Kahf-aya ya 32 mpaka 44)
"وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلاً۬ رَّجُلَيۡنِ جَعَلۡنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيۡنِ مِنۡ أَعۡنَـٰبٍ۬ وَحَفَفۡنَـٰهُمَا بِنَخۡلٍ۬ وَجَعَلۡنَا بَيۡنَہُمَا زَرۡعً۬ا "
"Na Wapigie mfano wa (Watu)waja wawili, Mmoja wao tulimjaalia(Kumpa)Mabustani mawili(Mashamba)ya mizabibu, Na tukaizungushia mitende, Na pia katikati yake tukatia miti ya Nafaka(Ya kila aina)."
Mfano ndio mfano, unaweza kuwa wa aina yoyote, lakini cha muhumu ndani ya mfano huo kuna mafundisho, unaweza kuwa mfano huo wako wewe uko Dubai na mwenzio yuko pemba, au ukawepo England na mwenzio yuko yupo Unguja, ama wewe upo Oman na Rafiki yako yupo Tabora, la Muhimu ni mfano ulotolewa na Mwenye enzi Mungu na unaendelea kutokea mpaka hii leo kwako na kwangu, kumbuka ukipewa na Mollah wako hakuna kupingwa na mtu yoyote, Baraka zake zinaendelea kukushukia.
Na pia napenda utambue huu ni mfano wa waja wawili waliopo kwenye Mji fulani.
Endelea kukifatilia kisa hiki kwenye part 3 mpaka 6 itakayomalizikia wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment