Sunday, May 18, 2014

UGUMU WA UCHA MUNGU PART 1

Asalaam Aleiykum,

Watu wengi wanaamini au wamefunikwa na dhana ya kuwa Ucha Mungu ni Jambo Rahisi unaloweza kulipata kwa njia ya (Cheap). Napenda kukujulisha ni vigumu sana kuwa Mcha Mungu, kwa sababu mtihani wa Ucha Mungu unatoka kwa yule alokuumba, Sasa baba au mama, au bosi wako unaweza kuwadanganya lakini vipi utaweza kumdanganya Mwenye kusikia,Kuona,kujua,asiyesahau au kupatwa na usingizi, vipi utamdanganya unaweza kudanganya viumbe vyake lakini sio Huyo Mwenye kutoa hiyo hadhi ya Ucha Mungu.
Sasa hebu jiangalie ikiwa Mitihani hii ya duniani lazima ukopie, ukitaka kutoa (Speech)Khutba lazima uandike, nini habari yako wewe na huo Mtihani wa Ucha Mungu, Mtihani ambao majaribio yake yanatoka kwa Mollah wako. Kutoka kwa Mollah wako unapewa karatasi nyeupe unaweza fanya mtihani wa Taqwa fanya, huwezi basi subiri Rehma za Mollah wako zikufikie, lakini usijinasibu hata kwa siri kuwa wewe Mcha Mungu.
Nimesikia Bwana Mmoja baada ya kusikia mawaidha makali yakamtoka machozi baada ya kujiona kafeli mitihani ya Mwenye enzi Mungu, ikisha akasema ingekua sio (Sex) sasa hivi namie  nakwenda peponi. Maneno mazuri sana katumia, kajielewa kwamba  yeye keshaingia kwenye gari la (motoni) ndio maana akasema ingekua sio (Sex) Na sio (Sex) pekee kuna mambo  mengi yanokuzuilia kuingia Peponi, mengi yanakuzuilia kuwa Mcha Mungu na usende peponi, Lakini hili la (Sex) ni (Nature) na kama jambo la (Nature) basi acha sasa nikupeleke  kwenye (Nature) yenyewe huko kwenye Mbuga za wanyama nikakuoneshe wanyama labda wanaweza kukutibu.
Wewe una kawaida ya kujiita Simba,(Kidume) Basi Simba yupo porini, sasa muangalie uone tafauti yako na yake, Simba akiwa na njaa anatafuta mawindo anakamata kinyama ikisha anakula akashiba, Basi utamuona Simba huyo hata ampitie kondoo mbele yake anakua hana haja, hatamani tena, lakini jitizame simba wewe, Nyumbani una Mke au Mume, unafurahishwa upendavo, basi ukimaliza tu uko kwenye simu unataarisha furaha nyengine za nje, Na hasara ilioje kwani nyumbani umefurahishwa wewe na kule nje unakwenda kumfurahisha mwengine, unayumba na makapu yako ya vitoweo, unapepesuka na doti za kanga, cheni za dhahabu na venginevyo, basi hiyo ndio tafauti yako wewe Simba wa mjini na yule wa porini, halafu tena unakaa kuomba Toba lazima useme ingekua si (Sex). endelea part 2

No comments:

Post a Comment