Sunday, August 31, 2014

MAISHA YA AKHERA PART 1

Asalaam Aleiykum

Umeishi Maisha ya Duniani mpaka sasa unayajua yalivyo, Jee unayo habari ya Maisha ya Akhera? zimekujia fikra kuwa yapo maisha mengine ambayo utakayokwenda kuishi, ni vigumu kukujia fikra hizo kwa kuwa unaishi katika hali ya kusahau katika Ulimwengu huu, ila jambo moja una hakika nalo kuwa kuna siku nitaondoka katika Dunia hii nakwenda huko pahala panapo itwa Akhera.
Japo hujui siku gani lakini kimya kimya ushajiandaa, ushakubali utaondoka, sasa kama yote hayo unayatambua kwanini hujiulizi (Adress)gani utafikia huko uendako, Sababu kubwa huwezi kui(Google)hiyo(Adress)yako ni kuogopa kwako kutokana na matukio ya matendo yako unajua fika makaazi yako yatakua si mazuri, unaogopa kuijua (Anwani)yako ilo mbaya, kwa hiyo wewe kila saa na dakika unapigana bila ya kujijua kusahau maisha haya ya Akhera, Lakini kwa kuwa unapendwa na Mollah wako kwa hiyo kupitia kwa Mtume wake s.a.w kakuletea kauli ya Hadith ambayo inasema "Kahudhurieni Makaburi yakukumbusheni Akhera".
Hapo kuna mambo makubwa yakuzingatiwa na mwanaadamu, kwanza hukutakiwa uchukue chochote, hukutakiwa ukamate kitabu au umtegemee Sheikh akwambie fanya hivi au fanya vile, haitakiwi Akili ya mtu yoyote ikuamrishe kitu, bali unatakiwa wewe mwenyewe utoke iwe usiku au mchana uko mweupe huna mashiko yoyote ufanye safari ya kwenda kuhudhuria (Kaburi).
Sasa kwanini ikawa kaburi ndio likukumbushe Akhera, Kwanini hukumbuki mwenyewe, kwanza kabisa napenda uelewe Maisha yako ya Duniani yanaanzia takriban kitandani na hususan usiku, na huishia Makaburini hususan mchana na hapo ndio Daraja la wewe kuvuka kurejea huko Akhera ambako ndiko uliko tokea.
Na la pili huwezi kukumbuka kwa sababu wewe mwenyewe upo katika dunia hii unajiona unaishi lakini ushakufa kitabia, umekufa katika mazoea ya usahaulifu, umeota mizizi katika katika mazingira ya kawaida yako unavyoishi kula, kulala, kuamka kwenda kazini, kurudi nyumbani ima barazani au kwenye TV, na kesho yake hivyo hivyo huna mbadala, kawaida yako inajulikana ya mwenendo maalumu, kwa kuwa umesahau kabisa Maisha haya ya Akhera ndio unaambiwa hebu nenda "Makaburini", kahudhurie maziko, huenda asaa ukakumbuka kitu, huenda kuna kitu kikatokezea labda unaweza kukurupuka usingizini, ukaamka ghafla ukakumbuka Akhera, sasa ili ukumbuke uende vipi huko makaburini au "Mazikoni". Endelea part 2

MAISHA YA AKHERA PART 2

Asalaam Aleiykum

Inayotakiwa kukumbuka ni Nafsi yako ilojificha katika mambo mengine chungu nzima, ambayo machache nimeyataja huko mwanzoni, ndio maana hukuambiwa nenda makaburini ila umeambiwa kahudhurie.
Nini Kuhudhuria? Kuhudhuria ni kitendo cha kuwapo (Present), sasa kabla ya kuzungumzia huu muhudhurio wacha nikukumbushe vipi wewe unahudhuria hayo makaburi, unakwenda Makaburini pengine baada ya Miaka na tena labda yawepo maziko, halafu ukishafika hapo mazikoni ile maana nzima ya mahudhurio unaitupa pembeni ima utakua umenasa kwenye (Whatssup)kwa siku hizi, ama umejaa katika mazungumzo, au utajikuta kwenye mawazo ya ubishi unataka kujua hawa watafanya manyago gani leo, umejaa ubishi, shari ya ushindani imekushika, hizo ndio hali zetu leo tunapo hudhuria makaburi.
Sasa mahdhurio gani yalokusudiwa? kumbuka unasoma kitu cha kukumbusha Akhera na wewe una hamu ya kujua utafikia (Adress)gani siku yako ikifika, basi kuwa mstahamilivu wakati tukipita taratibu katika kukumbushana huku.
Kinachotakiwa kuhudhuria Makaburini ni wewe Mwenyewe sio (Mind) yako, na wala sio mara moja huwezi kulipata tukio la ukumbusho huo, kusudio zima la zoezi hili ni kuvunja Kiburi chako, kuondosha mimi fulani ,kuvunja kujiona kwako, kuondoshea mbali cheo chako, kuutupa utajiri wako pembeni kabisa, kukufanya wewe ni udongo mtupu, huna ulicho kamata kwenye ulimwengu huu, kufanywa wewe (Empty) kabisa, Na kama umehudhuria kweli Makaburini basi itakupata (Shock)kama vile ulivyoshituliwa au kukosa kugongwa na gari au mshtuko wowote unaoukumbuka ukaona umekwenda moyoni, na moyo sasa unakwenda mbio.
Leo unashuhudia Baba, Ndugu, Marafiki wanamzika na kumfukia Kipenzi chao ambacho jana pengine walikua wakicheka nae, wakila naye, wakimsifu kwa uzuri, leo wanamfukia haraka ili asije akaleta udhia, muda na wakati wake ushamalizika, viumbe wa Akhera mpokeeni mwenzenu sisi tushaishi naye na leo hatumjui tena, si mwenzetu, na huku unawaona wale wale walokua vipenzi vyake pengine wanafanya na (Masikhara)hapo hapo makaburini huku wanajaza dongo likufunike futi sita chini ya Ardhi, wanasahau kama jana tulikua tukila nae, anasahu kila mtu alokuwepo hapo kama pengine siku chache tu itakua zamu yake. Sasa nini kinatokezea ikiwa wewe kweli umehudhuria?
Endelea part 3

MAISHA YA AKHERA PART 3

Asalaam Aleiykum

Sasa ikiwa ulohudhuria umepata bahati ya ukumbusho moja kwa moja unapata bahati ya kujua kwenye moyo wako sio katika Akili yako kuwa wewe sio hichi kiwiliwili wanachokizika, na ukiweza kumtizama huyo Maiti kama umepata huo ukumbusho utaona kuna kitu kimeondoka, kuna kitu kimepungua ukiligundua hilo (Eureka) hutokua kama zamani tena, utabadilika milele, utakua umegundua kitu ambacho watu wengi hawakigundui mpaka mwisho wa umri wao, kwanza itakuingia khofu ikisha yataingia mapenzi ya kutaka kujua zaidi vipi Maisha ya Akhera yakoje, pia utagundua kumbe katika Ulimwengu huu mimi ni mgeni, utagundua tafauti yako na kiwiliwili chako, utagundua katika Ulimwengu huu mimi sina Uhusiano wa kudumu na yoyote, mimi ni mpita njia ambaye naishi kwenye Ulimwengu huu kwa muda mchache sana, Ikiwa kiwiliwili kinafukiwa na wale walo wangu niloishi nao Ulimwenguni, Sasa hebu nifanye kujijua mie nani na safari yangu nakwenda wapi kuanzia leo, leo napata nafasi ya kujijua kuwa asilimia kubwa ya kiwiliwili changu ni hii Ardhi, ambayo hivi sasa wako mbioni kunirejesha kama ilivyosemwa kwenye sura ya (Taha aya ya 55)
 مِنۡہَا خَلَقۡنَـٰكُمۡ وَفِيہَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡہَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ 
Katika hii (Ardhi)Tumekuumbeni, Na Humo tutakurudisheni, Na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine (Tena)
Kuwa na hakika kwa mujibu wa aya hiyo kwamba utarejea tena katika maisha kama haya lakini kwenye mji wa Akhera, utapata kuelewa kumbe kinachokufa na kuzikwa ni kiwiliwili changu tu, lakini mimi mwenyewe niko hai na nashuhudia kufa kwa kiwiliwili changu na naendelea kusihi na Mauti hayanigusi ila na hama kwenye Ulimwengu huu na kuhamia huko Akhera ambako safari yake inaanzia Makaburini nilikoambiwa nikahudhurie, Huko Akhera, Jee kukoje huko Akhera, mie nitaishi vipi huko Akhera, nani atakua Mwenyeji wangu, mapokezi yangu yatakua vipi, hawa nilowaita wenzangu Ulimwenguni wananifukia na kunisahau jee Maisha yangu ya Akhera yatakua vipi.
Hayo ndio Maswala unayotakiwa kujiuliza, khasa ukijua Umri wenyewe ushakatika na ni muda mchache unaishi katika Ulimwengu huu, Mwaka wa hamsini huu wale wote walokwenda hawajarudi, wana hali gani huko Akhera, wanaishi vipi huko katika Mamlaka ya Akhera, namie nifanye nini nikenda huko niipate salama Usalimini, najua hapa Duniani nimepokewa na viumbe wenzangu nikakaa nao, wako walonichukia wakanidhulumu, wakanipiga, wakanipa machungu, nilogombana nao nikatenda nilotenda, ikisha nikachukua zawadi nzuri na mbaya sasa nini yatakua mapokezi yangu kwa hao viumbe nisowajua katika Maisha ya Akhera. Mollah nijaalie Radhi zako huko ninapokuja niwe nimefaulu, nisiwe katika Ulimwengu huu nimepata misukosuko na huko Akhera napata misukosuko, wapi yatakua makaazi yangu huko Akhera?

Sunday, August 24, 2014

LAZARU LAZARU AMKA PART 2

Asalaam Aleiykum

Sheria zote ni za Mwenye Enzi Mungu, ndio Maana mimi binafsi siwezi kuishambulia (Biblia)ile ya kweli ambayo haikuongezwa ufundi ndani yake kwa sababu najua asilimia 75% ya (Biblia)imo ndani ya Quraan au kinyume chake, Ndio Maana katika Quraan kuna andiko la aya ya 285 sura ya (Baqarah) linalosema"Mtume(Muhammad s.a.w)ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mollah wake, Na waislam (Waumini pia wameamini hayo),wote wamemuamini Mwenye enzi Mungu, Na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake, (Na hao Waislam na Mtume wao husema)Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume yake, (Tunawaamini wote)Na husema Tumesikia na tumetii,(Tunakuomba)Msamaha Mollah wetu Na marejeo ni kwako.
Lazaru Lazaru Amka: Uislam usiwe mgeni kwako, sababu kila mmoja anazaliwa Muislam. Nini Uislam? Uislam ni ku (Surrender)una(Surrender) kwa nani kwa Mwenye enzi Mungu wako, ndio utaona watoto wote wanazaliwa wametangulia Vichwa, mara chache sana mtoto kutangulia miguu, na akifanya hivyo inakua balaa kubwa, kwa mama na walomzunguka. Na Yesu alipoulizwa na Wanafunzi wake vipi Unasali alianguka na kusujudu hivyo ndio ku(surrender) na ndivyo walivyofanya Mitume yote(Surrender to Uknown) hiyo ndio maana ya (Laaillah illah Allah)katika Uislam.
Umenitaka nichangie neno katika Ukiristo, nitachangia maneno mawili tu, nalo la kwanza ni hili la Yesu (Jesus)Mwenyewe alipomfufua Lazaru alipomwambia Lazaru Lazaru amka (Lazaru alikua kesha kufa kama siku 4 hivi, baada ya kupewa taarifa na Dada yake Lazaru ndipo alipokwenda kaburini na Kumwita kwa Sauti kwa Kusema Lazaru Lazaru Nyanyuka Uje)(John 11:43)Ilikua kama Lazaru kalala anaamshwa.
Na mimi mchango wangu ni huu wa kuamsha (Wakorinto 6:10) "Hakuna yoyote ambaye ni Mwizi, au Mlevi,Mwenye kuchukua mali za watu kwa nguvu(Rushwa)Mwenye kutumia kauli za nguvu(Za kuwatisha wenzie)ambaye ataingia kwenye Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu) Tamaa ya wanaadamu sote, Na Dini zote zinazungumzia Ufalme huu, wengine wanaita Pepo, wengine wanaita Ufalme, kwani huko kila mtu atakua mfalme, lakini kwa kupitia huu Mtihani wa wewe kuwacha mambo ya uchafu ya uzinifu na ulevi na kujiweka karibu na Mwenye Enzi Mungu wako.
Sasa vipi Nakuamsha? Kuwa Mcha Mungu, usikubali tena kutoa Mshahara wako ukampa Mtu alovaa (Uniform)Maalumu akakutolee sadaka, Sadaka ya Bwana itoe Mwenyewe, kama kuna Mayatima watafute ukawape mwenyewe, kama unachangia wakapewe Maskini basi toka ukawape kwa mkono wako kwani unawajua wanapoishi, acha kufanya Biashara na Wakubwa wa Madhehebu yako, Kwani (Dini) ni Baina yako na Mungu wako(Usiweke Mjumbe kati yake) Jiulize kwanini Ulipie, kwanini maombi yako ayapeleke Mtu, Amka  uone haya maguo tunovaa ni kwa ajili ya kazi maalumu tu, Mimi na wewe kwa Baba hatuna tafauti, sote tuko sawa kama ananisikia mimi na ana uwezo ule ule wa kukusikia wewe. Endelea part 3


LAZARU LAZARU AMKA PART 3

Asalaam Aleiykum

Sasa ushaamka huna haja tena ya kutenda Dhanbi ikisha ukenda kumuhadithia Mtu, Uungama kwa Mungu wako wewe Mwenyewe, huna haja ya kutia pesa kwenye kisanduku ili usamehewe, Baba anasamehe Bure, kinachotakiwa ufanye mawasiliano naye binafsi baina ya wewe na yeye (Amka Usiku Uungame Ewe Baba hakika nimetenda makosa na wewe tu ndiye uyajuae, na hakuna mwengine anasamehe makosa isipokuwa wewe, basi kwa hilo naomba msamaha wako sitorejea tena, hiyo ndio ahadi ninayoweka baina yangu na wewe Mungu wangu).
Na hiyo ndio (Sipiritual Path) ya kuifata, na nyengine zote ni nyenzo (Fake) za kutengeneza utajiri na hivi na vile, Na Lazaru wapo katika kila Dini, na wengi tu Malazaru na huu ndio ukweli lazima usemwe, utaona katika Dini zote pengine mtu anatubu kwa siku tatu tu ndio keshakua Mcha Mungu, mpenzi wa Mungu, ndio keshatubu na kusamehewa, anakua kasisi wa kulinda Madhehebu yake, ana msimamo mkali, anaonesha shahada ya kusamehewa, nakwambia ndugu yangu ondosha tamaa hiyo, kusamehewa kwanza lazima ubadilike, na mabadiliko lazima yatokee ndani, sio nje kwa ajili ya kuonesha watu sasa mimi Mtu mzuri, kumbe sawa sawa na Paka aloikamata (Tasbih) ya Dagaa, ikawa Panya wanaona huyu sasa kapona, kaacha kula hata Samaki, (Tasbih) yake vichwa vya samaki, lakini panya wanajiuliza mbona tunapungua kidogo kidogo, ndio utaona mpaka leo panya wameamka wanamkimbia Paka.
Lazaru Lazaru na wewe amka useme (Enough)Makanisa yanatosha, Miskiti inatosha, sasa tulishe Maskini, tuwalishe Mayatima na Wajane na wale wote wasokua na uwezo, hayo ndio maamrisho ya Mwenye enzi Mungu.
Na kumbuka huwezi kuamka ukabadilika mpaka uanze mazoezi ya kwenda (Beyond) ya hayo mambo ulokusanya kwenye Umri wako, Yepi, ondoa kwenye Moyo wako Chuki, Hamaki, kupenda Rushwa, Maasi kama vile ya (Ngono)na mengine unayajua yote lazima utafute njia ya kuyafuta kwenye Akili yako hapo ndipo utapata kuamka.
Na Mchango wangu wa pili utakua ule wa (Yesu) alipowaambia Mmoja wa wafuasi pale  watu wa Mji walipokuja na kumwambia Baba yenu amekufa twendeni mkamzike,(Yesu) akajibu hakuna haja, Maiti watamzika maiti mwenzao, Hapo alitumia mfano mzuri sio kuwa uwapuuze Familia yako ila alitumia neno hilo kukumbusha wito wa Mwenye enzi Mungu unakuja mwanzo, na ikiwa unataka kuokoka basi waache maiti watamzika maiti mwenzao, sababu hawataki mabadiliko, hawataki kufata ukweli, hawataki nuru iwamurike, mimi binafsi najaribu kuwaita marafiki zangu na walo karibu yangu, Lazaru Lazaru Amka, nitizameni mimi nini kimetokea juu yangu, jee niko kama zamani au nimebadilika lakini wote bado wamelala.
Naziona Tabia zao za miaka 30 ilopita ndio zilezile kama (Mbio za Mwenge) ndio nikikutana nao inabidi wananipa kazi nimtizame huyu mtu wa aina gani halafu na mimi nijirudishe kwenye hiyo aina ili tupate kuwa (Level)Moja, akizungumza mpira na mimi nakua mchezaji, ni tabu sana kila mara kujibadilisha lakini inabidi kwa kuwa unakutana na Lazaru wengi, kila mmoja kafa kitabia ndio yesu akatumia fumbo waache watazikana wenyewe kwa wenyewe, wachache sana wanoamka, wachache sana wanoigundua siri hii ya muamsho wa Lazaru na kuufata.
Na mimi kazi yangu kubwa ni kuamsha watu na kuwafahamisha fanya hivi na vile utaamka, utapata manufaa haya na yale, utapata kujijua kuwa wewe ni Roho na ufate maamrisho ya Kiroho ili uwe karibu na Mungu wako. Kwa hiyo Neno langu sasa usikubali kubakia Maiti, fanya kuamka mwenyewe, Ukiristo unakataza Ulevi, unakataza uzinifu, unakataza kutembea uchi, unakataza kudhulumu unataza yale yote yanokatazwa kwenye Uislam kwa hiyo ndio maana unaona maneno yangu yanakuvutia na kufanya usome maandiko yangu, naomba endelea kufanya hivyo utapata faida kubwa ya kuamka, ama ukiendelea kulala na mimi nitasema wacha Wafu wamzike Mfu mwenzao.

Sunday, August 17, 2014

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 4

Asalaam Aleiykum

Tunaendelea na uchambuzi wetu wa elimu mbili hizi na leo tukiwa tunaishi katika aya ya 72 mpaka mwisho wa safari hiyo alokwenda Mja mwema (Khidhir na Na Nabii Musa a.s).

قَالَ أَلَمۡ أَقُلۡ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِىَ صَبۡرً۬ا 
Akasema sikukwambia hutoweza kuvumilia kuwa pamoja na mimi.
Hivi ndivo wafanyavyo wanafunzi wote hawana subira, wanataka jawabu lije haraka haraka, wajue haraka hakuna kusubiri, mtu akikosa kazi au kama hajapata cheo, anakua mkali hasira zinamshika hana subira, lau angerudi kwenye jukwaa la subira pengine angepata jawabu tumekunyima kukupa hichi na kile kwa sababu wewe utakua chanzo cha hichi na kile,tunakunusuru wewe na wengine hali kadhalika.

قَالَ لَا تُؤَاخِذۡنِى بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرۡهِقۡنِى مِنۡ أَمۡرِى عُسۡرً۬ا 
(Musa a.s) Akasema usinichukulie kwa niliyo yasahau wala usinipe uzito kwa jambo langu.
Haijambo Nabii Musa kakubali kuwa kasahau, kajigundua katumia akili yake, basi akaomba asipewe uzito,(asikataliwe kuwa mwanafunzi)asije kwa kusahau huko kukamkosesha ujuzi wa hekima.

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا لَقِيَا غُلَـٰمً۬ا فَقَتَلَهُ ۥ قَالَ أَقَتَلۡتَ نَفۡسً۬ا زَكِيَّةَۢ بِغَيۡرِ نَفۡسٍ۬ لَّقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـًٔ۬ا نُّكۡرً۬ا 
Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana (Yule mja mwema)akamuua, Musa a.s akasema hee umemuua Mtu asiyekua na kosa na wala hakuua, ama hakika umefanya jambo baya kabisa.
Uwezo wa Mwenye enzi Mungu ni mkubwa lakini waso hekima hawafahamu kabisa, unaweza kuona pahala labda mnaonewa kumbe hiyo ndio inakua sababu ya nyinyi kupata nguvu kuyashinda maonevu hayo, watu watasema ilikuaje kafa wakati alikua haumwi chochote, alikua mzima, au kwanini wanamuua bure hiyo ndiyo inakua tafsiri  ya yule asiyekua na hekima, lakini mwenye hekima anajua siri ya kwanini ikawa hivyo, anajua nikifa mie ni sababu ya wenzangu kushika nafasi zao, ushapita vifo vingi ambavyo sasa wenzio wameshika nafasi zako, na wewe umebaki na kaburi limeandikwa (Rest in peace)Fulani, wewe ulikua mtoto, ukawa kijana vyote vifo, huwezi kufanya mambo kadhaa uliyokua unayafanya nyuma, basi  sasa umefika wakati uwachie ngazi usisubiri mpaka akatokea mtu kukusukuma kwa ajili ya kuendelea kufanya kwako ufisadi.

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 5

Asalaam Aleiykum

قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكَ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِىَ صَبۡرً۬ا 
Akasema jee sikukwambia kwamba hakika wewe huwezi kuvumilia kuwa pamoja namie.
Siku zote haraka zetu zinatuponza, hatuna subira, na ukitaka kujifunza kwa Mja mwenye Hekima lazima uwe na subira, lazima uvumilie mara nyengine unaweza kuambiwa kitu ili utizamwe subira yako ikoje , jee unaweza kuyajua mambo ya akhera ukayavumilia.

قَالَ إِن سَأَلۡتُكَ عَن شَىۡءِۭ بَعۡدَهَا فَلَا تُصَـٰحِبۡنِى‌ۖ قَدۡ بَلَغۡتَ مِن لَّدُنِّى عُذۡرً۬ا 
(Nabii Musa a.s)Akasema nikikuuliza kitu chochote baada ya haya usifatane na mimi, kwani umeshakwisha pata udhuru kwangu.
Daima anayetaka kujifunza anakua shujaa, akitaka mwache anifundishe hataki basi, lakini mie ndio nishamwambia, ukimuona Mtu ana dalili hizo unajua moja kwa moja hapa pana matatizo, huyu hataki kujifunza, ila anataka adokoe kidogo kisha huyo akaanze kubishana, anatafuta elimu za fujo, anatoa nyudhuru yoyote ile aoneshe kuwa Mkufunzi mwenyewe hajui kitu.

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَيَآ أَهۡلَ قَرۡيَةٍ ٱسۡتَطۡعَمَآ أَهۡلَهَا فَأَبَوۡاْ أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيہَا جِدَارً۬ا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُ ۥ‌ۖ قَالَ لَوۡ شِئۡتَ لَتَّخَذۡتَ عَلَيۡهِ أَجۡرً۬ا 
Basi wakatoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja wakawaomba watu wake wawape chakula nao wakakataa kuwakaribisha, hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka,(Yule Mja mwema)akausimamisha(Nabii Musa a.s)akasema ungelitaka ungechukua ujira kwa hili.
Ukiwa huna Hekima unafanya mambo kwa kuchupia chupia, hujui unafanya kheri au shari, bado upo gizani huwezi kujua mbele kuna nguzo au shimo, unakua unatenda mambo kimikasa unataka kutoa sadaka baada ya kualika maskini waje kula unaalika matajiri. Wewe unapanga yako na Mungu ana maamuzi yake.

قَالَ هَـٰذَا فِرَاقُ بَيۡنِى وَبَيۡنِكَ‌ۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأۡوِيلِ مَا لَمۡ تَسۡتَطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرًا 
(Yule Mja Mwema)Akasema huku ndiko kufarikiana baina ya mimi na wewe, Hivi sasa nitakwambia hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavumilia.

أَمَّا ٱلسَّفِينَةُ فَكَانَتۡ لِمَسَـٰكِينَ يَعۡمَلُونَ فِى ٱلۡبَحۡرِ فَأَرَدتُّ أَنۡ أَعِيبَہَا وَكَانَ وَرَآءَهُم مَّلِكٌ۬ يَأۡخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصۡبً۬ا 
Ama ile jahazi ilikua ya Maskini za Mungu wafanyao kazi baharini, nilitaka kuiharibu kwani nyuma yao alikuwako Mfalme anaghusubu(Anachukua)majahazi yote.
Hiyo ndio Elimu ya Akhera, inafundisha (Future) itatokea nini, au tuendako kukoje, na hapo kuna mafundisho makubwa pengine na wewe yanakugusa. Basi endelea part 6 upate kuyajua.

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 6

Asalaam Aleiykum

Ama hiyo Jahazi ilikua ya Maskini, Na hivi ndio Serekali zetu hususan za Kiafrica zinavofanya, Viongozi wote wanageuka wafalme na watendaji wao wanageuka kuwa manokoa(Machifu)ikisha wanachukua Mali za Maskini, Maskini hawana haki hata za kusema, kila Msomi au Mtu mwenye cheo Mfalme kazini kwake, ukifanya kazi serekalini unadokoa Mali ya Umma, wachache sana wanoepuka na jambo hilo, basi ikiwa katika miongoni mwa wachukuaji Mali ya Maskini adhabu za Mollah hazina shaka zitakufika, kwani Maskini wanahuzunika na kusema, wale wana magari makubwa makubwa, wanabadilisha mboga kila siku, wanapata wapi pato hilo na sisi hata hicho chakula kukipata upigane vita vya kweli ndio tonge iende kinywani.
Hivyo ndio wafanyavo Wafalme wetu wanawakalia Raia nyuma na kuwadhulumu haki zao, Na akitokea Mtu na kutaka kutoboa Siri zenu na kuinusuru mali ya maskini, huyo ndio anakua adui wenu, mnamtengenezea na kesi ili mumtie ndani ili asizikere mbinu zenu na kutoboa masikio ya maskini wakaanza kusikia maovu yanotendeka, na yoyote yule ni Mfalme awe katibu, mfanya biashara midamu unawadhulumu wanyonge juwa na wewe huna salama.

وَأَمَّا ٱلۡغُلَـٰمُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤۡمِنَيۡنِ فَخَشِينَآ أَن يُرۡهِقَهُمَا طُغۡيَـٰنً۬ا وَڪُفۡرً۬ا 
Ama yule kijana, wazazi wake walikua Waislamu kamili, tukahofia kwamba asije akawapelekea(Wazee hao) katika uasi na ukafiri.
Yanaendelea mafunzo haya kuwajulisha enyi wazazi msiwapende watoto wenu mkawa mnawaridhia mpaka ikafikia mnajua huyu analeta haramu na nyinyi mnachukua bila wasiwasi, wakakufanyeni mpaka mkamuasi Mollah wenu, pengine ujanani mefanya mema mtoto ndio anakulazimisheni mfanye mambo ya kikafiri, Elimu ya akhera imechanganywa na ya dunia ili kukupeni tahadhari ya baadae.

فَأَرَدۡنَآ أَن يُبۡدِلَهُمَا رَبُّہُمَا خَيۡرً۬ا مِّنۡهُ زَكَوٰةً۬ وَأَقۡرَبَ رُحۡمً۬ا 
Basi tulitaka Mollah wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika na aliye karibu zaidi kwa huruma.
Usiwe na huzuni hata huyo mtoto akisema mie sikusaidii mpaka ufanye hivi na vile, kataa usikubali, fanya utiifu kwa Mollah wako basi atakuletea japo mtoto wa Jirani akusaidie, akuonee huruma na kuwa karibu na wewe kuliko huyo ulomzaa, hii ndiyo Elimu ya akhera inavofundisha ondoa huzuni.


وَأَمَّا ٱلۡجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَـٰمَيۡنِ يَتِيمَيۡنِ فِى ٱلۡمَدِينَةِ وَكَانَ تَحۡتَهُ ۥ كَنزٌ۬ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَـٰلِحً۬ا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبۡلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسۡتَخۡرِجَا كَنزَهُمَا رَحۡمَةً۬ مِّن رَّبِّكَ‌ۚ وَمَا فَعَلۡتُهُ ۥ عَنۡ أَمۡرِى‌ۚ ذَٲلِكَ تَأۡوِيلُ مَا لَمۡ تَسۡطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرً۬ا 
Na Ama huo ukuta ulikua wa Vjana wawili mayatima kule mjini, Na chini yake ilikuwako khazina yao, Na baba yao alikuwa ni Mtu mwema, Basi Mollah wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni Rehma itokayo kwa Mollah wako mlezi, wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu, hiyo ndio tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria.
Na Ama ukuta umejengwa sababu ya baba yao tu alikua mtu mwema, Sasa nini habari yetu sisi kama mtajenga Nchi yenu kwa uadilifu na haki, kwa misingi na mazingira ya kidini, pengine hapo mlipo popote pale wakiishi watu wema, na sasa mshakua watu wazima (Gas) inajitokeza, mafuta yanamiminika, mnatakiwa sasa kuyachimba wenyewe, kwanini hamshikamani mkaleta umoja ili kunusuru magonvi ambayo Elimu ya akhera ishatubashiria, kama mtagombea khazina basi magonvi yakianza hayatomalizika daima, kila mmoja achukue khazina yake muishi kwa salama, natoa tahadhari msidhani mtamtoa ngombe mmoja ndio awe kafara, bali kuna hatari ya kutoka zizi zima liwe ndio kafara ya hiyo khazina, na hapa ndio mwisho wa uchambuzi wangu wa Elimu ya Dunia na Akhera.

Sunday, August 3, 2014

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 1

Asalaam Aleiykum

Limekuja swali Muulizaji kauliza anataka kujua kama iko tafauti ya Elimu ya Dunia na Elimu ya Akhera, Na Jawabu lake nimelijibu hivi, Naam tafauti ipo japokua Elimu ni hiyo hiyo moja,  tafauti yake Elimu ya Dunia (Ni Past Education)Na Elimu ya Akhera(Ni Future Education). Basi kwanza kabla ya kwenda huko mbali tuijue nini Elimu?.
Elimu ni nyenzo au mjumbe anokutoa kwenye kiza na kukupeleka kwenye Taa, Na kwa Maana hiyo lazima wewe uko pahala umekaa, na hapo pahali wewe yaonekana huwezi kutumia macho yako ukaona ndio lazima upelekwe kwa daktari wa macho akuangalie, akuoneshe hii A, hii B, na hii C. Lakini ungekua unaona basi huna haja ya kupelekwa kwa Daktari, na wako wachache wanatoka wenyewe kwenye kiza na kwenda kwenye Nuru.
Na hivi sasa Wanasayansi wametengeneza Miwani unaona ukiwa kizani bila ya matatizo, Na hiyo ndio sawa na Elimu wewe mwenyewe unaishi ndani ya hiyo Elimu, Kila kitu kimezungukwa na Elimu,  tafauti hii ya Dunia ni ya (Copy) au kama nilivyo ita mwanzoni ya (Past) au niseme (Dead education) kwanini nikaita imekufa sababu imeandikwa kwenye mabuku, mwalimu wako kasoma ikisha kakusomesha wewe, au mtu kapata mafundisho ikisha kakufundisha wewe, kila kitu unachosoma wenzio washasoma kabla yako, sio kipya kabisa fani yoyote ile wewe sio wa mwanzo, hiyo ndio Elimu ya Dunia ambayo mifano yake imetajwa Mpaka kwenye Quraan, kama zilivotajwa kwenye sura ya Rahman kuhusiana na Bahari mbili zisizoingiliana na mengi mengineyo ya Elimu za Kidunia.
Halafu kuna Elimu ya Akhera , hii ni Elimu ya (Future) ijayo, hii haisomwi, ina njia moja tu nayo kuijua, lakini huko kujua unatakiwa uwe na jitihada kubwa kwa sababu kujua sio sawa na kusoma. Kusoma utakwenda kwa Mwalimu, utakwenda kwa Sheikh, wote watakusomesha, lakini kujua lazima ukae na anaejua upate kuona kajua vipi ili apate kukufundisha na wewe mbinu za kujua, lazima uwe karibu akupe ujuzi wa kuona gizani, mabuku hapo hayafai, haitakiwi (Tuition)hapo, sasa huyu unokaa nae kwani yeye ana nini?.
Yeye anakua kapata kitu cha kumuwezesha kuona pande zote mbili za Elimu ya Dunia na ile ya Akhera, kumbuka nyote mnaona lakini tafauti yake ni ya (Level) Ya muono wenyewe, kenda zaidi ya kuona na kabahatika kwenda (Beyond Education) Na ukenda (Beyond Education) unakua hujenda kokote ila umerejea kwenye hiyo (Source)ya (Education) Ambayo ndio hiyo (Inteligence).
Nini (Inteligince)? Ukiniuliza mimi nitakwambia (Inteligence) ni Rehma, Na Rehma hii ya (Inteligence)kila Mtu kabarikiwa kuwa nayo, isipokua ina (Level) mbili, ya kwanza inakua wazi haina kipingamizi chochote, kama ilivokuja ndivo inavotumika, Na ya pili inapata kizingiti cha Elimu yako ya Dunia una (Block Inteligence) haifanyi kazi tena kama ilivo sasa mpaka hesabu unafanyiwa na (Computer) huwezi hata kufanya hesabu ya kujumuisha.
Kwa hiyo utaona Baina ya hiyo (Inteligence) kuna hizo tafauti mbili za Elimu ya Dunia na ya Akhera, (Inteligence) ndio inokusaidia uzipate elimu mbili hizo. Na hiyo (Inteligence) yenyewe haina (Past) au (Future) ni huu wakati tulonao ndio wakati wa hiyo Rehma ya (Inteligence) ukirudi (School) utamiss na ukisubiri Akhera utakua umechelewa, unatakiwa Elimu hizo zote mbili uzipate sasa hivi ndio ziwe na manufaa na wewe,yepi ? hii ya dunia ikupatie mkate wako wa kila siku hapa Ulimwenguni, na hiyo ya Akhera ikakupatiea hayo uliyopewa ahadi kuwa utayapata. Na hapo ndio wacha nikuchukue kwenye safari ilojaa hiyo (Inteligence) au Rehma au Tuite Hekima ilotokeya kwa hao walokwenda na wewe utofatia kwenda katika safari yako yoyote ulokusudia.
Endelea part 2

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 2

Asalaam Aleiykum

Katika Safari hii unaweza kushikwa na hamu ya kutaka kujua haraka haraka, kwa hiyo chuku mizigo yako ya Fikra upate kuichambua Safari hii ili upate kujua Jee kweli hapa kuna jawabu la Elimu ya Dunia na Akhera?
Basi nakupeleka mpaka pale kwenye safari maarufu alokwenda Nabii Musa a.s na kijana wake ambaye aliyemuona samaki akirejea Baharini wakati kashapikwa, pengine na wewe utaambulia machache katika maajabu hayo, kumbuka tuko kuchambua jawabu la Elimu ya Dunia na Akhera, na tunalipata jawabu letu kwenye sura ya Kahf aya ya 60 na kuendelea.
وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَٮٰهُ لَآ أَبۡرَحُ حَتَّىٰٓ أَبۡلُغَ مَجۡمَعَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ أَوۡ أَمۡضِىَ حُقُبً۬ا 
Na(Wakumbushe)Musa alipomwambia kijana wake, Nitaendelea tu kwenda mpaka nifike katika maungano ya Bahari mbili, au niendelee karne na karne.
Kumbuka Nabii Musa a.s anamwambia kijana wake kuwa anakwenda kwenye Maungano ya Bahari mbili, yeye mwenyewe hapajui na huyo kijana hapajui, lakini kuna Elimu ya Dunia imewaambia hapa pahala pako, na akasema Musa a.s (Na hata kama hakuna sehemu hii basi nitakwenda karne na karne ili kupatafuta, hapo unafundishwa jitihada na wala usikate tamaa,usije kuchoka kujifundisha au kusoma(Sasa mwenyewe amua hiyo jitihada ni elimu ya dunia au ya akhera na kwanini akasema karne mpaka karne)?.
فَلَمَّا بَلَغَا مَجۡمَعَ بَيۡنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ سَرَبً۬ا 
Basi walipofika wote wawili(Hapo pahala)zinapoungana (Bahari mbili)walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kwenda baharini, hali ya kuwa inafanya Alama.
Hapo kuna maajabu na ndani yake kuna mfano, kuna wito na mafunzo ya hali ya juu kwa kitendo cha miujiza ya samaki huyo, kwanza kabisa inatufunza vipi akili ilivokua na tabia ya kusahau, vipi Akili ilivokua haijui mambo ya (Ghaib)hawajagundua hata hizo Bahari mbili kama zipo mbele yao,ndio maana samaki akawa anaacha alama,kumbuka alama pia ni mafundisho, ndio maana hata ukiendesha gari unaekewa hapa (No Entry) Nk .
فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَٮٰهُ ءَاتِنَا غَدَآءَنَا لَقَدۡ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبً۬ا
Na Walipofika mbele (Nabii Musa a.s) alimwambia kijana wake tupe chakula chetu cha asubuhi, maana tumepata uchofu katika safari yetu hii.
قَالَ أَرَءَيۡتَ إِذۡ أَوَيۡنَآ إِلَى ٱلصَّخۡرَةِ فَإِنِّى نَسِيتُ ٱلۡحُوتَ وَمَآ أَنسَٮٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيۡطَـٰنُ أَنۡ أَذۡكُرَهُ ۥ‌ۚ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ عَجَبً۬ا 
Akasema unaona pale tulipopumzika katika mlima, basi hapo nimesahau(Kukwambia)yule Samaki, Na hakuna aliyenisahaulisha isipokua Shetani, nisikumbuke, Naye (Huyo Samaki)akashika njia yake Baharini kwa njia ya Ajabu.
Akili zetu zinavo sahau hata umuone samaki anashika njia anarudi Baharini wewe hukumbuki, Hiyo ndio Elimu ya Dunia unayopewa School , leo ukiulizwa ulisomeshwa nini ushasahau, ila umebaki na Samaki wako kwenye (Frame)kutujulisha na wewe ulipita baharini, Na vizuri tumekumbushwa Bahari mbili, na sisi tumo tunachambua elimu mbili, ya Dunia na ya Akhera, kwa hiyo na wewe unatundika (Certificate)kuonesha umepata Elimu ya Dunia, lakini nini habari yako wewe kuhusiana na Elimu ya Akhera?. Ndio unapewa wewe huo mfano wa Samaki alorejea Baharini huku akiwacha Alama, huyu Samaki anatufundisha kuwa nyinyi mmesahau mlipotoka kwa hiyo rejeeni kwenye hiyo (Source) ya Elimu ili mpate faida kubwa kubwa,na hiyo ndio maana ya alama kuwa nyinyi iko sehemu mliyotokea, kwa hiyo rejeeni ili Mpate hiyo Rehma ya (Inteligence) ndio maana huyo Samaki akarejea japokua kashapikwa, na unaambiwa na wewe japokua una Elimu yako rejea haraka upate na Elimu ya Akhera.
قَالَ ذَٲلِكَ مَا كُنَّا نَبۡغِ‌ۚ فَٱرۡتَدَّا عَلَىٰٓ ءَاثَارِهِمَا قَصَصً۬ا 
(Musa a.s)Akasema hapo ndipo tulipokua tunapataka,Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia (ile ile).
Na wewe ndio unatakiwa urudi kufata njia ile ile,urejee ulikotoka, umesahau kuwa umetokea utotoni, ikisha ukapita ujanani, kumbuka wakati ule ulikua na mawazo, ulikua na Elimu (No)ulikua unafanya mambo yako kutumia (Inteligence)japokua mengine yalikua na madhara lakini haijambo ulikua karibu na (Source)lakini umefikia sasa uzeeni umejaa makengele ya mawazo na ukibaki hivyo hivyo huwezi kuipata hiyo Hekima.
Endelea part 3

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 3

Asalaam Aleiykum

فَوَجَدَا عَبۡدً۬ا مِّنۡ عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَـٰهُ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا وَعَلَّمۡنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمً۬ا 
Basi wakamkuta Mja katika waja wetu, Tuliyempa Rehma kutoka kwetu(Inteligence)na tuliyemuelimisha ilmu zinazotoka kwetu. Kutoka kwa Mollah wako ndiko unakofundishwa elimu zote mbili, ukiwa makini unaweza kuzigundua, na ukaelewa kuwa mafunzo yanaendelea wakati wote, lakini sasa ushakua mjuaji husikilizi tena ile sauti ya upole inayokufundisha, na hata ukikutana na Mja anayejua jichunguze ima utaanza kwa ubishani au utatoa vitabu uanze kujifanya unajua.

قَالَ لَهُ ۥ مُوسَىٰ هَلۡ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰٓ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمۡتَ رُشۡدً۬ا 
(Nabii)Musa a.s akamwambia nikufate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa wewe.
Mtume wa Mwenye enzi Mungu kakubali kuwa hana ujuzi mbele ya Mja huyu, anaomba nikufate ili unifunze ule uongofu uliofunzwa wewe, sasa jitizame wewe umemfata nani ukamuomba akufundishe uongofu, jee unaweza Ku(surrender) ili ufundishwe uongofu, jee umemfata Mja ili akufundishe vipi utaziondoa dhiki zako za Moyo, sikioni ila ni kiburi na ushindani tu ulobakia na huku kila mmoja wetu muflis, na wanojua mafunzo ya uongofu wanaona bora nife nao kuliko nikaadhiriwa na watu hawa.

قَالَ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِىَ صَبۡرً۬ا 
Akasema(Yule Mja)hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami.
Hamuwezi kabisa kuvumilia, mkijaribiwa kidogo mara ushageuka unaanza kumkashifu anajua nini, mbona anavuta uradi kwa sauti, na hivi na vile, na huku unakosa kitu adhimu kabisa, unashindwa kufahamu kwamba elimu zengine haziko kwenye vitabu, zinapita mdomo kwa mdomo, moyo kwa moyo, Mja kwa Mja ndio unapata hayo mafunzo ya uongofu, wewe umezoea Urahisi mtu atoe mawaidha wewe usikilize, akimaliza unasahau hapo hapo, hupati mabadiliko yoyote, sababu hiyo ni elimu, na elimu inakaa kwenye (Akili) lakini mafunzo ni yenye kudumu ambayo yana kaa kwenye Roho yako.

وَكَيۡفَ تَصۡبِرُ عَلَىٰ مَا لَمۡ تُحِطۡ بِهِۦ خُبۡرً۬ا 
Na utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua vilivyo undani wake.
Huwezi kuvumilia ndio kwa hasira unasema hichi hakifai kile hakifai, sababu hujui mambo kwa undani, hujapata mafunzo ukajua kwanini tunafanya hayo tuyafanyayo, wewe hujakutana na mambo ya (Ghaib) ya huko Akhera, na sio kama yamejificha yapo, na zipo njia za kupata elimu hiyo lakini umefunikwa Akili kwa misemo ya baadhi ya watu na wamekunyima fursa ya ku(Explore)hawataki uwatafute waja wa hekima wakupe mafunzo hayo, nini kimekutokezea umebaki huna unacho jua wala huvumilii kufahamishwa undani wa hayo mambo, Na ukimkuta Sheikhe kavaa suruali unasema Aah huyu nimecheza nae hana chochote, Jiulize jee unaujua Undani?.

قَالَ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ صَابِرً۬ا وَلَآ أَعۡصِى لَكَ أَمۡرً۬ا 
(Nabii Musa a.s)Akasema Inshaa Allah Mwenye enzi Mungu akipenda utaniona mvumilivu, wala sitoasi amri yako.
Nabii Musa a.s anatufundisha tujitupe kwa Mollah wetu, hakusema tu nitavumilia bali kasema akipenda Mollah wangu, akitaka Mollah wangu, lazima ku(Surrender) wewe huna uwezo, unamtegemea Mollah wako, na wala sitoasi amri yako, sitotukana Masheikh, sitokashifu wanazuoni hata kama walikosea, kwa ajili mimi nataka kujua mafunzo ya Mollah wangu basi utaniona maridhia juu yako,Na (Kumbukeni hiyo kusema kwetu Inshaa Allah ambayo sasa tunakatazwa tusiseme basi sisi wa mwanzo kutufundisha neno hilo ni huyo msemezwa na Mwenye enzi Mungu nabii Musa a.s na wala hatukulitunga sisi neno hilo kama aya inavoonesha hapo juu).

قَالَ فَإِنِ ٱتَّبَعۡتَنِى فَلَا تَسۡـَٔلۡنِى عَن شَىۡءٍ حَتَّىٰٓ أُحۡدِثَ لَكَ مِنۡهُ ذِكۡرً۬ا  
Akasema (Yule Mja Mwema)basi ukinifata usinulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia.
Inatakiwa subira kumfata mwenye Hekima, hataki msimamo wako wala elimu yako ulonayo, anachotaka kwako subira ikiwa mwaka miaka, usipite ukaanza kuuliza uliza kwa mitego na kutafuta makosa(huku una majawabu yako ya Sheikh fulani kichwani, sasa kama una jawabu ya nini unauliza swali?) utakosa mafunzo, subiri mapaka uhadithiwe, hivyo ndio mafunzo ya Akhera yanavopatikana, sio haraka haraka ukakae kwa Shekhe siku tatu unyanyuke na wewe Shekhe, vipi wewe utakua sawa na yule alokaa miaka 9 anafunzwa kidogo kidogo mpaka akahitimu, usipite ukauliza mbona hivi, mbona hadith sio sahihi, sasa ushaita hadith vipi itakua sahihi, inaweza kuwa sahihi au ikaongezwa majambo (Who know)?ndio maana ukaambiwa hadith, subiri mpaka uhadithiwe tena una hiari yako kukubali au kukataa, Na kumbuka kuambiwa ni neno, lakini kutajiwa ni mafunzo ambayo yanaishi na wewe milele.

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِى ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَا‌ۖ قَالَ أَخَرَقۡتَہَا لِتُغۡرِقَ أَهۡلَهَا لَقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـًٔا إِمۡرً۬ا 
Basi wakatoka wawili hawa hata walipopanda jahazi (Yule Mja Mwema)akaitoboa(Nabii Musa a.s)akasema unaitoboa uwazamishe watu wake, hakika umefanya jambo baya.
Hivi ndio sote tuonavyo kwa kutumia Akili, Akili inakufanya utafsiri mambo vyengine kabisa, unapita kusema mambo huyajui mwanzo wake wala mwisho wake, ni vigumu kwenu kuelewa au kujifunza elimu za Akhera sababu mshafunga milango yenu kwa kufuli za daima, huwezi kujua hekima ya gari kuharibika unapotaka kuanza safari, pengine njiani unanusuriwa na ajali, Inshaa Allah zaidi tutendelea wiki ijayo kwa leo tumalizie hiyo aya ya 71, na tutaendelea na part 4,5,6 kwa uchambuzi zaidi.