Sunday, August 17, 2014

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 4

Asalaam Aleiykum

Tunaendelea na uchambuzi wetu wa elimu mbili hizi na leo tukiwa tunaishi katika aya ya 72 mpaka mwisho wa safari hiyo alokwenda Mja mwema (Khidhir na Na Nabii Musa a.s).

قَالَ أَلَمۡ أَقُلۡ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِىَ صَبۡرً۬ا 
Akasema sikukwambia hutoweza kuvumilia kuwa pamoja na mimi.
Hivi ndivo wafanyavyo wanafunzi wote hawana subira, wanataka jawabu lije haraka haraka, wajue haraka hakuna kusubiri, mtu akikosa kazi au kama hajapata cheo, anakua mkali hasira zinamshika hana subira, lau angerudi kwenye jukwaa la subira pengine angepata jawabu tumekunyima kukupa hichi na kile kwa sababu wewe utakua chanzo cha hichi na kile,tunakunusuru wewe na wengine hali kadhalika.

قَالَ لَا تُؤَاخِذۡنِى بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرۡهِقۡنِى مِنۡ أَمۡرِى عُسۡرً۬ا 
(Musa a.s) Akasema usinichukulie kwa niliyo yasahau wala usinipe uzito kwa jambo langu.
Haijambo Nabii Musa kakubali kuwa kasahau, kajigundua katumia akili yake, basi akaomba asipewe uzito,(asikataliwe kuwa mwanafunzi)asije kwa kusahau huko kukamkosesha ujuzi wa hekima.

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا لَقِيَا غُلَـٰمً۬ا فَقَتَلَهُ ۥ قَالَ أَقَتَلۡتَ نَفۡسً۬ا زَكِيَّةَۢ بِغَيۡرِ نَفۡسٍ۬ لَّقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـًٔ۬ا نُّكۡرً۬ا 
Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana (Yule mja mwema)akamuua, Musa a.s akasema hee umemuua Mtu asiyekua na kosa na wala hakuua, ama hakika umefanya jambo baya kabisa.
Uwezo wa Mwenye enzi Mungu ni mkubwa lakini waso hekima hawafahamu kabisa, unaweza kuona pahala labda mnaonewa kumbe hiyo ndio inakua sababu ya nyinyi kupata nguvu kuyashinda maonevu hayo, watu watasema ilikuaje kafa wakati alikua haumwi chochote, alikua mzima, au kwanini wanamuua bure hiyo ndiyo inakua tafsiri  ya yule asiyekua na hekima, lakini mwenye hekima anajua siri ya kwanini ikawa hivyo, anajua nikifa mie ni sababu ya wenzangu kushika nafasi zao, ushapita vifo vingi ambavyo sasa wenzio wameshika nafasi zako, na wewe umebaki na kaburi limeandikwa (Rest in peace)Fulani, wewe ulikua mtoto, ukawa kijana vyote vifo, huwezi kufanya mambo kadhaa uliyokua unayafanya nyuma, basi  sasa umefika wakati uwachie ngazi usisubiri mpaka akatokea mtu kukusukuma kwa ajili ya kuendelea kufanya kwako ufisadi.

No comments:

Post a Comment