Sunday, August 24, 2014

LAZARU LAZARU AMKA PART 3

Asalaam Aleiykum

Sasa ushaamka huna haja tena ya kutenda Dhanbi ikisha ukenda kumuhadithia Mtu, Uungama kwa Mungu wako wewe Mwenyewe, huna haja ya kutia pesa kwenye kisanduku ili usamehewe, Baba anasamehe Bure, kinachotakiwa ufanye mawasiliano naye binafsi baina ya wewe na yeye (Amka Usiku Uungame Ewe Baba hakika nimetenda makosa na wewe tu ndiye uyajuae, na hakuna mwengine anasamehe makosa isipokuwa wewe, basi kwa hilo naomba msamaha wako sitorejea tena, hiyo ndio ahadi ninayoweka baina yangu na wewe Mungu wangu).
Na hiyo ndio (Sipiritual Path) ya kuifata, na nyengine zote ni nyenzo (Fake) za kutengeneza utajiri na hivi na vile, Na Lazaru wapo katika kila Dini, na wengi tu Malazaru na huu ndio ukweli lazima usemwe, utaona katika Dini zote pengine mtu anatubu kwa siku tatu tu ndio keshakua Mcha Mungu, mpenzi wa Mungu, ndio keshatubu na kusamehewa, anakua kasisi wa kulinda Madhehebu yake, ana msimamo mkali, anaonesha shahada ya kusamehewa, nakwambia ndugu yangu ondosha tamaa hiyo, kusamehewa kwanza lazima ubadilike, na mabadiliko lazima yatokee ndani, sio nje kwa ajili ya kuonesha watu sasa mimi Mtu mzuri, kumbe sawa sawa na Paka aloikamata (Tasbih) ya Dagaa, ikawa Panya wanaona huyu sasa kapona, kaacha kula hata Samaki, (Tasbih) yake vichwa vya samaki, lakini panya wanajiuliza mbona tunapungua kidogo kidogo, ndio utaona mpaka leo panya wameamka wanamkimbia Paka.
Lazaru Lazaru na wewe amka useme (Enough)Makanisa yanatosha, Miskiti inatosha, sasa tulishe Maskini, tuwalishe Mayatima na Wajane na wale wote wasokua na uwezo, hayo ndio maamrisho ya Mwenye enzi Mungu.
Na kumbuka huwezi kuamka ukabadilika mpaka uanze mazoezi ya kwenda (Beyond) ya hayo mambo ulokusanya kwenye Umri wako, Yepi, ondoa kwenye Moyo wako Chuki, Hamaki, kupenda Rushwa, Maasi kama vile ya (Ngono)na mengine unayajua yote lazima utafute njia ya kuyafuta kwenye Akili yako hapo ndipo utapata kuamka.
Na Mchango wangu wa pili utakua ule wa (Yesu) alipowaambia Mmoja wa wafuasi pale  watu wa Mji walipokuja na kumwambia Baba yenu amekufa twendeni mkamzike,(Yesu) akajibu hakuna haja, Maiti watamzika maiti mwenzao, Hapo alitumia mfano mzuri sio kuwa uwapuuze Familia yako ila alitumia neno hilo kukumbusha wito wa Mwenye enzi Mungu unakuja mwanzo, na ikiwa unataka kuokoka basi waache maiti watamzika maiti mwenzao, sababu hawataki mabadiliko, hawataki kufata ukweli, hawataki nuru iwamurike, mimi binafsi najaribu kuwaita marafiki zangu na walo karibu yangu, Lazaru Lazaru Amka, nitizameni mimi nini kimetokea juu yangu, jee niko kama zamani au nimebadilika lakini wote bado wamelala.
Naziona Tabia zao za miaka 30 ilopita ndio zilezile kama (Mbio za Mwenge) ndio nikikutana nao inabidi wananipa kazi nimtizame huyu mtu wa aina gani halafu na mimi nijirudishe kwenye hiyo aina ili tupate kuwa (Level)Moja, akizungumza mpira na mimi nakua mchezaji, ni tabu sana kila mara kujibadilisha lakini inabidi kwa kuwa unakutana na Lazaru wengi, kila mmoja kafa kitabia ndio yesu akatumia fumbo waache watazikana wenyewe kwa wenyewe, wachache sana wanoamka, wachache sana wanoigundua siri hii ya muamsho wa Lazaru na kuufata.
Na mimi kazi yangu kubwa ni kuamsha watu na kuwafahamisha fanya hivi na vile utaamka, utapata manufaa haya na yale, utapata kujijua kuwa wewe ni Roho na ufate maamrisho ya Kiroho ili uwe karibu na Mungu wako. Kwa hiyo Neno langu sasa usikubali kubakia Maiti, fanya kuamka mwenyewe, Ukiristo unakataza Ulevi, unakataza uzinifu, unakataza kutembea uchi, unakataza kudhulumu unataza yale yote yanokatazwa kwenye Uislam kwa hiyo ndio maana unaona maneno yangu yanakuvutia na kufanya usome maandiko yangu, naomba endelea kufanya hivyo utapata faida kubwa ya kuamka, ama ukiendelea kulala na mimi nitasema wacha Wafu wamzike Mfu mwenzao.

No comments:

Post a Comment