Asalaam Aleiykum
Sheria zote ni za Mwenye Enzi Mungu, ndio Maana mimi binafsi siwezi kuishambulia (Biblia)ile ya kweli ambayo haikuongezwa ufundi ndani yake kwa sababu najua asilimia 75% ya (Biblia)imo ndani ya Quraan au kinyume chake, Ndio Maana katika Quraan kuna andiko la aya ya 285 sura ya (Baqarah) linalosema"Mtume(Muhammad s.a.w)ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mollah wake, Na waislam (Waumini pia wameamini hayo),wote wamemuamini Mwenye enzi Mungu, Na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake, (Na hao Waislam na Mtume wao husema)Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume yake, (Tunawaamini wote)Na husema Tumesikia na tumetii,(Tunakuomba)Msamaha Mollah wetu Na marejeo ni kwako.
Lazaru Lazaru Amka: Uislam usiwe mgeni kwako, sababu kila mmoja anazaliwa Muislam. Nini Uislam? Uislam ni ku (Surrender)una(Surrender) kwa nani kwa Mwenye enzi Mungu wako, ndio utaona watoto wote wanazaliwa wametangulia Vichwa, mara chache sana mtoto kutangulia miguu, na akifanya hivyo inakua balaa kubwa, kwa mama na walomzunguka. Na Yesu alipoulizwa na Wanafunzi wake vipi Unasali alianguka na kusujudu hivyo ndio ku(surrender) na ndivyo walivyofanya Mitume yote(Surrender to Uknown) hiyo ndio maana ya (Laaillah illah Allah)katika Uislam.
Umenitaka nichangie neno katika Ukiristo, nitachangia maneno mawili tu, nalo la kwanza ni hili la Yesu (Jesus)Mwenyewe alipomfufua Lazaru alipomwambia Lazaru Lazaru amka (Lazaru alikua kesha kufa kama siku 4 hivi, baada ya kupewa taarifa na Dada yake Lazaru ndipo alipokwenda kaburini na Kumwita kwa Sauti kwa Kusema Lazaru Lazaru Nyanyuka Uje)(John 11:43)Ilikua kama Lazaru kalala anaamshwa.
Na mimi mchango wangu ni huu wa kuamsha (Wakorinto 6:10) "Hakuna yoyote ambaye ni Mwizi, au Mlevi,Mwenye kuchukua mali za watu kwa nguvu(Rushwa)Mwenye kutumia kauli za nguvu(Za kuwatisha wenzie)ambaye ataingia kwenye Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu) Tamaa ya wanaadamu sote, Na Dini zote zinazungumzia Ufalme huu, wengine wanaita Pepo, wengine wanaita Ufalme, kwani huko kila mtu atakua mfalme, lakini kwa kupitia huu Mtihani wa wewe kuwacha mambo ya uchafu ya uzinifu na ulevi na kujiweka karibu na Mwenye Enzi Mungu wako.
Sasa vipi Nakuamsha? Kuwa Mcha Mungu, usikubali tena kutoa Mshahara wako ukampa Mtu alovaa (Uniform)Maalumu akakutolee sadaka, Sadaka ya Bwana itoe Mwenyewe, kama kuna Mayatima watafute ukawape mwenyewe, kama unachangia wakapewe Maskini basi toka ukawape kwa mkono wako kwani unawajua wanapoishi, acha kufanya Biashara na Wakubwa wa Madhehebu yako, Kwani (Dini) ni Baina yako na Mungu wako(Usiweke Mjumbe kati yake) Jiulize kwanini Ulipie, kwanini maombi yako ayapeleke Mtu, Amka uone haya maguo tunovaa ni kwa ajili ya kazi maalumu tu, Mimi na wewe kwa Baba hatuna tafauti, sote tuko sawa kama ananisikia mimi na ana uwezo ule ule wa kukusikia wewe. Endelea part 3
No comments:
Post a Comment