Sunday, August 17, 2014

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 5

Asalaam Aleiykum

قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكَ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِىَ صَبۡرً۬ا 
Akasema jee sikukwambia kwamba hakika wewe huwezi kuvumilia kuwa pamoja namie.
Siku zote haraka zetu zinatuponza, hatuna subira, na ukitaka kujifunza kwa Mja mwenye Hekima lazima uwe na subira, lazima uvumilie mara nyengine unaweza kuambiwa kitu ili utizamwe subira yako ikoje , jee unaweza kuyajua mambo ya akhera ukayavumilia.

قَالَ إِن سَأَلۡتُكَ عَن شَىۡءِۭ بَعۡدَهَا فَلَا تُصَـٰحِبۡنِى‌ۖ قَدۡ بَلَغۡتَ مِن لَّدُنِّى عُذۡرً۬ا 
(Nabii Musa a.s)Akasema nikikuuliza kitu chochote baada ya haya usifatane na mimi, kwani umeshakwisha pata udhuru kwangu.
Daima anayetaka kujifunza anakua shujaa, akitaka mwache anifundishe hataki basi, lakini mie ndio nishamwambia, ukimuona Mtu ana dalili hizo unajua moja kwa moja hapa pana matatizo, huyu hataki kujifunza, ila anataka adokoe kidogo kisha huyo akaanze kubishana, anatafuta elimu za fujo, anatoa nyudhuru yoyote ile aoneshe kuwa Mkufunzi mwenyewe hajui kitu.

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَيَآ أَهۡلَ قَرۡيَةٍ ٱسۡتَطۡعَمَآ أَهۡلَهَا فَأَبَوۡاْ أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيہَا جِدَارً۬ا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُ ۥ‌ۖ قَالَ لَوۡ شِئۡتَ لَتَّخَذۡتَ عَلَيۡهِ أَجۡرً۬ا 
Basi wakatoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja wakawaomba watu wake wawape chakula nao wakakataa kuwakaribisha, hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka,(Yule Mja mwema)akausimamisha(Nabii Musa a.s)akasema ungelitaka ungechukua ujira kwa hili.
Ukiwa huna Hekima unafanya mambo kwa kuchupia chupia, hujui unafanya kheri au shari, bado upo gizani huwezi kujua mbele kuna nguzo au shimo, unakua unatenda mambo kimikasa unataka kutoa sadaka baada ya kualika maskini waje kula unaalika matajiri. Wewe unapanga yako na Mungu ana maamuzi yake.

قَالَ هَـٰذَا فِرَاقُ بَيۡنِى وَبَيۡنِكَ‌ۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأۡوِيلِ مَا لَمۡ تَسۡتَطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرًا 
(Yule Mja Mwema)Akasema huku ndiko kufarikiana baina ya mimi na wewe, Hivi sasa nitakwambia hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavumilia.

أَمَّا ٱلسَّفِينَةُ فَكَانَتۡ لِمَسَـٰكِينَ يَعۡمَلُونَ فِى ٱلۡبَحۡرِ فَأَرَدتُّ أَنۡ أَعِيبَہَا وَكَانَ وَرَآءَهُم مَّلِكٌ۬ يَأۡخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصۡبً۬ا 
Ama ile jahazi ilikua ya Maskini za Mungu wafanyao kazi baharini, nilitaka kuiharibu kwani nyuma yao alikuwako Mfalme anaghusubu(Anachukua)majahazi yote.
Hiyo ndio Elimu ya Akhera, inafundisha (Future) itatokea nini, au tuendako kukoje, na hapo kuna mafundisho makubwa pengine na wewe yanakugusa. Basi endelea part 6 upate kuyajua.

No comments:

Post a Comment