Sunday, August 31, 2014

MAISHA YA AKHERA PART 1

Asalaam Aleiykum

Umeishi Maisha ya Duniani mpaka sasa unayajua yalivyo, Jee unayo habari ya Maisha ya Akhera? zimekujia fikra kuwa yapo maisha mengine ambayo utakayokwenda kuishi, ni vigumu kukujia fikra hizo kwa kuwa unaishi katika hali ya kusahau katika Ulimwengu huu, ila jambo moja una hakika nalo kuwa kuna siku nitaondoka katika Dunia hii nakwenda huko pahala panapo itwa Akhera.
Japo hujui siku gani lakini kimya kimya ushajiandaa, ushakubali utaondoka, sasa kama yote hayo unayatambua kwanini hujiulizi (Adress)gani utafikia huko uendako, Sababu kubwa huwezi kui(Google)hiyo(Adress)yako ni kuogopa kwako kutokana na matukio ya matendo yako unajua fika makaazi yako yatakua si mazuri, unaogopa kuijua (Anwani)yako ilo mbaya, kwa hiyo wewe kila saa na dakika unapigana bila ya kujijua kusahau maisha haya ya Akhera, Lakini kwa kuwa unapendwa na Mollah wako kwa hiyo kupitia kwa Mtume wake s.a.w kakuletea kauli ya Hadith ambayo inasema "Kahudhurieni Makaburi yakukumbusheni Akhera".
Hapo kuna mambo makubwa yakuzingatiwa na mwanaadamu, kwanza hukutakiwa uchukue chochote, hukutakiwa ukamate kitabu au umtegemee Sheikh akwambie fanya hivi au fanya vile, haitakiwi Akili ya mtu yoyote ikuamrishe kitu, bali unatakiwa wewe mwenyewe utoke iwe usiku au mchana uko mweupe huna mashiko yoyote ufanye safari ya kwenda kuhudhuria (Kaburi).
Sasa kwanini ikawa kaburi ndio likukumbushe Akhera, Kwanini hukumbuki mwenyewe, kwanza kabisa napenda uelewe Maisha yako ya Duniani yanaanzia takriban kitandani na hususan usiku, na huishia Makaburini hususan mchana na hapo ndio Daraja la wewe kuvuka kurejea huko Akhera ambako ndiko uliko tokea.
Na la pili huwezi kukumbuka kwa sababu wewe mwenyewe upo katika dunia hii unajiona unaishi lakini ushakufa kitabia, umekufa katika mazoea ya usahaulifu, umeota mizizi katika katika mazingira ya kawaida yako unavyoishi kula, kulala, kuamka kwenda kazini, kurudi nyumbani ima barazani au kwenye TV, na kesho yake hivyo hivyo huna mbadala, kawaida yako inajulikana ya mwenendo maalumu, kwa kuwa umesahau kabisa Maisha haya ya Akhera ndio unaambiwa hebu nenda "Makaburini", kahudhurie maziko, huenda asaa ukakumbuka kitu, huenda kuna kitu kikatokezea labda unaweza kukurupuka usingizini, ukaamka ghafla ukakumbuka Akhera, sasa ili ukumbuke uende vipi huko makaburini au "Mazikoni". Endelea part 2

No comments:

Post a Comment