Asalaam Aleiykum
فَوَجَدَا عَبۡدً۬ا مِّنۡ عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَـٰهُ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا وَعَلَّمۡنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمً۬ا
Basi wakamkuta Mja katika waja wetu, Tuliyempa Rehma kutoka kwetu(Inteligence)na tuliyemuelimisha ilmu zinazotoka kwetu. Kutoka kwa Mollah wako ndiko unakofundishwa elimu zote mbili, ukiwa makini unaweza kuzigundua, na ukaelewa kuwa mafunzo yanaendelea wakati wote, lakini sasa ushakua mjuaji husikilizi tena ile sauti ya upole inayokufundisha, na hata ukikutana na Mja anayejua jichunguze ima utaanza kwa ubishani au utatoa vitabu uanze kujifanya unajua.
قَالَ لَهُ ۥ مُوسَىٰ هَلۡ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰٓ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمۡتَ رُشۡدً۬ا
(Nabii)Musa a.s akamwambia nikufate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa wewe.
Mtume wa Mwenye enzi Mungu kakubali kuwa hana ujuzi mbele ya Mja huyu, anaomba nikufate ili unifunze ule uongofu uliofunzwa wewe, sasa jitizame wewe umemfata nani ukamuomba akufundishe uongofu, jee unaweza Ku(surrender) ili ufundishwe uongofu, jee umemfata Mja ili akufundishe vipi utaziondoa dhiki zako za Moyo, sikioni ila ni kiburi na ushindani tu ulobakia na huku kila mmoja wetu muflis, na wanojua mafunzo ya uongofu wanaona bora nife nao kuliko nikaadhiriwa na watu hawa.
قَالَ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِىَ صَبۡرً۬ا
Akasema(Yule Mja)hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami.
Hamuwezi kabisa kuvumilia, mkijaribiwa kidogo mara ushageuka unaanza kumkashifu anajua nini, mbona anavuta uradi kwa sauti, na hivi na vile, na huku unakosa kitu adhimu kabisa, unashindwa kufahamu kwamba elimu zengine haziko kwenye vitabu, zinapita mdomo kwa mdomo, moyo kwa moyo, Mja kwa Mja ndio unapata hayo mafunzo ya uongofu, wewe umezoea Urahisi mtu atoe mawaidha wewe usikilize, akimaliza unasahau hapo hapo, hupati mabadiliko yoyote, sababu hiyo ni elimu, na elimu inakaa kwenye (Akili) lakini mafunzo ni yenye kudumu ambayo yana kaa kwenye Roho yako.
وَكَيۡفَ تَصۡبِرُ عَلَىٰ مَا لَمۡ تُحِطۡ بِهِۦ خُبۡرً۬ا
Na utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua vilivyo undani wake.
Huwezi kuvumilia ndio kwa hasira unasema hichi hakifai kile hakifai, sababu hujui mambo kwa undani, hujapata mafunzo ukajua kwanini tunafanya hayo tuyafanyayo, wewe hujakutana na mambo ya (Ghaib) ya huko Akhera, na sio kama yamejificha yapo, na zipo njia za kupata elimu hiyo lakini umefunikwa Akili kwa misemo ya baadhi ya watu na wamekunyima fursa ya ku(Explore)hawataki uwatafute waja wa hekima wakupe mafunzo hayo, nini kimekutokezea umebaki huna unacho jua wala huvumilii kufahamishwa undani wa hayo mambo, Na ukimkuta Sheikhe kavaa suruali unasema Aah huyu nimecheza nae hana chochote, Jiulize jee unaujua Undani?.
قَالَ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ صَابِرً۬ا وَلَآ أَعۡصِى لَكَ أَمۡرً۬ا
(Nabii Musa a.s)Akasema Inshaa Allah Mwenye enzi Mungu akipenda utaniona mvumilivu, wala sitoasi amri yako.
Nabii Musa a.s anatufundisha tujitupe kwa Mollah wetu, hakusema tu nitavumilia bali kasema akipenda Mollah wangu, akitaka Mollah wangu, lazima ku(Surrender) wewe huna uwezo, unamtegemea Mollah wako, na wala sitoasi amri yako, sitotukana Masheikh, sitokashifu wanazuoni hata kama walikosea, kwa ajili mimi nataka kujua mafunzo ya Mollah wangu basi utaniona maridhia juu yako,Na (Kumbukeni hiyo kusema kwetu Inshaa Allah ambayo sasa tunakatazwa tusiseme basi sisi wa mwanzo kutufundisha neno hilo ni huyo msemezwa na Mwenye enzi Mungu nabii Musa a.s na wala hatukulitunga sisi neno hilo kama aya inavoonesha hapo juu).
قَالَ فَإِنِ ٱتَّبَعۡتَنِى فَلَا تَسۡـَٔلۡنِى عَن شَىۡءٍ حَتَّىٰٓ أُحۡدِثَ لَكَ مِنۡهُ ذِكۡرً۬ا
Akasema (Yule Mja Mwema)basi ukinifata usinulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia.
Inatakiwa subira kumfata mwenye Hekima, hataki msimamo wako wala elimu yako ulonayo, anachotaka kwako subira ikiwa mwaka miaka, usipite ukaanza kuuliza uliza kwa mitego na kutafuta makosa(huku una majawabu yako ya Sheikh fulani kichwani, sasa kama una jawabu ya nini unauliza swali?) utakosa mafunzo, subiri mapaka uhadithiwe, hivyo ndio mafunzo ya Akhera yanavopatikana, sio haraka haraka ukakae kwa Shekhe siku tatu unyanyuke na wewe Shekhe, vipi wewe utakua sawa na yule alokaa miaka 9 anafunzwa kidogo kidogo mpaka akahitimu, usipite ukauliza mbona hivi, mbona hadith sio sahihi, sasa ushaita hadith vipi itakua sahihi, inaweza kuwa sahihi au ikaongezwa majambo (Who know)?ndio maana ukaambiwa hadith, subiri mpaka uhadithiwe tena una hiari yako kukubali au kukataa, Na kumbuka kuambiwa ni neno, lakini kutajiwa ni mafunzo ambayo yanaishi na wewe milele.
فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِى ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَاۖ قَالَ أَخَرَقۡتَہَا لِتُغۡرِقَ أَهۡلَهَا لَقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـًٔا إِمۡرً۬ا
Basi wakatoka wawili hawa hata walipopanda jahazi (Yule Mja Mwema)akaitoboa(Nabii Musa a.s)akasema unaitoboa uwazamishe watu wake, hakika umefanya jambo baya.
Hivi ndio sote tuonavyo kwa kutumia Akili, Akili inakufanya utafsiri mambo vyengine kabisa, unapita kusema mambo huyajui mwanzo wake wala mwisho wake, ni vigumu kwenu kuelewa au kujifunza elimu za Akhera sababu mshafunga milango yenu kwa kufuli za daima, huwezi kujua hekima ya gari kuharibika unapotaka kuanza safari, pengine njiani unanusuriwa na ajali, Inshaa Allah zaidi tutendelea wiki ijayo kwa leo tumalizie hiyo aya ya 71, na tutaendelea na part 4,5,6 kwa uchambuzi zaidi.
No comments:
Post a Comment