Sunday, August 3, 2014

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 2

Asalaam Aleiykum

Katika Safari hii unaweza kushikwa na hamu ya kutaka kujua haraka haraka, kwa hiyo chuku mizigo yako ya Fikra upate kuichambua Safari hii ili upate kujua Jee kweli hapa kuna jawabu la Elimu ya Dunia na Akhera?
Basi nakupeleka mpaka pale kwenye safari maarufu alokwenda Nabii Musa a.s na kijana wake ambaye aliyemuona samaki akirejea Baharini wakati kashapikwa, pengine na wewe utaambulia machache katika maajabu hayo, kumbuka tuko kuchambua jawabu la Elimu ya Dunia na Akhera, na tunalipata jawabu letu kwenye sura ya Kahf aya ya 60 na kuendelea.
وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَٮٰهُ لَآ أَبۡرَحُ حَتَّىٰٓ أَبۡلُغَ مَجۡمَعَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ أَوۡ أَمۡضِىَ حُقُبً۬ا 
Na(Wakumbushe)Musa alipomwambia kijana wake, Nitaendelea tu kwenda mpaka nifike katika maungano ya Bahari mbili, au niendelee karne na karne.
Kumbuka Nabii Musa a.s anamwambia kijana wake kuwa anakwenda kwenye Maungano ya Bahari mbili, yeye mwenyewe hapajui na huyo kijana hapajui, lakini kuna Elimu ya Dunia imewaambia hapa pahala pako, na akasema Musa a.s (Na hata kama hakuna sehemu hii basi nitakwenda karne na karne ili kupatafuta, hapo unafundishwa jitihada na wala usikate tamaa,usije kuchoka kujifundisha au kusoma(Sasa mwenyewe amua hiyo jitihada ni elimu ya dunia au ya akhera na kwanini akasema karne mpaka karne)?.
فَلَمَّا بَلَغَا مَجۡمَعَ بَيۡنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ سَرَبً۬ا 
Basi walipofika wote wawili(Hapo pahala)zinapoungana (Bahari mbili)walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kwenda baharini, hali ya kuwa inafanya Alama.
Hapo kuna maajabu na ndani yake kuna mfano, kuna wito na mafunzo ya hali ya juu kwa kitendo cha miujiza ya samaki huyo, kwanza kabisa inatufunza vipi akili ilivokua na tabia ya kusahau, vipi Akili ilivokua haijui mambo ya (Ghaib)hawajagundua hata hizo Bahari mbili kama zipo mbele yao,ndio maana samaki akawa anaacha alama,kumbuka alama pia ni mafundisho, ndio maana hata ukiendesha gari unaekewa hapa (No Entry) Nk .
فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَٮٰهُ ءَاتِنَا غَدَآءَنَا لَقَدۡ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبً۬ا
Na Walipofika mbele (Nabii Musa a.s) alimwambia kijana wake tupe chakula chetu cha asubuhi, maana tumepata uchofu katika safari yetu hii.
قَالَ أَرَءَيۡتَ إِذۡ أَوَيۡنَآ إِلَى ٱلصَّخۡرَةِ فَإِنِّى نَسِيتُ ٱلۡحُوتَ وَمَآ أَنسَٮٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيۡطَـٰنُ أَنۡ أَذۡكُرَهُ ۥ‌ۚ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ عَجَبً۬ا 
Akasema unaona pale tulipopumzika katika mlima, basi hapo nimesahau(Kukwambia)yule Samaki, Na hakuna aliyenisahaulisha isipokua Shetani, nisikumbuke, Naye (Huyo Samaki)akashika njia yake Baharini kwa njia ya Ajabu.
Akili zetu zinavo sahau hata umuone samaki anashika njia anarudi Baharini wewe hukumbuki, Hiyo ndio Elimu ya Dunia unayopewa School , leo ukiulizwa ulisomeshwa nini ushasahau, ila umebaki na Samaki wako kwenye (Frame)kutujulisha na wewe ulipita baharini, Na vizuri tumekumbushwa Bahari mbili, na sisi tumo tunachambua elimu mbili, ya Dunia na ya Akhera, kwa hiyo na wewe unatundika (Certificate)kuonesha umepata Elimu ya Dunia, lakini nini habari yako wewe kuhusiana na Elimu ya Akhera?. Ndio unapewa wewe huo mfano wa Samaki alorejea Baharini huku akiwacha Alama, huyu Samaki anatufundisha kuwa nyinyi mmesahau mlipotoka kwa hiyo rejeeni kwenye hiyo (Source) ya Elimu ili mpate faida kubwa kubwa,na hiyo ndio maana ya alama kuwa nyinyi iko sehemu mliyotokea, kwa hiyo rejeeni ili Mpate hiyo Rehma ya (Inteligence) ndio maana huyo Samaki akarejea japokua kashapikwa, na unaambiwa na wewe japokua una Elimu yako rejea haraka upate na Elimu ya Akhera.
قَالَ ذَٲلِكَ مَا كُنَّا نَبۡغِ‌ۚ فَٱرۡتَدَّا عَلَىٰٓ ءَاثَارِهِمَا قَصَصً۬ا 
(Musa a.s)Akasema hapo ndipo tulipokua tunapataka,Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia (ile ile).
Na wewe ndio unatakiwa urudi kufata njia ile ile,urejee ulikotoka, umesahau kuwa umetokea utotoni, ikisha ukapita ujanani, kumbuka wakati ule ulikua na mawazo, ulikua na Elimu (No)ulikua unafanya mambo yako kutumia (Inteligence)japokua mengine yalikua na madhara lakini haijambo ulikua karibu na (Source)lakini umefikia sasa uzeeni umejaa makengele ya mawazo na ukibaki hivyo hivyo huwezi kuipata hiyo Hekima.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment