Sunday, August 17, 2014

ELIMU YA DUNIA NA AKHERA PART 6

Asalaam Aleiykum

Ama hiyo Jahazi ilikua ya Maskini, Na hivi ndio Serekali zetu hususan za Kiafrica zinavofanya, Viongozi wote wanageuka wafalme na watendaji wao wanageuka kuwa manokoa(Machifu)ikisha wanachukua Mali za Maskini, Maskini hawana haki hata za kusema, kila Msomi au Mtu mwenye cheo Mfalme kazini kwake, ukifanya kazi serekalini unadokoa Mali ya Umma, wachache sana wanoepuka na jambo hilo, basi ikiwa katika miongoni mwa wachukuaji Mali ya Maskini adhabu za Mollah hazina shaka zitakufika, kwani Maskini wanahuzunika na kusema, wale wana magari makubwa makubwa, wanabadilisha mboga kila siku, wanapata wapi pato hilo na sisi hata hicho chakula kukipata upigane vita vya kweli ndio tonge iende kinywani.
Hivyo ndio wafanyavo Wafalme wetu wanawakalia Raia nyuma na kuwadhulumu haki zao, Na akitokea Mtu na kutaka kutoboa Siri zenu na kuinusuru mali ya maskini, huyo ndio anakua adui wenu, mnamtengenezea na kesi ili mumtie ndani ili asizikere mbinu zenu na kutoboa masikio ya maskini wakaanza kusikia maovu yanotendeka, na yoyote yule ni Mfalme awe katibu, mfanya biashara midamu unawadhulumu wanyonge juwa na wewe huna salama.

وَأَمَّا ٱلۡغُلَـٰمُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤۡمِنَيۡنِ فَخَشِينَآ أَن يُرۡهِقَهُمَا طُغۡيَـٰنً۬ا وَڪُفۡرً۬ا 
Ama yule kijana, wazazi wake walikua Waislamu kamili, tukahofia kwamba asije akawapelekea(Wazee hao) katika uasi na ukafiri.
Yanaendelea mafunzo haya kuwajulisha enyi wazazi msiwapende watoto wenu mkawa mnawaridhia mpaka ikafikia mnajua huyu analeta haramu na nyinyi mnachukua bila wasiwasi, wakakufanyeni mpaka mkamuasi Mollah wenu, pengine ujanani mefanya mema mtoto ndio anakulazimisheni mfanye mambo ya kikafiri, Elimu ya akhera imechanganywa na ya dunia ili kukupeni tahadhari ya baadae.

فَأَرَدۡنَآ أَن يُبۡدِلَهُمَا رَبُّہُمَا خَيۡرً۬ا مِّنۡهُ زَكَوٰةً۬ وَأَقۡرَبَ رُحۡمً۬ا 
Basi tulitaka Mollah wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika na aliye karibu zaidi kwa huruma.
Usiwe na huzuni hata huyo mtoto akisema mie sikusaidii mpaka ufanye hivi na vile, kataa usikubali, fanya utiifu kwa Mollah wako basi atakuletea japo mtoto wa Jirani akusaidie, akuonee huruma na kuwa karibu na wewe kuliko huyo ulomzaa, hii ndiyo Elimu ya akhera inavofundisha ondoa huzuni.


وَأَمَّا ٱلۡجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَـٰمَيۡنِ يَتِيمَيۡنِ فِى ٱلۡمَدِينَةِ وَكَانَ تَحۡتَهُ ۥ كَنزٌ۬ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَـٰلِحً۬ا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبۡلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسۡتَخۡرِجَا كَنزَهُمَا رَحۡمَةً۬ مِّن رَّبِّكَ‌ۚ وَمَا فَعَلۡتُهُ ۥ عَنۡ أَمۡرِى‌ۚ ذَٲلِكَ تَأۡوِيلُ مَا لَمۡ تَسۡطِع عَّلَيۡهِ صَبۡرً۬ا 
Na Ama huo ukuta ulikua wa Vjana wawili mayatima kule mjini, Na chini yake ilikuwako khazina yao, Na baba yao alikuwa ni Mtu mwema, Basi Mollah wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni Rehma itokayo kwa Mollah wako mlezi, wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu, hiyo ndio tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria.
Na Ama ukuta umejengwa sababu ya baba yao tu alikua mtu mwema, Sasa nini habari yetu sisi kama mtajenga Nchi yenu kwa uadilifu na haki, kwa misingi na mazingira ya kidini, pengine hapo mlipo popote pale wakiishi watu wema, na sasa mshakua watu wazima (Gas) inajitokeza, mafuta yanamiminika, mnatakiwa sasa kuyachimba wenyewe, kwanini hamshikamani mkaleta umoja ili kunusuru magonvi ambayo Elimu ya akhera ishatubashiria, kama mtagombea khazina basi magonvi yakianza hayatomalizika daima, kila mmoja achukue khazina yake muishi kwa salama, natoa tahadhari msidhani mtamtoa ngombe mmoja ndio awe kafara, bali kuna hatari ya kutoka zizi zima liwe ndio kafara ya hiyo khazina, na hapa ndio mwisho wa uchambuzi wangu wa Elimu ya Dunia na Akhera.

No comments:

Post a Comment