Sunday, August 31, 2014

MAISHA YA AKHERA PART 2

Asalaam Aleiykum

Inayotakiwa kukumbuka ni Nafsi yako ilojificha katika mambo mengine chungu nzima, ambayo machache nimeyataja huko mwanzoni, ndio maana hukuambiwa nenda makaburini ila umeambiwa kahudhurie.
Nini Kuhudhuria? Kuhudhuria ni kitendo cha kuwapo (Present), sasa kabla ya kuzungumzia huu muhudhurio wacha nikukumbushe vipi wewe unahudhuria hayo makaburi, unakwenda Makaburini pengine baada ya Miaka na tena labda yawepo maziko, halafu ukishafika hapo mazikoni ile maana nzima ya mahudhurio unaitupa pembeni ima utakua umenasa kwenye (Whatssup)kwa siku hizi, ama umejaa katika mazungumzo, au utajikuta kwenye mawazo ya ubishi unataka kujua hawa watafanya manyago gani leo, umejaa ubishi, shari ya ushindani imekushika, hizo ndio hali zetu leo tunapo hudhuria makaburi.
Sasa mahdhurio gani yalokusudiwa? kumbuka unasoma kitu cha kukumbusha Akhera na wewe una hamu ya kujua utafikia (Adress)gani siku yako ikifika, basi kuwa mstahamilivu wakati tukipita taratibu katika kukumbushana huku.
Kinachotakiwa kuhudhuria Makaburini ni wewe Mwenyewe sio (Mind) yako, na wala sio mara moja huwezi kulipata tukio la ukumbusho huo, kusudio zima la zoezi hili ni kuvunja Kiburi chako, kuondosha mimi fulani ,kuvunja kujiona kwako, kuondoshea mbali cheo chako, kuutupa utajiri wako pembeni kabisa, kukufanya wewe ni udongo mtupu, huna ulicho kamata kwenye ulimwengu huu, kufanywa wewe (Empty) kabisa, Na kama umehudhuria kweli Makaburini basi itakupata (Shock)kama vile ulivyoshituliwa au kukosa kugongwa na gari au mshtuko wowote unaoukumbuka ukaona umekwenda moyoni, na moyo sasa unakwenda mbio.
Leo unashuhudia Baba, Ndugu, Marafiki wanamzika na kumfukia Kipenzi chao ambacho jana pengine walikua wakicheka nae, wakila naye, wakimsifu kwa uzuri, leo wanamfukia haraka ili asije akaleta udhia, muda na wakati wake ushamalizika, viumbe wa Akhera mpokeeni mwenzenu sisi tushaishi naye na leo hatumjui tena, si mwenzetu, na huku unawaona wale wale walokua vipenzi vyake pengine wanafanya na (Masikhara)hapo hapo makaburini huku wanajaza dongo likufunike futi sita chini ya Ardhi, wanasahau kama jana tulikua tukila nae, anasahu kila mtu alokuwepo hapo kama pengine siku chache tu itakua zamu yake. Sasa nini kinatokezea ikiwa wewe kweli umehudhuria?
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment