Asalaam Aleiykum
Hata siku moja hujakaa ukatizama kitu ambacho kitakukumbusha Ufalme wako, kitu gani hicho kiwezacho kukumbusha Ufalme wako? kama nilivyosema huko nyuma Ufalme wako umefunikwa na usingizi wa mambo mengi ya tamaa za kidunia kwa hiyo ili kupata huo ukumbusho, ili ujijue wewe Mfalme basi itakubidi jambo la mwanzo usamehe Usingizi, kwa sababu hivi sasa wewe mvivu unalazwa mchana na mambo ya kidunia, ikisha unalala usiku na mambo ya (akhera) kinachotakiwa wewe Mwenyewe ujikaze kwanza kupigana na usingizi wa Usiku kwa kufanya (Ibada) كَانُواْ قَلِيلاً۬ مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَہۡجَعُونَ
"Walikua wakilala kidogo(Nyakati za)Usiku"
Kugundua Ufalme huu lazima ufanye jitihada ya kuondosha mazoea ya usingizi, masaa manne yanakutosha huna haja ya kukoroma mpaka majirani wakasikia, ukipata mazoea haya kidogo kidogo uvivu utaanza kuondoka, ndoto za kiajabu ajabu zitaanza kupotea, usingizi wako utakua(Light)utakua una mazoea ya kumkumbuka Mollah wako kwa Ibada, na utakua japo umelala lakini upo (Alert)huhitaji (Alarm)tena unaamka kwa kutegesha (alarm)yako ya (Awareness).
وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ
"Na Wakiomba Msamaha Nyakati kabla ya Alfajiri"
Ukiwa (Alert)kumbukumbu za mwanzo kuhudhuria ni zile za makosa zilojaa katika Akili yako, hapo Mja alokwisha anza kukumbuka Ufalme wake hana budi ila kujitupa kwa Mollah wake na kuomba Msamaha, na hakuna nyakati nzuri kama zile za karibu ya Alfajiri, kuna siri kubwa katika nyakati hizo ambazo nitazizungumza siku za mbele.
وَفِىٓ أَمۡوَٲلِهِمۡ حَقٌّ۬ لِّلسَّآٮِٕلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
"Na katika mali zao ilikuwa haki ya kupewa maskini aombaye na ajizuiaye kuomba"
Wao washagundua hii Mali imepitia tu katika mikono yao, wamepewa na Mollah wao ili waifikishe kwa wale waombao na pia wasioomba, wao washajua haina faida yoyote kwao, ikiwepo au isiwepo mali hiyo, washagundua kuwa kuna siku watafukiwa chini ya Ardhi na mali yote ibaki juu ya Ardhi na kutafunwa na watu wengine, sasa kuna faida gani ya kuichunga na kuumia kwa kuishughulikia huku unasahau Ufalme ulio nao, itoe kwa njia za kheri ili ipate mali hiyo kukumbusha Ufalme wako, kwani kila ukiweka matamanio ya ulimbikizaji yanazidi, lakini ukitoa na matamanio yanaondoka(Unless)uwe mgonjwa wa kutafuta mali, lakini siku zote kutoa kunakuletea Faraja fulani inayotokea kwenye huo Ufalme ninaozungumza.
وَفِى ٱلۡأَرۡضِ ءَايَـٰتٌ۬ لِّلۡمُوقِنِينَ
"Na katika Ardhi zimo alama(Za kuonesha Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu")kwa wenye yakini.
Pita kwenye Ardhi utizame uhai uloanzia kwenye vidudu mpaka vinyama, ukafikia mpaka Baharini tukawa tunaona vyote vilo hai, mpaka miti na ndege wanavoishi, kaa uwatizame ndege wendavyo kwenye nyumba zao magharibi, na panapo pambazuka alfajiri uone vipi wanavotoka kwenda kutafuta Riziki zao, umewatizama ngombe na farasi wanavokula majani yao, umejiuliza kwanini wakiwekwa kwenye msitu hawali majani yote bali wanachagua baadhi ya majani kuyatafuna, nini kimefichwa kwenye majani hayo hata ikawa Ngombe lazima ayapate hayo, Umeichunguza miti inapokua na furaha vyote hivyo vina uhai kinachotakiwa wewe tu kuyagundua hayo yote yalo wazi mbele yako na yenye yakini, basi itafute hiyo yakini ikuvae kwenye ujuzi wako na ukipata uhakika sasa wewe utakua tayari kukumbuka kwamba, daah, kama mimi nimeweza kuyajua haya basi mimi ni Mfalme, kwa vipi?
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment