Asalaam Aleiykum
Ushapata kujiuliza kwanini ikawa umepewa nafasi Usali Sala hii ya Toba,? Kwani si ingetosha kuomba kwa kusema ikawa mambo yamekwisha, kuna tukio gani limejificha katika Sala hii ya toba, tumo katika maudhui ya Sala hii ya Toba ili tupate faida mbili tatu zipate kutusaidia kwa kuipata Rehma ya Mollah wetu ya kusamehewa, sasa ilikuaje mpaka tukafika katika tendo hilo la Toba, wacha nikujulishe kitu kiwe msaada katika safari yako hii ya Kusali Sala ya Toba.
Woga au (Hofu) ni (Absence) ya Utiifu, najua utashangaa lakini ndio hali ilivyo kila kitu kipya kinashangaza, Unamuogopa Nyoka sababu umempitia karibu na ushasikia ana sumu kali lakini hajawahi kukutafuna, hapo woga ushakuvaa, Unamuogopa Baba kakutisha atakupiga, Unamuogopa Mama kakwambia atakutia adabu hakupi chakula,Unaogopa Utawala sababu utakuadhibu, Unaogopa kiza hujui kitatokea nini ndani ya kiza hicho, unaogopa kufa sababu hujui kama kuna uhai mwengine kaburini au Akhera, na zaidi unaogopa kama upo uhai mwengine basi vipi utazikabili adhabu za huko, huo ni upande mmoja wa woga.
Upande wa pili wa Shilingi hii ya woga kuna Ushujaa, Ushujaa ni kama vile ulivyo woga, ila tafauti yake shujaa ni (Rebel)anaupinga huo utiifu, anaamua kuukabili, anaamua kuukabili utiifu na kupambana nao japo anajua kuna madhara, yeye anapinga kila kitu kwa kuvaliwa na jambo katika mambo mawili yaloujenga huu woga na ushujaa, na hakuna jengine ila hili la (Dark)na(Light) kusahau na kukumbuka, ukitizama kwa undani utajua anayeogopa ni Mwenye kukumbuka, na Shujaa ni Mwenye kusahau, Wawili hawa hawa wote wanapita kwenye (Usiku) na (Mchana) wa (Maasi) na (Kujuta), Mwoga akikumbuka anajuta ikisha (Anatubia)halafu anasahau, Shujaa anakumbuka lakini hajuti ikisha anaendelea kusahau, na wote wanayo ile (Nature) ya kuogopa ambayo inathibitisha kuwapo kwa adhabu za aina fulani, bila ya hivyo kuogopa kusingekuwepo.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment