Anakaa Ibilis kwenye maisha yetu na kutuzunguka katika kila nyanja ya maisha yetu kuanzia kuamka kwetu mpaka kulala kwetu, kama alivyosema.
ثُمَّ لَأَتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيہِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَـٰنِہِمۡ وَعَن شَمَآٮِٕلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَـٰكِرِينَ
"Kisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao na kuumeni(Kulia)kwao na kushotoni kwao, wengi katika wao hutawakuta(Hutowaona)ni wenye kukushukuru(Kukumbuka)"
Wapi ntaanzia ili nipate kuwasahulisha kama wewe umewaumba na unataka kushukuriwa kwa hilo na kukumbukwa, Nimesema anaingia Shetani katika njia za halali, wala si haramu akijua yakini atakushughulisha mpaka umsahau Mollah wako,(1) kwanza anaingia katika ugonjwa wako wa kutafuta mali, huwezi kumkumbuka tena wakati duka umefungua na wateja wanamiminika hivyo kweli unadhani utaikumbuka (Subhanna)migodi ya dhahabu inapasuka unyenyembe huko utakumbuka Mollah kasema nini, Biashara zinatoka unanunua na kuuza utakumbuka kumtaja Mollah wako,uko kwenye mkutano wa siasa unaweza wewe kumsabahi Mollah wako, ofisini unafunga mahesabu unaweza kumkumbuka Mollah wako, haya umekaa barazani hufanyi chochote unaweza kumkumbuka Mollah wako,(Ibilis kazunguka kila pahala, ukiweza kumkumbuka wakati wote ambao umenasa kwenye biashara, maongezi, mikutano ya siasa,ofisini au umekaa barazani au unatizama senema basi wewe moja kwa moja ni mtu wa peponi, ndio maana vitabu vya dini zote vikahimiza kumkumbuka Mollah, vigumu sana kuupata Ufalme wa Mwenye enzi Mungu kwa kuwa Shetani anajua japokua hili ni halali lakini nitatumia njia hii kama silaha ya kuwasahaulisha Mollah wao.
(2)Pili ntawaingia hawa kwenye kadhia ya Mwanamke, kwanza ntamshughulisha huyu Mwanamke awe hana jengine isipokua kuushughulikia mwili wake kwa ajili ya kuutengeneza kwa kujipamba kwa hichi na kile mpaka atakua hamkumbuki Mollah wake kwa lolote isipokua kutaka kuwaridhisha walimwengu wamuone mzuri hususan hawa wanaume, atakua anajipamba huyu usiku na mchana, nitamtia wazimu wa (Shopping)nifisidi kipato chake awe hatoi hata ndururu ya sadaka, na kila akiangalia (TV)yangu hichi kioo ntakua na mwambia bado hujapendeza,Nguo haijabana vizuri, watasemaje kama hutingishiki, itampata shughuli atakua hana muda hata wa sekunde wa kumkumbuka Mollah wake, ikisha nahitimisha kwa Muziki ili nipate kuingia nao kwa urahisi, ndio maana utaona mwanamke akiingia katikati ya ngoma anakatika viuno basi anapata dharau kubwa, sababu hao wenye kushuhudia wanajua huyo tayari kashafukuzwa kwenye Ufalme wa Mwenye enzi Mungu. Na hawa wanaume japokua ni nyendo za halali nitawashughulisha wawe wanamsahau Mollah wao kwa ajili ya kushughulika zaidi na urembo wa mwanamke, kuangalia vifua vyao,kuangalia viuno vyao na kushughulika kuwatafuta mpaka wakawa hawana hamu tena ya kumkumbuka Mollah wao ila wanakumbuka mwanamke(Hiyvo kweli usikie mwanamke anakwita unaweza kumkumbuka Mollah wako), wanamfanyia kazi mwanamke, wanachuma kwa ajili ya mwanamke kutokana na matamanio waliyo nayo, katika viwili hivi ndio yatakua makaazi yangu makuu, nitawasahaulisha hawa hata wakenda kusali basi watakua wanakumbuka mambo yao kuliko kumkumbuka Mwenye enzi Mungu waliyekwenda kumuabudu. halafu nikisha wasahaulisha Mollah wao nitafanya nini?.
Nguvu zikimalizika kabisa, Familia zao walizokua wanazishughulikia na kuzikumbuka wakati wana afya wakifikia uzeeni kila mmoja anamkimbia hakuna anomsikiliza, wanamuacha peke yake na hakuna hata mmoja mwenye kumthamini hiyo ndio bei tunayolipia hapa hapa Ulimwenguni kwa ajili yakumsahau Mollah wetu, Familia, ndugu, wao ndio wanakuwa wa mwanzo ukiwa unaumwa kupanga mipango yako ya mazishi, Roho hata haijatoka uzuri unaona mtu anapita na sanda, mara karafuu maiti imemdondoka, na wewe upo kitandani wamekusahau kabisa kama ndio ulochuma mali, ndio ulojenga hiyo nyumba, ndio ulokua waziri, ukawa kiongozi wajuu na mtoa hukumu wenzio wateswe,leo Shetani kakumbia kakuacha uwazi wewe na wale ulokua ukiwapa kiupa umbele na kumsahau Mollah wako, leo hawana haja na wewe, yote yale yaliyokua yanakushughulisha yametoweka umebaki wewe na Mollah wako, mpaka Shetani keshakimbia, haji tena kwani huna maana kwake, unarudi kwenye Ufalme wa kweli wa Mollah wako ukiwa Muflis, huna kitu, mali zimerithiwa, mwanamke au mwanamme kaolewa au kaoa hivi ndio sote tunavoishi katika Ufalme wa Shetani Ibilis Ufalme wa udanganyifu. Sasa ukitaka uokoke, uepuke na janga hili la kupotezwa na Ibilis ufanye nini?
Endelea Part 3

No comments:
Post a Comment