Sunday, July 29, 2012

ISHARA ZA KUSAMEHEWA(KUMI LA MAGHFIRA)PART 1

Asalaam Aleiykum.
Tumeingia katika kumi la kusamehewa inafaa tumshukuru Mollah wetu alomtukufu katika kutuwekea Rehma hii ya kutusamehe katika mwezi huu wa Ramadhan, Imekujia habari kwamba kila jambo lina ishara katika ulimwengu huu, hujawahi kupata habari yakuwa wanyama wanakimbia masaa machache kabla ya kutokea kinmbunga au tetemeko la Ardhi katika mji, jee hujapata kuwatizama ndege wanavojificha robo saa kabla ya kuanza mvua, zote hizo ni ishara nyengine hata huzijui huna elimu nazo, kama mwili wako binaadamu miezi sita kabla hujaumwa unaleta ishara za ugonjwa lakini wengi hatujui, Hata mauti kwa wenye kujua miezi sita kabla wanajua safari ishawadia lakini tumo katika lepe lepe la usingizi hatuyajui hayo.
Aliuliza mtoto wa Bwana Mtume s.a.w bibi Fatma "Ewe Baba utakapokufa wewe mimi baada ya muda gani nitakufata""akajibiwa baada ya miezi sita wala si zaidi,na kweli baada ya miezi sita akafariki, "ndio maana utaona wale wacha Mungu wa kweli kweli anaweza kukwambia nimebakisha miezi mitatu au siku tatu katika ulimwengu huu, na hata watu wa kawaida hupata ndoto au ilham ikawa wanasema maneno ya kukuaga na wewe ukawa unashangaa, naam hivi ndivo ilivo kila kitu kina ishara na leo hii tunapita katika mti wa ishara sasa wacha tugusie hii ishara ya kusamehewa ambayo imehusu maudhui yetu ya leo.
Kwanini unasamehewa?, Kusamehewa ni Rehma itokayo kwa Mollah wako alompangia mja wake yoyote yule atakae muomba toba, "Akasema Mollah wako mlango huu wa Rehma ya Toba uko wazi  kwa wale wafanyao madhanbi,wanoasi, na waloghafilika.
"Ewe nafsi Tubi"wewe umemaliza kumi la Rehma na sasa umo katika kumi la Maghfira basi ikiwa umefunga kwa Iman na ikhtisaba katika kumi hili wewe hapo ulipo umejaa Rehma za Mollah wako na yatosha hiyo pekee kuwa ishara ya kusamehewa, lau kama unataka uthibitisho ili uridhike kabla hatujaanza kuzichambua ishara nyengine basi yapitie maneno ya Mollah wako yaliyomo kwenye (surat-Zumar)

قُلۡ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسۡرَفُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ لَا تَقۡنَطُواْ مِن رَّحۡمَةِ ٱللَّهِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًا‌ۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

"Sema"Enyi waja wangu mlodhulumu nafsi zenu,msikate tamaa na Rehma za Mwenye-enzi-Mungu, Hakika Mwenye-enzi-Mungu husamehe dhanbi zote,hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe na mwingi wa Kurehemu".
Ikiwa walotenda dhanbi hali hiyo, wanapewa ahadi ya kusamehewa dhanbi zao zote kutokana na Rehma ya Mwenye-enzi-Mungu, Nini habari yako wewe ulofunga katika mwezi huu na ukapita katika kumi la mwanzo lilojaa hizo Rehma, hujapata ishara zozote za huzuni katika moyo wako kuhusiana na dhanbi zako ulotenda ukaanza kuomba Toba,Na jee bado hayajakuingia majuto moyoni mwako kwa makosa uloyafanya, ikiwa hujapata bado ishara hizo mbili basi ikumbatie ishara hii ya (Taqwa)hebu miminika machozi kwa wingi katika kumi hili la msamaha upate kusamehewa dhanbi zako zilopita, isije ikakupita kumi hili ukawa huna hata ishara moja katika hizi tatu nilozitaja, usugue moyo wako labda kutu zimezidi uzidishie moyo wako imani ili Mollah wako akufunike kwenye bawa la Msamaha.
Sasa kwanini isiwe hivyo wakati umefanikiwa kupiga hatua moja kubwa ya kuirekebisha tabia yako kubwa kuliko zote ilokuganda ya kujizuia kula, ikiwa kwa muda wa siku kumi umeweza kupiga hatua hii umeonesha mfano sasa kwanini Mollah wako asikupe ishara za kukusamehe, Na ukitaka kuzijua ishara zilobakia zakwamba sasa una tamaa ya kusamehewa-enedelea sehemu ya pili.

ISHARA ZA KUSAMEHEWA(KUMI LA MAGHFIRA)PART 2

Asalaam Aleiykum.
Umeweza kurekebisha tabia yako ndani ya moyo mpaka ukapata Rehma ya Mollah wako inayoonekana nje, sasa hata ukiona vyakula japo unatamani huvigusi ila kwa wakati mahsusi tena kwa ajili ya Imani ya Mollah wako(Kwanini usisamehewe)hilo pekee ni Ishara nyengine. Kutokana na hali hiyo umeonesha una uwezo hata mengine unaweza kuyaacha ukitaka, ndio maana nikakwambia kwa ishara hiyo fanya ujute kwa makosa yalopita Mollah wako atakusamehe.
Na pia kumbuka huu msimamo ulo shika katika mwezi huu waweza kukusaidia hata baada ya Ramadhani kupita kwanini uweze mwezi huu na ushindwe miezi mengine jee umewahi kujiuliza swali hili, Nataka uelewe tabia za maasi ni adui wako basi kwanini huchagui tabia za kheri zenye malipo ya kudumu zenye kukuunganisha na Mollah wako, Basi hebu jitahidi ikisha Ramadhani ubakie na hizi tabia njema ulozimudu hivi sasa.
Kwa kukumbuka hayo tokwa na machozi kumbe unaweza kukaa bila ya kutenda makosa lakini umetawaliwa na kusudi, kwa kumuhofia alokuumba acha machozi yakumiminike na ikisha uweke ahadi katika kumi hili yakua "Ewe Mollah wangu ukinisamehe"sitorejea tena haya makosa ya kusudi, Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani Mollah kakupa nguvu kuweza kuyashinda mambo yote ya Shetani na vishawishi vyake na wewe angalau kwa siku hizi chache umepata daraja la Uwalii, Basi muombe Mollah wako asikuondoshee Rehma hii ili uwe umetubu toba ya moja kwa moja, kumbuka tafauti yako na walii yeye anadumu katika hali hii ya mwezi wa Ramadhani na wewe ni mwenye kupita njia, Basi ukitaka na wewe udumu katika ishara za kusamehewa hebu pata huzuni katika mwezi huu  kwanini unashindwa kuendelea na tabia hii njema ya kufanya Taqwa.
Ukipata hisia hizo ujue Mollah wako kesha kukubali na wakati wowote anaweza kukushushia Rehma zake ukadumu katia hali hiyo.Sasa pata ishara zaidi za kusamehewa ukiwa nazo hata moja basi jijue umeingia katika kumi hili na umo katika Rehma ya (Toba).
Na Ishara zenyewe utakazozipata mja za kusamehewa, hebu utizame ulimi wako jee umebadilika, Unahifadhika wewe kwa mambo ya kusema uongo, kusengenya na uzushi pamoja na ufedhuli wa maneno, jee unaushughulisha ulimi wako kwa kusoma Qur'aan na kumkumbuka Mollah wako.
Ishara nyengine ya kusamehewa jee unajichunga na sheria za tumbo kuwa huli isipokua cha halali.
Ishara ya kusamehewa jee unaikumbuka Amri ya macho hutizami mambo ya haramu na wala huangalii matamanio ya kidunia yakaku sahaulisha Mollah wako, isipokua macho hayo yawe yenye kudumu kutizama ufalme wa Mollah wako na mafunzo yake.
Na Ishara ya kusikia inayokufanya usamehewe, Amri za sikio   kusikiliza mambo ya maasi ikawa kutwa umedumu katika kusikiliza mipasho ya uongo,habari za watu, kusengenya nk. Jitizame wewe nini yanaingia masikioni mwako, jee sauti za kheri zilojaa makumbusho ya Mollah wako zinapita katika shikio hilo.
Na ishara inayofatia ujijue umesamehewa, jee unajiepusha na maamrisho ya mikono wewe, hukamati au kubeba vilivyo haramu, au kuchukua mali isiyokua halali yako,Na kama vile kukishika kile usojuzu kukikamata, mfano kumshika mwanamke asokua muharim wako,(kama kupeana mikono).Basi inatakiwa mikono hiyo idumu kufanya amali za utiifu kwa ajili ya Mollah wako.
Na ishara inayokujulisha kusamehewa kwako ni kama hii miguu, jee huendi wewe kwenye sehemu za maasi na uchafu, ila uwe unakwenda katika misikiti na kufanya kheri za jihad na sehemu za mambo ya kheri.
Na ishara zengine za kusamehewa zilochupa katika moyo, basi usafishe moyo wako kwa uadui katika dunia hii, usafishe na uhasidi kwa ajili ya watu(ondosha husda)ujaze moyo wako mambo mema na maombezi kwa wenzio na uwe mtu wa nasaha kwa wenzako.
Na japo zipo nyingi hii ya mwisho ya kufungia maudhui yetu ishara yake ya kusamehewa ni kuhusu Ucha Mungu wako uwe mwenye Ikhlas kwa ajili ya Mwenye-enzi-Mungu, Ujiepushe na mambo ya (Riyah)kiburi na jeuri kwa wanaadamu wenzako.
Basi mwenye kuzipata ishara hizi japo moja na hali yakua yumo ndani ya kumi la maghfira basi ajijue yumo katika kundi la kusamehewa na (Inshaallah Mwenye-enzi-Mungu atujaalie tuwemo katika walokubaliwa msamaha)Amin.
A.Baja

Thursday, July 26, 2012

BAHARI YA TAQWA(KUMI LA REHMA)PART 1

Asalaam Aleiykum,
Katika simulizi ya hadith ya hekima inasimuliwa kisa katika vitabu vya zamani kuhusiana na Mji katika miji karibu na Sham. Katika mji huo kulikuwa na wacha Mungu wakiishi na Waumini wa kawaida katika harakati za maisha ya kila siku, Ikawa kila mwaka wale wacha Mungu mmoja moja anachupa katika bahari kuogelea, lakini inatokea ajabu kila akipiga mbizi Mcha Mungu basi haji juu tena anapotea, basi kuona vile Waumini wa kawaida ikawashika shauku kutaka kujua nini kinaendelea, Kwanini Wacha Mungu wanagombea safari hii zamu yangu niachieni mimi nk. Waumini wa kawaida wakaamua safari hii achupe mmoja katika wao lakini lazima katika kukoga huko wamfunge kamba halafu apige mbizi ili wapate kujua huko chini kuna nini na kwanini watu wakenda hawataki kurudi.
Wakamfunga kamba mwenziwao ikisha akachupa alipokwisha kuchupa na kupiga mbizi baada ya muda wakaamua kuivuta kamba lakini alipokuja juu akaja na maradhi yaani akawa bubu, hakusema tena yale aloyaona huko chini(upande wa pili)watu wakashikwa na khofu ikawa sasa hata kuogelea hawendi tena.
Na hali kama hii ndio imetukumba mpaka sasa watu hawataki kabisa kujua upande wa pili kuna nini, Mambo ya dini yanawekera, habari za Mollah wao ndio mama hazitakiwi kabisa, inakua kusikiliza au kusoma mambo haya ni dhiki tupu, massage ya mwanzo kutupa ni ya mambo ya (Dini)anasema mtu usitutie dhiki na vitisho vyako, kumbe tumo katika kuwakumbusha zawadi na fadhila zilizopo upande wa pili (Akhera)ni nyingi na kubwa kuliko hizi chache zilizopo(duniani), Lakini wapi kila mtu anaogopa kuchupa bahari nyeusi (Deep sea)kiza kitupu watu wote wanaogopa. Naam Ucha Mungu unataka kujitolea muhanga upige mbizi hujui chini au (Upande wa pili kuna nini?).Ndio maana utaona watu wote wanalimbikiza vitega uchumi vyote hapa Duniani, Pengine ume (invest)kwenye mapenzi, au una vitega uchumi kwenye maduka, au pengine una majumba au una mashamba au una cheo serekalini na hicho ndio unacho kiabudu huna chengine hivyo unadhani utajishughulisha kutafuta (Taqwa),unaweza kufanya mazoezi ya (Taqwa)ukajihisi unayo taqwa na sijida kubwa ikakudanganya kumbe ni kovu tu, Lakini hiyo (Taqwa)lazima uweke vitega uchumi vya huko akhera, na vitega uchumi vya huko ni vigumu, kwanza unaambiwa nini katika Qura'an' 
ٱلۡمَالُ وَٱلۡبَنُونَ زِينَةُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا‌ۖ وَٱلۡبَـٰقِيَـٰتُ ٱلصَّـٰلِحَـٰتُ خَيۡرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابً۬ا وَخَيۡرٌ أَمَلاً۬ "Mali na watoto ni mapambo ya duniani,Vinavyobakia ni vitendo vizuri, na ni bora mbele ya Mollah wako kwa Thawab na matendo ya kheri"
Hizo mali mnazozichuma na kuziabudu na hao watoto mnaoringia Mwenye-enzi-Mungu anasema ni mapambo hamna uhusiano wowote wa kudumu baina yenu, ndio maana ukiumwa uko peke yako watoto wote wanakukimbia, ukifa peke yako, ukiwa mzee peke yako, kama ulivokuja peke yako na wao wamekuja peke yao kwa hiyo na hiyo mali imekuja isikushughulishe ukasahau yule alokuleta, mkumbuke yule anokupa usingizi, mkumbuke anokusaidia kuvuta pumzi, mkumbuke yule anaekufanya ukaona na kusikia, yule mwenye kukupa afya, basi huzioni Rehma zote hizo ukazinduka yakakutoka machozi kwa ajili ya Mollah wako ukaona hujafanya chochote katika mwezi huu wa Ramadhani kuitafuta hiyo Taqwa, sasa ufanye nini japo kuikaribia hiyo Taqwa. Endelea sehemu ya pili 2.

BAHARI YA TAQWA(KUMI LA REHMA)PART 2

Asalaam Aleiykum.
Sasa unataka kuipata Taqwa umejiuliza katika mwezi huu wana hali gani wale wasokua na futari ili uwasaidie(Hiyo Taqwa)Nini hali ya wazee walokuwa wagonjwa(HiyoTaqwa)kwanini unaendelea kuzuia hizo pesa au mali yako kwa faida ya nani?,jikumbushe umekuja katika dunia hii huna kitu na utaondoka huna kitu, "Enyi matajiri nyinyi isifike siku ya kufukiwa na hali umeacha marundo ya mali duniani bado hujayatolea zaka au sadaka"atahadhari sana mtu kumfika siku hiyo mapesa yamelaliana bank hususan katika mwezi huu waRamadhan, Qura'an inatukumbusha:.يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡتَنظُرۡ نَفۡسٌ۬ مَّا قَدَّمَتۡ لِغَدٍ۬‌ۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ
"Enyi Mloamini mcheni Mwenye-enzi-Mungu na kila nafsi iangalie(kile)inachotanguliza kwa ajili ya huko (Akhera), Na mcheni Mwenye-enzi-Mungu, Hakika Mollah wenu ana habari(Anayajua)yale yote mnayoyatenda"
Naam vinatakiwa hapo vitendo vya Taqwa ndio vyenye uzito mkubwa kesho wakati umefunikwa vipande vya vitambaa, amali zote zishakatika, nafasi hii ulopewa uko hai hujaitumia umeshghulika na dunia, sasa ufanye nini upate hiyo Taqwa na malipo mema kwa Mollah wako Masharti yenyewe hata sio mengi hayafiki hata kumi huna haja hata yakutoa rushwa, sasa ufanye nini kinachotakiwa hapo kama wewe una mali sio tajiri limetumika neno una mali pesa pia zimo katika mali,nini tunatakiwa tufanye tuipate hiyo Taqwa na tuweke zawadi zetu za huko Akhera, la Mwanzo kabisa unatakiwa utoe hicho ulichokua nacho kwa mapenzi sio umenuna, toeni hiyo mali mnayoipenda ikiwa pesa au kitu chengine, kwanza kabisa wapeni walo jamaa zenu, halafu Mayatima, ikisha maskini, na wapeni wasafiri waloharibikiwa njiani, na wale wenye kukuombeni msiwakimbie, ikisha hayo yote sasa simamisheni sala na kutoa zaka, na mtekeleze ahadi mnazozitoa basi mkitenda hayo mtakua wacha Mungu wa kweli na wale wasokua na kitu kamataneni na kamba ya kumkumbuka Mollah wenu kwa wingiwa ibada, na mkitekeleza hilo moja tu basi na nyinyi mtakua katika wacha Mungu wa kweli, na hiyo ndio kheri anayokutakieni Mollah wenu na atakuruzukuni pasi na hisabu.Umo katika mwezi wa kulea Roho fanya japo machache ujikurubishe kwa Mollah wako.


Abdulla Baja










Sunday, July 15, 2012

SIRI YA RAMADHAN(VIPI UPATE TAQWA)PART 1

Asalaam Aleiykum
nimeona nikuleteeni japo kwa uchache dhumuni la hii funga ya Ramadhani najua Masheikh wakubwa wanaileza ipasavyo na kwa upeo mkubwa lakini na mimi nataka niizungumze kwa njia nyengine ili upate kujua siri ya (saum)pengine itakusaidia ikiwa unaona ina manufaa na wewe.
Enyi Mloamini melazimishwa kufunga(Saum)kama walivolazimishwa kufunga waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.
Katika mada hii nitajaribu kugusia hasa dhumuni la kwanini ukalazimishwa, pametiwa ulazimu kutokana na miezi yote kumi na moja mwanaadamu umefungika katika shughuli iwe ya kumsahau Mollah wako au maasi yasokua na hesabu, Na kwanini isiwe hivo hali yakua wewe umeumbwa na uhuru kamili ufanye upendavo na katika uhuru huu wewe uko dhaifu, umekutana na mambo mengi huwezi kujizuia umemuasi Mollah wako na kutenda yalojiri mwenyewe unayajua,Sasa kwa mapenzi ya Mollah wako umefika mwezi huu kakutengea japo siku chache ikiwa wewe ni Muumin na una mapenzi ya Mollah wako basi sasa fanya (Taqwa)ucha Mungu.
kuna swali jengine hapa litakuzukia na kujiuliza mimi muumin najihesabu miezi hii yote kumi na moja nafanya taqwa nasimamisha sala,natoa sadaka, sasa leo vipi (Mollah)wangu ananitaka hususan katika mwezi huu nijifunge ili nifanye hiyo (Taqwa). Mambo yanakushangaza muumin, Sasa usipate taabu unaingia katika Ustaadh wa kulea (Roho)pata faida wewe na wenzako ili mwaka huu Ramadhan yako iwe ya aina nyengine kabisa na ujifunge kupata huo (Ucha-Mungu)unaotakiwa. Kabla ya kwenda mbele hebu tujiulize hili neno (Taqwa)lina maana gani, ukitaka kulitafsiri neno hili basi hata bahari haitoshi kuliandika tafsiri yake, lakini wacha tupate uchache wa maana yake ili tukiendelea mbele tujue nini tunachokizungumza, Nini (Taqwa) taqwa ni mapenzi ya kukurejesha kwa Mollah wako,Taqwa ni vitendo vyote vya kheri alivoridhia Mollah wako,Taqwa ni huruma,Taqwa ni kufa ukiwa hai kwa ajili ya Mollah wako(hii inataka ufafanuzi inshaalah siku za mbeleni),Taqwa ni subira na kama nilivosema zipo tafsiri nyingi ya maana ya neno hili na mwisho kabisa kufupisha tafsiri yetu niseme (Taqwa)ni kurejea nyumbani ulikotoka kwa Mollah wako.
Sasa kabla ya kupata hii Taqwa kuna kitu lazima ukipate ili kikuchukue kukupeleka katika hiyo Taqwa, kitu gani hicho kinacho kupeleka, tutegee sikio kuisikiliza hadith ilopokelewa na Sahaba Salman farsy r.a "Anasema Bwana Mtume s.a.w"Umekujieni mwezi Mtukufu wenye baraka, ndani ya mwezi huu kuna mafungu matatu,Fungu la kwanza Rehma,na la pili Maghfira, na la tatu kuipata Pepo na kuepushwa na Jahannam. Sasa kazi yangu ya leo nikukujulisha hiyo Rehma inapatikana vipi kama unajua basi hakuna ziada njema tembea na mimi ili tukachume mti huu wa Rehma ili tupate kujuwa hili tunda la (taqwa)lina ladha gani?.endelea part 2





SIRI YA RAMADHAN(VIPI UPATE TAQWA)PART 2

Asalaam Aleiykum:
Naam sasa kwanini likatajwa hili fungu la mwanzo kuwa la Rehma, Sababu kubwa hapa mwanzoni kuna mtihani(ule wa samaki mkunje yungali mbichi)ni mtihani mkubwa wa hicho kinachoitwa (Saum)ili upate hiyo (Taqwa).
Napenda kama unanifatilia kwa makini basi rejea tena ile aya inayo amrisha huku kufunga inasemaje katika hili neno linalosema(KUFUNGA)sio kama saum zetu ambazo tumezigeuza kujizuia,elewa chochote kile unachozuia kuna wakati utachoka lazima ukiwachie, Ndio maana utaona saum zetu tunajizuia mchana, ikisha usiku tunajiachia na hasara yako ukijiachia hakuna (Taqwa)muflis inakua kukaa kwako na njaa hakuna faida yoyote kwa sababu hujafunga kama ulivotakiwa ili upate kuipata hiyo (Taqwa)"Enyi mloamini nimekulazimisheni kufunga ili mpate kumcha Mungu". Unaingia katika Ustaadh wa kulea Roho soma taratibu na kwa makini ili upate kujua hii Rehma na Taqwa inapatikana vipi katiki hili kumi la mwanzo ili na wewe upate radhi za Mollah wako.
Naam sasa ufunge vipi upate hiyo Rehma ili ikupeleke kwenye Taqwa, umeijua taqwa japo kidogo basi pata japo kwa uchache uijue Rehma nayo ikoje.Rehma ziko za aina mbili zenye kuonekana na zisizo onekana(au zilofichika)wale walo karibu na Mollah wao sana wanapata bahati kuona na kuzijua japo kwa uchache na ndio wao wakapata kutuhadithia na sisi japo hatufahamu nini tunahadithiwa,Hizo rehma zipo bila ya idadi yaani nyingi sana na inatakiwa ujitupe kwa Mollah wako kupata fursa za kufahamu, kama nilivosema Rehma inakamatana na hii taqwa, kwa sababu lazima mwanzo upate hii Rehma halafu ndio upate hiyo taqwa,kama nilivotaja huko mwanzoni  katika baadhi ya sifa zilobebwa na Rehma ndipo inapatikana katika tafsiri yake, Huruma,upole,imani na hii Rehma ndio njia ya kupita kwenda katika huo mlango wa Taqwa wa kurejea kwa Mollah wako.
Sasa vipi ufunge kuyapata hayo?
Kusudio la kuambiwa ufunge ni matarajio ya kutakiwa ufunge kila kitu unachojua au kudhani kitakunyima fursa ya kupata Rehma na Taqwa, ndio maana ukaambiwa jitahidi siku zenyewe chache usione taabu, sasa vitu gani hivo (uvifunge)au kama unavoita wewe ujizuie navyo sasa tega shikio nikujulishe nini hasa unatakiwa uvifunge.
Endelea part 3

SIRI YA RAMADHAN(VIPI UPATE TAQWA)PART 3

Asalaam Aleiykum:
Siku zote mnaambiwa Shetani katika mwezi huu anafungwa na mimi leo nakwambieni vifaa vya shetani havifungwi viko wazi na mnaendelea kuvitumia kama kawaida.
Sasa funga ina maana gani? maana yake vile vitu vyote vyenye kukuondoa au kukufanya mwaka mzima ukamsahau Mollah wako basi sasa uvifunge, kama TV, kama Karata,kama Senema,kama Baraza za mambo ya kipuuzi, kama kucheza Game au Video za harusi, kama kusikiliza nyimbo, kama kutizama mambo ya maasi na kuyatenda na mengine mengi nyinyi mnayajua sina haja mimi kutaja kimoja kimoja.
Funga maana yake katika mwezi huu usiruhusu kupita kitu chochote katika akili yako kika kusahaulisha kumdhukuru Mollah wako hata dakika moja na ukaacha kumkumbuka, sababu hayo yote yanakunyima fursa ya kuipata hiyo Rehma na kuishi ndani ya (Taqwa).
Sasa wacha tuiguse maana ya kufunga ili tujue Rehma inapatikana vipi, kufunga ni kufanya gap au kujenga daraja baina ya Roho na kiwiliwili,au maana nyengine kuwa(aware-alert)au kuwasha nuru au taa katika umbile lako kwa yale masaa yote unayofunga au siku zote yategemea funga yako ya aina gani, na la muhimu linachowasha hiyo taa au kukufanya (aware)au kukupa hiyo nuru ni hicho chakula, mimi hapa leo nitagusia hili moja la chakula kwa kuwa funga zetu ndio zinanzia hapo na kuishia hapo hapo.
Jee umeshawahi kujiuliza kwanini hasa ukifunga kutwa unakua unafikiri chakula, mara madizi mabivu, mara kalmati n.k imekupitikia katika akili kwanini inakua hivyo, kumbuka tena Shetani kafungwa lakini nyenzo zake zinaendelea ikiwemo akili haitaki kabisa kumkumbuka Mollah wake lakini imeshghulika na chakula mchana kutwa, na hilo ni moja linalo kukuondoshea ghushui na taqwa na kuikosa Rehma ya Mollah wako, nimechagua kulizungumza hili la chakula kwa kuwa ni rahisi kwangu kukuonesha njia za rahisi kuipata hiyo Rehma, njia ziko nyingi lakini zengine ni ngumu kwako, natumai hili la chakula linaweza kukusaidia.
Sasa ikiwa hiyo akili inakupeleka katika kukumbuka vyakula basi tambua ina uwezo wa kukupeleka katika upande mwengine, nini kinyume cha shibe ni njaa hata siku moja hujawahi kuifikiria njaa, wengi wetu tunakula hata bila ya kushikwa na njaa, tunakula kwa ajili ya tabia usibishe fanya uchunguzi wewe mwenyewe hivyo ushawahi kushikwa na njaa ukenda kula, au wakati wa kula ndio umefika unakwenda kula?na hilo unalitenda lakini huna njaa yoyote na unachofanya ni tabia, Sasa leo nataka kukufundisha hiyo njaa inaweza kuwa hilo daraja la kukuvusha ukenda sehemu nyengine, siku zote njaa inakupeleka wewe pasi na kujua unaanza kufikiri chakula, basi kuanzia leo kaa makini isubiri pale njaa inapokuja kuna wakati njaa inakuja lakini wewe fikira zako zote zinapelekwa katika chakula, sasa kuanzia leo subiri ikija njaa anza kuifikiri hiyo njaa,teremka chini kwenye tumbo, kuna kitu utahisi baina ya kitovu na mbavu kinakaa kwa muda mchache ukiweza kua (aware)na kitu hicho basi mara moja utaona njaa inapotea na nguvu zake zinakua (transform)katika hali nyengine kabisa, ukimaliza hapo kukigundua kitu hicho kamata (Mashafu)au kakae msikitini, nenda katizame wagonjwa, au kasaidie wazee na hali itakayokutokezea hapo ndio hiyo Rehma na hapo kama huna cha kufanya aya ya mbele inakwambia kakae itikafu, utaona unakua mpole, hamaki zitakuondoka,utaanza kuwa (alert)kama taa ilowaka hapo utaipata (siri ya ramadhan),lakini usije ukababaishwa na uangukaji wa damu(low blood sugar)lazima ujue tafauti yake.
Napenda uelewe njaa ni kitu kilichomo katika mwili wako na hizo ni Rehma katika uweza wa Mollah wako itumie ikubadilishe kutoka katika kuwaza mambo ya vyakula ikupeleke kwengine.Njaa inakufanya (alert)ndio maana huwezi kukuta mtu ana njaa akatafuta mambo ya uasherati n.k kwa kuwa wakati ule yuko (alert)kasha washa taa lakini ya kumurika chakula sasa imurike neema ya Mollah wako kwa kufanya (Taqwa)uwe katika walofuzu, napenda kukujulisha pia ndio maana mkaambiwa mkifutari msishibe sana kwani shibe inakupelekeni katika kiza mnakua hamuezi kutenda ibada wala kumkumbuka Mollah wenu, ukiacha hayo nilokwambia mwanzoni, ukaacha kauli za kipuuzi na kuchunga ulimi wako, ukajikinga na mambo ya maasi basi Bwana Mtume s.a.w anakwambia katika hili kumi la mwanzo utapata Rehma na mambo mawili yatafatia nayo ni.endelea part 4.

SIRI YA RAMADHANI(VIPI UPATE TAQWA)PART 4

Asalaam aleiykum:
Mkipata hiyo Rehma mtapata mambo mawili kwa manne, leo kwanza nitayataja mawili nalo la kwanza ni:
Anasema Bwana Mtume s.a.w "atakuridhieni Mollah wenu katika kuipata hiyo shahada ya Laa-illah-illah-Allah na la pili itakua kwenu kuomba Maghfira"na hapo ndipo yanapatikana maneno ya Bwana Mtume s.a.w "hakika hii ndio Ramadhani, mwezi wenye Baraka,ni mwezi wa kumogopa Molla wenu, na katika mwezi huu ndipo anakuteremshieni hiyo Rehma, kakufanyieni hii funga akukingeni na makosa na kukubalieni dua zenu, na zinatizamwa nafsi zenu zinavoshinda katika mambo ya kheri.
Akasema Bwana Mtume s.a.w"Wamepewa umati wangu mambo matano hajapewa Mtume yoyote kabla yangu"(1)Katika usiku wa mwanzo huwatazama Mollah wako waja wake(Katika Ramadhan)na ambae alotizamwa na Mollah wake hato adhibiwa abadan"(2)"Malaika wanawaombea  maghfira usiku na mchana"(3)Mwenye-enzi-Mungu anaiamrisha pepo kwa kuiambia,jipambe kwa ajili viumbe wangu walofunga ili waje kupumzika na tabu(walozipata)duniani"(4)Na harufu zao ziwe nzuri kuipita misk"(5)Na inapofika usiku Mwenye-enzi-Mungu ana ghufuria(Kusamehe)madhanbi yao yote.Iwe(Mfano kama kwamba vile wafanyakazi wanapomaliza kazi zao wakalipwa ujira wao)Na hili ndio kumi la mwanzo na hilo ndio kumi la Rehma maana yake ni nuru,maana yake sasa usha washa taa, sasa humo tena kizani, hukai tena katika himaya ya Iblis, umo katika (Awareness)kwani kumbuka mambo yote ya ufisadi huyafanyi ila uwe umelala katika akili(unconciousness)lakini ukiwa(Alert)hufanyi kabisa kama nilivosema katika darsa zilizopita yakua huwezi kutenda dhanbi hali ya kuwa unamkumbuka Mollah wako, basi fungeni ili mpate kufanya hiyo Taqwa. Tunamuomba Mollah wetu atujaalie tuipate (saum)kwa ukamilifu na Iman inshaallah.
Abdulla Baja

Monday, July 9, 2012

UMUHIMU WA DUA NA MAISHA YAKO(PART 1)

Asalaam-Aleiykum: Leo katika darsa hii nitazungumzia umuhimu wa dua na chanzo chake, kuna watu wengi tu hawajui nini dua na umuhimu wake,wamekua sasa wenye kuipuuza kabisa haitakiwi dua katika mkusanyiko wowote hata kwenye darsa siku hizi kitu hiki kimeondoka, Mara chache sana utakuta Darsa inaanza au kumalizwa na dua, sina haja ya kuzungumzia msiba siku hizi ukenda kwenye nyumba ilofikwa na msiba mazungumzo makubwa ni mambo ya mpira n.k. Katika maudhui hii nitagusa japo kidogo kwa undani ili upate kuijua nini Dua? na wapi imetokea, Halafu tena una hiyari yako kusoma au kuacha kama unavoshauriwa na Masheikh wako. Naam Nini Dua? Dua ni maombi ya (IBADA)au kwa msemo mwengine ni sawa sawa na (KUMKUMBUKA-MOLLAH-DHIKR)Ni kitendo cha kupeleka maombi kwa Mollah wako kwa unyenyekevu,heshima na matumaini makubwa ya kukubaliwa yawe maombi hayo ya furaha au huzuni.Sasa wapi na lini Dua ilpoanzia, Hapa itabidi Tuilize Qura'an kwa sababu ndio pekee itakayotupa yakinifu ya jambo hili, Na hapana pahala pengine pakuanzia ila pale Nabii Adam a.s alipofanya makosa na kuasi-Qura'an-sura-ya-Baqarah-aya-ya(37) فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَـٰتٍ۬ فَتَابَ عَلَيۡهِ‌ۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ "Ikisha Adam akapokea maneno kutoka kwa Mollah wake,Akatubu hakika (Mollah)wako ni mwingi wa kupokea Toba na mwingi wa kurehemu". Naam hiyo ndio Dua mwanzo inaanza na Toba ikisha Inamalizikia na Rehema, Na maneno haya katuletea, katupangia mwenyewe Mollah wetu ili tupate kitu cha kufungamana na yeye Mlezi wa viumbe vyote, Na kwanini isiwe hivyo wakati wewe Mollah wetu ndie ulikata, ukaamua baina yako na Mja (utadumu msamaha)vipi leo tuambiwe hata dua ina makosa. Nikizungumza Dua sina maana ile ya mchezo mchezo watu wamekaa na vichekesho vyao halafu anazuka mtu lete dua, laa ile sio dua ile wazungu wanaita (Lip-service)ninachozungumza hapa ni ile dua (sincere)itokayo moyoni, Inayotoka kwa utulivu na huku Moyo unatetemeka kwa Imani, siyo ile inayotoka mdomoni kwa ajili ya mazoea, Ndio maana Bwana Mtume s.a.w akawa anawfundisha Umma wake dua nyingi ili zipate kuendelezwa na wala hajaweka kikomo au muda au pahala maalumu. Nini Dua?.Akasema Tena Mollah wako kumwambia Mtume s.a.w-(Baqarah-aya-ya-186) وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِى عَنِّى فَإِنِّى قَرِيبٌ‌ۖ أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِ‌ۖ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لِى وَلۡيُؤۡمِنُواْ بِى لَعَلَّهُمۡ يَرۡشُدُونَ "Waja wangu watakapokuuliza (kuhusu mimi)mimi niko karibu nao,Naitikia maombi ya Muombaji(Talib wa Mattlub)anaponiomba, Basi na waniitikie na waniamini, ili wapate kuongoka". Hapo Bwana Mtume s.a.w hakuambiwa waambie,imetoka (Direct-line)mimi niko karibu nao naitikia maombi ya muombaji anaponiomba,"Ewe Mollah wetu unatupa pasi sisi kukuomba" lakini limewekwa shuruti kwanza uitikie halafu uamini,uitikie kwa kukubali au (surrender)na uamini sio bure unaomba lakini katika nafsi yako huamnini, iwe ukifanya kosa basi amini kama unatubu kwa moyo mkamilifu utasamehewa lakini utaamini vipi wakati wewe huishi na imani mtihani mkubwa huu. Katika maswala ya Dua itakiwayo Imani uwe umejitupa kikweli huna wasi wasi, uwe na tamaa ya kujiamini kuwa Mollah wako ni mwenye kukubali maombi yako,ukumbuke anakupa ulichoomba na hata usichoomba, na wala isikushike shaka katika kuomba huko anasema Mollah wako sura ya (Rahman-aya-ya-29) يَسۡـَٔلُهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ‌ۚ كُلَّ يَوۡمٍ هُوَ فِى شَأۡنٍ۬ "Vinamuomba yeye vilivyomo mbinguni na ardhini,na kila siku(Mollah wako)yumo katika mambo mengine(mapya)". Kwanini ukatazwe kumuomba Mollah wako wakati wewe Mollah wako kakuumba (Special-Unique)uko peke yako katika ulimwengu huu na ikisha akakupa Akili(Brain-Mental-capacitiy)ya kuwasiliana naye,Nini sasa kinachotakiwa hapo ni kuisafisha (Microphone)yako, rekebisha mitambo yako yakurushia hiyo dua ili ipate kufika huko unakoituma, vipi utafanya endelea sehemu ya pili upate kujua kuna siri gani ya dua yako kufika kwa aliyeumba Mbingu na Ardhi.

UMUHIMU WA DUA NA MAISHA YAKO(PART 2)

Asalaam-Aleiykum: Sasa nini chakufanya jambo la mwanzo unatakiwa uteremke katika katika moyo wako, kwani ndani ya huo moyo ndipo inapokaa imani yako, na ndani ya hiyo Imani ndipo inapotokea hiyo Dua (ndio maana mwanzoni katika ile aya ukaambiwa waniamini)ukiwa na hiyo Imani basi umeshapata(Miracle)hutaki Sheikh,wala Ustaadh au mwengine yoyote, na wala asipite mtu akakwambia ahh usiombe dua hivi na vile,haramu haifai, wote hao ni mabingwa wa kupanga maneno, wachunguze wenyewe hawana Imani ni maneno yanawatoka vinywani mwao hawana yakinifu yoyote, muulize vipi Dua itakua haramu au makosa wakati imeshuka kwa sababu ya hiyo haramu na makosa. Na kama itakupata shaka jitizame wewe mwenyewe ni dua tupu toka unaamka mpaka una lala,Maisha yako yote ni dua tupu, ukitaka kula dua, ukishikwa na kiu dua, kuvuta kwako pumzi dua kila kitu chako ni dua mpaka ukitaka kunyanyua mguu dua lakini masikini bado hujajua siku utakayo kuja kujua yatakutoka machozi Mollah wako akikufungulia (Elimu)hiyo. Nini Dua?. Dua ni mfano wa Ua likitaka kuchanua halisubiri eti mpaka wewe upite eti ndio lichanue, wakati ukifika halijali chochote linachanua tu umepita hukupita wala halichagui wakati na hivyo ndio dua ya imani itokayo moyoni, haijali pahala au aibu(haimuogopi sheikh eti atasikia na yeye kashanikataza)kwani humuoni Imam Mtu mzima anaomba dua machozi yanamiminika hajapigwa au kufanywa chochote na wewe kama uko nyuma yake au unatizama kwenye TV inakutoka (Amin)bila ya kukusudia wapi yule Imam dua ile imetokea na wewe kagusa vipi?hebu jiulize maswala haya usiwe unakubali mambo bila ya kuyafanyia uchunguzi. Naam hapo nyote wawili inakua mmepagusa pale panapotokea dua na hiyo ndio dua ya kweli inayotokea Moyoni hapakugusi hapo isipokua ujue kipimo cha Imani yako. Na usijizuie ukitaka kulia kwani hata Bwana Mtume s.a.w Alitokwa na machozi kama anavotuhadithia Ibn Umar r.a "Mtume s.a.w Alikwenda kumtizama Bwana Saad Bin Ubeidah r.a alipokuwa anaumwa kwa kuwa Bwana Mtume s.a.w ni mtu wa mapenzi na wakati wote akiishi katika moyo wa Imani machozi yakawa yanamiminika, Katika mahudhurio yale alikuwepo masahaba Abrahman bin Auf r.a Sad bin Waqas r.a na Abdullah bin Masoud r.a na wao machozi yakawa yanawatoka hizo ndizo imani hizo ndio hisia,Bwana Mtume s.a.w akwaambia sikilizeni Mollah hampi adhabu mtu kwa kulia au kuhuzunika ila ana adhibu au kusamehe kutokana na yale yalotamkwa na ulimi(Maasi-au Dua). Inasikitisha siku hizi unakwenda kwenye nyumba za misiba eti watu sijui wanaogopa au wamekatazwa(leo mpaka dua upewe ruhusa)lakini utakuta mwenye msiba yupo kimya walokwenda kutoa pole wanazungumza mambo ya kipuuzi au mpira (Lakini dua haramu)hususan wanaume na hivi ndio tulivofikia kujua kwetu sana kumetufikisha katika hali kama hii. Nakumbuka katika darsa zetu hapo zamani lazima itolewe (Riwaya)si hadith napenda uelewe ni riwaya za kuchangamsha (Darsa)lakini ndani yake kuna mafunzo makubwa,"Kilitolewa kisa cha (IBILIS)kitafakari sana kisa hiki halafu utafikia uamuzi kina mafunzo au hakina.(Mke wa Ibilis siku moja alimuuliza mumewe "Ewe Ibilis mbona siku hizi nakuona huna raha ukiingia umenuna ukitoka mnyonge"Akajibu Ibilis ninahuzuni kubwa kwani nimekuwa (Jobless)sina kazi siku hizi."Akasema yule mke hee mbona mambo makubwa haya kwani wewe si kazi yako ya milele""akajibu Ibilis Ahh bibie siku hizi wameingilia katia watu wanojiita masheikh watu hawa imekua dhiki juu yangu, wanawakataza watu wao kuelekea kwa Mungu,kumkumbuka Mollah wao sasa mpaka dua wanaziondosha, wanadhulumu waumini kazi zote nilokua nafanya mimi wamechukua wao. Na Hii ndio hali tulofikia watu wanaifanya kazi za Ibilis lakini huwezi kugundua mpaka uwe na upeo wa kuona. Sasa nakuusieni mkifikwa na misiba mtu aseme kabisa mnakuja mjue hapa tunasoma dua au tuna nyamaza kimya mpaka mnaondoka, pia tambueni Mollah wenu kakupeni siku hizi tatu kubwa akakutakeni mumkumbuke kwa dua katika siku hizi, lakini wapi sie ndio tumechagua siku hizi ndio kumsahau kabisa Mollah wetu, siku gani hizi, siku ya kuzaliwa mtoto, siku yako ya harusi au unapokufika msiba, asije akaja mtu akakwambieni vyengine hebu takeni ushahidi japo kidogo katika Qura'an asije mtu na hadith yake moja akakuondosheeni Rehema zote zilizomo ndani ya DUA. Sasa namuomba Mollah wangu kwa kusema"Ewe Mollah wangu Nakuomba kwa sifa za majina yako yote utuongeze nguvu za moyo wa imani na roho zetu asiweze yoyote yule kuja kuuingia nyoyo zetu akatwambia dua ni haramu na sisi tukamkubalia, Nakuomba Mollah wangu usafishe ulimi wangu uyathibitishe ukweli wa maneno yangu. Mollah wangu nipe mimi na waislamu wenzangu mioyo ya kimaskini wakutaka radhi zako katika kutukubalia maombi yetu(DUA)utie khofu moyo huu wa kukuogopa wewe na kuwa karibu na wewe,Mollah wangu yafanye maneno yangu yapokelewe kwa moyo mkunjufu kwa wale wenye Imani na wanokupenda wewe, Na mwisho Mollah wangu nipe ukaribu niwe karibu ya wale wenye kukujua wewe, namalizia kwa kumsalia kipenzi chetu Mtume s.a.w Amin. Abdullah Baja

Sunday, July 1, 2012

VAZI LA UCHA MUNGU (PART 1)

Asalaam Aleiykum. Leo tunaingia katika mada ambayo pengine yaweza kuwa ufahamu wako haujawahi kukutana na maelezo kama haya ikawa hichi kinacho andikwa kipya kwako, Basi nakuomba ufanye hisani ya kuyazingatia na kuyasoma kwa utulivu mkubwa ili upate kufahamu kwa uzuri haya yaloandikwa. Binaadamu tumebahatika sana kupewa (Rehma)na Mollah wetu katika mambo haya mawili yaliyohusiana na maumbile yetu, La kwanza (Nature)au Umbile letu halina tafauti na Mnyama, Halafu la pili tukapewa nafasi sisi ni viumbe pekee tulopewa uwezo wa kupanda daraja kutoka katika hali ya Wanyama na kwenda zaidi hata kufikia upeo wa juu kabisa ambao ndio huo (Ukhalifa)au Ucha Mungu katika ardhi hii. Katika maudhui hii tutaziangalia njia zote mbili ili tuweze kujua vipi unaweza kutoka njia moja ukajiunga na njia nyengine itakayo kukupeleka katika huo Ucha Mungu,(Mimi hapa nataja hiyo source)wewe una hiyari yako vipi unataka kuifanyia kazi ikiwa za kheri au shari uamuzi ni wako mwenyewe. Sasa haiwezekani kabisa kuzungumzwa mada hii bila kwanza kugusia kisa cha Nabii Adam a.s na Bibi hawa kilichotokea hapo mwanzoni ili upate kufahamu vyema maana hususia ya (Vazi la Ucha Mungu)huwezi kuhadithia kisa ukaanza mwisho na ukaacha mwanzo wake, Sasa huo mwanzo ulikuwaje? jikumbushe na aya za Quraan sura ya Baqarah-aya-35: وَقُلۡنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٣٥) "Na tulimwambia "ewe Adam kaa wewe na mkeo katika bustani(peponi),kuleni humo mmeridhiwa popote mpendavyo,lakini msiukaribie mtii huu,msije mkawa katika waliodhulumu(kuto kutii amri ya Mwenye-enzi-Mungu)". Katika aya hii ndio tunasoma yale maneno unayosikia kila siku yakitajwa ndoa zinafungwa au zinaandikwa mbinguni, Mollah wako mwanzo kabisa anawaambia "Ewe Adam kaa na mkeo"sio hawara,au mchuchu,au girlfriend,au kimada kaa wewe na mkeo,ukifanya vyengine basi wewe umo katika makosa,huna hiyo (Taqwa)hata chembe na wala hutoipata mpaka mauti yatapokukuta, Na sababu kubwa umepiga mbizi katika dhuluma,unaishi kinyume na mwenendo alokupangia Mollah wako.Naam kaeni wewe na mkeo,lakini sharti ni moja msije kula katika mti huu,(kwani mkitenda hivyo mtajitia katika giza,kwani neno dhulumu limetokana na asili ya neno kiza, Na neno kiza mwenzie katika tafauti ni Nuru)Na hii nuru ndio kawaida yetu tunaishi ndani ya hii nuru na hii nuru ndio hiyo(Taqwa)kama tutavosoma huko mbeleni.Wawili hawa wakakaa salama kila kitu chao wanakipata wapendavyo,Shetani akawaingia kuwashawishi na kuwafanya wale katika ule mti kama inavyoendelea katika aya ya (36-sura-ya Baqarah)mpaka mwisho wake, Sasa nini kilitokea?. Wlipokula tu lile tunda hapo wakawa wenye kwenda kinyume na amri ya Mollah wao wakatumbukia (Gizani)Nini kiza?wanasayansi wanasema (Darkness is Absencess of light)ikawaondokea ile (privilage)haki ya Utiifu na kupata wanachokitaka katika maraha ya peponi ikatoeka ile(Blissfull life)hapo taa ya (Ucha)Mungu ikawzimikia na hapa ndio inaingia ile aya ya (27-sura-ya-Al-Aaraf)يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّڪُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡہُمَا لِبَاسَہُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٲتِہِمَآ‌ۗ إِنَّهُ ۥ يَرَٮٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُ ۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَہُمۡ‌ۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَـٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ (٢٧) "Enyi wanaadamu asikufitinini Shetani,Kama alivyo watoa wazee wenu peponi,(alifanya nini shetani)Akawavua nguo zao(Taqwa-Utiifu-Nuru)ili awaoneshe tupu zao, Hakika yeye pamoja na kabila lake wanakuoneni, na hali yakuwa (nyinyi)hamuwaoni,Sisi tumwajaalia mashetani kuwa marafiki wa wale wasoamini". Naam hiyo nguo hususan ndio inalenga maudhui yetu, tunataka kujua nguo hii ni ya aina gani na kwanini walipokwisha kula hilo (Tunda) mara wakaziona tupu zao, na vipi imehusiana na chakula hayo yote tutayafahamu huko mbele ikiwa utasoma kwa njia ya utulivu na kutanguliza fahamu mbele, Na kwanini isiwe chakula wakati Mollah wetu Amesema katika sura ya (Abasa-aya-ya-24) فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦۤ "Basi Na atizame mwanaadamu chakula chake". Katika karne yetu hii tunajua kwa ukamilifu vipi chakula kinavyofanya kazi zake katika mwili wetu, tunaelewa kuwa (Akili-au-Brain)inachukua 85%ya vitamin zote zinazoingia mwilini, Sasa ilikuaje baada ya kula tu hilo tunda wakapoteza zile haki zote na neema zote walokua nazo,nini kilitokezea mpaka ikawa mpaka hii leo vigumu kwetu kuipata hiyo pepo, inakuaje safari hii inakua nzito sana, upo katika uchambuzi wa Vazi la Ucha Mungu endelea sehemu ya pili upate faida zake ili ukifunga saumu yako safari hii iwe ya aina nyengine kabisa.

VAZI LA UCHA MUNGU(PART 2)

Asalaam-Aleiykum. Inaendelea kutokea sehemu ya kwanza: "Walipokwisha kula tu hilo tunda hapo wakapata fahamu, ikawa sasa ni wenye kujua wamechukua madaraka mikononi mwao(wamezima ile taa)wao wenyewe wamejitumbukiza katika giza, na ukiingia katika kiza sasa ndio unaanza safari ya kuitafuta taa tena, na ukianza kutafuta inabidi utumie akili yako kurejea kwenye muangaza na kwa kuwa unajua kutafuta njia ya kurudi basi hapo unakua unafahamu kila kitu, Ndio maana mpaka leo ikawa mtoto akifikia (Umri)wa Baleghe anaanza kuwa na dhamana ya maisha yake, Hapo tena Bwana Adam a.s na Bibi Hawa wakapata fahamu wakaziona tupu zao wakajua tafauti waliyonayo na vilowazunguka wakajisitiri kwa majani,Na ukisha kujua au kufahamu unapoteza ile (Innocent)yako hapo ndipo aya iliposema:(An-Nisaa-17), إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَـٰلَةٍ۬ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ۬ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡہِمۡ‌ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَڪِيمً۬, Hakika ya toba inayokubaliwa na Mollah ni yale wale wanofanya maasi kwa ujinga(kutokufahamu)ikisha wakatubia kwa haraka, Hao ndio Mollah huipokea toba yao, Mollah(wako)ni mjuzi na mwenye hekima. Lakini hakuna toba inayopokelewa baada ya kujua kwako kama aya ya 18 inavoendelea mpaka ukasubiri tena ushakua mzee unataka kufa halafu useme umetubu, hakuna kabisa maadam umefanya jeuri subiri chamte-makuni kikufike,na hivi ndio maana mpaka hii leo inakua taabu kwetu sisi kuipata pepo,sote tunahangaika kurejea peponi hakuna asotaka lakini na maasi hatutaki kuyaacha na kwa kuwa tunae mpinga amri zake ndie alotuumba basi tutateseka mpaka mwisho wa umri wetu tulopangiwa kuishi kwenye Ulimwengu huu. Kutokana na madhila na tafrani na uzito tunaojipa sisi wenyewe wa kuipata hiyo pepo ndio maana wanaadamu wengi wetu tunachagua basi bora turejee katika hiyo jinsia ya (Unyama,)bora niwe mnyama ili nijifiche kwa kujitoa fahamu, sasa nifanye nini?Wengine wanaamua kutumia pombe,wengine wanatumia (Drugs)madawa ya kulevya,wengine wanatumia (sex)ili anadhani mtu atajishughulisha na kusahau apate usingizi apate (relief)ya matafrani lakini yote hayo kwa kuwa ni kinyume na mwenendo ano utaka Mollah wako yanakua (Temprory)dharura kwa muda mfupi tu, pombe ikisha au madawa ya kulevya ya kisha au hamu ya (ngono) ikisha unarejea pale pale katika hali ya njia ya kuelekea (Ukhalifa)au (Taqwa)Ucha Mungu. Mwanaadamu ni lazima uchague njia ya Ucha Mungu ndio njia pekee itakayo kufanya upate salama na amani na hayo unayo yataraji hapa duniani huko peponi, Na Mollah wetu hajatufukuza moja kwa moja ila katuwekea njia ya kurejea kwake hakutufungia mlango, akatwambia mkifanya (Taqwa)Ucha Mungu utiifu,basi mtaipata ile hali walokua nayo wazee wetu Nabii Adam a.s Na Bibi Hawa huko peponi. Sasa Mollah wetu katushushia Vazi la ucha Mungu na nini hasa kitacho kujulisha hilo vazi la ucha Mungu,sasa nakutaka urudi nyuma ukaitizame ile aya uzuri zaidi ilosema huko mwanzoni"wasiukaribie ule mti wakala hilo tunda, walipokwisha kula hilo tunda wakajitupa kwenye (Dhuluma)kiza, sasa ikabidi tuletewe mavazi ya Aina mbili kama inavosema (sura-ya-Aaraf-aya-ya-26)"ـٰبَنِىٓ ءَادَمَ قَدۡ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمۡ لِبَاسً۬ا يُوَٲرِى سَوۡءَٲتِكُمۡ وَرِيشً۬ا‌ۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقۡوَىٰ ذَٲلِكَ خَيۡرٌ۬‌ۚ ذَٲلِكَ مِنۡ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ (٢٦). "Enyi Wanaadamu tumekuteremshieni vazi ili mpate kusitiri (Uchi)tupu zenu na vazi la Ucha Mungu(Utawa) na hilo ndio bora zaidi,Hayo ni katika dalili(Neema)za Mollah wenu ili wapate kukumbuka". Hebu tuitupie macho nguo imetokana na nini, nguo imetokana na (Chakula)iwe ngozi au miti vyote hivyo vimetokana na ardhi,(Abasa-30) وَحَدَآٮِٕقَ غُلۡبً۬ا "Na miti ilosongana",ndio inayofanya nguo hizi tunazo zivaa hivi sasa,hili ndio vazi la kuhifadhi miili yetu, Halafu kuna nguo nyengine hii Wanaadamu tunaivaa ndani ya Mwili wetu na hii ndio inayotupelekea kuupata huo Ucha Mungu na vazi hili limewekewa fundi wake lazima upitie kwa fundi ndio akuvishe guo hili, endelea sehemu ya tatu ya Maudhui hii ili ukakutane na huyo fundi hususan mwezi mtukufu uko njiani unakaribia usije ukakosa nguo yako, pata japo kidogo na wewe kufahamu.

VAZI LA UCHA MUNGU (PART 3)

Asalaam-Aleiykum. Inaendelea kutokea sehemu ya pili, Hakuna jengine litakalo kukujulisha hilo vazi la ndani la Ucha Mungu ila upitie sura ya (Tariq-aya-ya-5-7) فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ مِمَّ خُلِقَ (٥) خُلِقَ مِن مَّآءٍ۬ دَافِقٍ۬ (٦) يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآٮِٕبِ (٧) "Na Ajitizame mwanaadmu, ameumbwa kwa kitu gani.Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa(Kasi).Yatokayo katikati ya mifupa ya mgongo na kifua(Mbavu)". Wote tunaelewa maji haya yakishuka chini yanatengeneza (Uhai)kutokana na uwezo wa Mollah wetu, na yanatoka kwa wote wawili mke na mume,sasa leo nakwambieni pia yana njia nyengine maji haya yakipanda juu yanakuwa (Taqwa)Vazi la Mcha Mungu na hiyo ndio maana ya vazi hili,sasa usianze kunikamatia majambia pengine hujasoma mambo haya kwa Sheikh wako yafanyie uchunguzi huku ukiendelea kupata maalumati haya. Katika Ulimwengu huu kuna kuna sheria mbili za (Nature)Yaani moja inaitwa(Gravitation)ambayo ina vuta kila kitu ardhini halafu kuna nyengine inaitwa (Levitation)hii inapandisha juu, katika sheria hii kila kitu kinapanda juu, lakini lazima kipate (Rehma)za Mollah wako, Maji ya Uzazi(Life Energy) yanatengenezwa pia na chakula yakija chini hii (life-Energy)inafanya kizazi,yakipanda juu yanakufanya uwe Mcha Mungu lakini kwa masharti yake;Ndio Maana Bwana Mtume s.a.w akasema "Ibada hazikubaliwi kabisa kwa muda wa siku arobaini ikiwa utakula chakula cha haramu(Taqwa)haiwezi kupatikana (system)haifanyi kazi na Mollah wetu katuhimiza katika aya nyingi(Mfano)(Baqarah-168)"Enyi wanaadamu kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri,wala msifuate nyayo za shetani,bila shaka yeye ni adui kwenu". Haiwezekani ufanye haramu, ule haramu halafu utarajie kuwa wewe Mcha Mungu huwezi kupata guo ukalivaa abadan, Amesema Bwana Mtume s.a.w Yoyote yule mwenye kupigana katika njia ya kutafuta kupata riziki ya halali basi atapata malipo kama yule alokufa kwa njia ya Mwenye-enzi-Mungu.Amesema Bwana Mtume s.a.w Yoyote yule atokula chakula cha halali kwa muda wa siku (40)basi Mollah wake ataungarisha moyo wake,na atamtia hikma katika moyo huo pamoja na ulimi wake, Bwana Mtume s.a.w katueleza kwa njia nyingi tu kama "alivosema:Ewe Umma wangu eleweni ya kwamba tumbo ni kama sehemu ya maji inotoa michirizi,na michirizi hii inapita katika njia za mwili ikiwa kitachopanda au kuteremka kikiwa halali basi mwili mzima utakua wenye kheri, na kikiwa kitokacho ni haramu basi hakuna kitofatia isipokua Maradhi matupu na shari, Masahaba baada ya kuijua siri hii walikua wakijitapisha na hadith ziko nyingi sana kuhusiana na kadhia hii,Alipewa Bwana mmoja Mcha Mungu chakula akakikataa, yule alompa akamuuliza imekuaje sahib yangu nimekupa chakula huja kitia mkono, akamjibu sili mimi isipokua chakula cha halali, Na kwa hilo moyo wangu unakua imara katika dini,nadumu katika ibada, na napata Ilham za Akhera, na kama nitakula haramu yoyote basi fadhila hizo zitapotea kwangu mimi,na hiyo ndio hali ya mawalii wacha mungu wanataka guo lao libakie safi halina dowa, Na siri hii ndio ilowafanya wakiristo wajipangie ule ukasisi kama inavosema Qur'aan-(Al-Hadyd-aya-ya 27). ثُمَّ قَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيۡنَا بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ وَءَاتَيۡنَـٰهُ ٱلۡإِنجِيلَ وَجَعَلۡنَا فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ رَأۡفَةً۬ وَرَحۡمَةً۬ وَرَهۡبَانِيَّةً ٱبۡتَدَعُوهَا مَا كَتَبۡنَـٰهَا عَلَيۡهِمۡ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ رِضۡوَٲنِ ٱللَّهِ فَمَا رَعَوۡهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا‌ۖ فَـَٔاتَيۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۡہُمۡ أَجۡرَهُمۡ‌ۖ وَكَثِيرٌ۬ مِّنۡہُمۡ فَـٰسِقُونَ (٢٧, "Ikisha tukawafatishia nyuma yao Mitume wetu(wengine)tukamleta Isa Bin Mariam, Na tukampa Injili na Tukauweka upole na Rehema katika nyoyo za wale walomfata na huu Uruhubani(Utawa-Wanaume wasioe na wanawake wasiolewe)wameubuni (wenyewe)sisi hatukuyaandika hayo,(Waliamua wenyewe)ili kuitaka radhi ya Mollah wao, Lakini hawakuufata,kama INAVOTAKIWA kuufata, basi tukawapa wale walioamini miongoni mwao ujira wao,na wengi wao ni waasi". Naam tupia macho neno katika aya hiyo neno hili(KAMA INAVOTAKIWA) hapo inakujulisha ipo (system)inayotakiwa kufatwa na hakuna njia nyengine isipokua (Saumu)funga ndio njia pekee inayobadilisha mwenendo huu baada ya kushuka chini maji haya yanapanda juu, ndio maana hapo mwanzoni ilipoteremka habari ya Ramadhani ikawa marufuku hata kufanya tendo la ndoa lakini watu ikawashinda japo kwa siku hizi chache za mwezi mmoja, ndipo ikashuka katika aya ya (187-sura-ya-Baqarah)أُحِلَّ لَڪُمۡ لَيۡلَةَ ٱلصِّيَامِ ٱلرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَآٮِٕكُمۡ‌ۚ هُنَّ لِبَاسٌ۬ لَّكُمۡ وَأَنتُمۡ لِبَاسٌ۬ لَّهُنَّ‌ۗ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّڪُمۡ كُنتُمۡ تَخۡتَانُونَ أَنفُسَڪُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡ وَعَفَا عَنكُمۡ‌ۖ فَٱلۡـَٔـٰنَ بَـٰشِرُوهُنَّ وَٱبۡتَغُواْ مَا ڪَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡ‌ۚ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِ‌ۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِ‌ۚ وَلَا تُبَـٰشِرُوهُنَّ وَأَنتُمۡ عَـٰكِفُونَ فِى ٱلۡمَسَـٰجِدِ‌ۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَقۡرَبُوهَا‌ۗ كَذَٲلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ ءَايَـٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ (١٨٧). "Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu, wao ni nguo kwenu na nyinyi nguo kwao,Mollah (wenu)anajua kwamba mlikuwa mkizihini(Mnapata taabu)nafsi zenu, kwa hiyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni, Sasa changanyikeni nao na takeni aliyokuandikieni Mollah(wenu)kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku, Ikisha itizimeni saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao na hali (yakua)mnakaa itikafu misikitini,hiyo ni mipaka ya Mollah(wenu)basi msiikaribie, Namna hivi Mollah wenu anabainisha hoja zake kwa watu ili wapate kumcha(Kumtii). Kama nilvoitaja wao wananguo(na huo ni mfano)kutokana na mwenendo wake wa kuenea mwili mzima na nyinyi mna nguo kwa ile kadara ya kushuka chini,kama ilivo kawaida ya kuvua na kuvaa, saumu ni njia moja ya kufanya (Energy)hii kupanda juu ndio maana ukaambiwa inakata matamanio, ndio maana ukaambiwa kakae msikitini usiipe nafasi (life Energy)hii kushuka chini katika mwezi huu, hebu ipe nafasi ipande juu, iwache ifanye kazi yake ili upate (Taqwa)ya Ramadhani, Jifunge usile haramu,na jiepushe na mambo ya kutizama mambo ya matamanio, Sasa nini kinatokea ikiwa utafanikiwa kutekeleza masharti yake likiwemo Riziki ya halali, Hapo utapata mambo haya,napenda pia uelewe hili ni vazi tu si vitendo itabidi ufanye vitendo kupata manufaa ya guo hili, dalili zake kama (life Energy)hii ishaanza kupanda juu utaona kwanza kabisa unakua mpole, unajaa huruma, imani inaongezeka, busara na hekima zinakushukia,unakua mtaratibu, mapenzi yanakuzidi kwa Mollah wako na Familia yako, utajiona unashiriki sana vitendo vya kheri, hata tabia zako kuelekea kwa mkeo zinabadilika, lakini yote hayo yanatokana na kula vya halali na saumu ilotimia ndio maana Bwana Mtume s.a.w "akawaambia wale vijana wasoweza kuoa juu yenu kuna Saumu na hiyo ni yenye kukata, ni (Method)ya kuzuia (Gravitation)kwani vijana wakiachiwa mtaani hapakaliki,na ikiwa watafunga vijana basi hapo itapatikana hiyo(Levitation)na panapatikana salama, vijana wanakua wacha Mungu, Kwani wewe hujui tafauti jee bado hujajichunguza(life Energy)hii ifanyavyo kazi zake, Inakuaje mmekaa kimya mnasoma darsa akiingia au akipita mtoto wa kike ndani ya chumba hali inabadilika mpaka akili hazifanyi kazi tena umepata kujiuliza kitu gani wakati ule kinatokea, basi kama bado anza uchunguzi wako, Usije ukakubali maneno yangu bila ya kuyafanyia uchunguzi, usichukue maneno Sheikh kasema basi na wewe unayakubali laa fanya uchunguzi japo kwa wiki mbili jitahidi kuichunga (Energy)yako, jitahidi kula halali, halafu funga saumu yako, na kama chochote hakijatokea basi rejea kwangu uje kuniuliza mbona hakuna chochote, lakini shuruti zake ni hizo itabidi ujikaze katika kuzuia (life Energy)yako isishuke chini kila mara, na kama ni mwenye kuweza basi utaona hata Afya yako inaanza kubadilika, mapenzi yanakuzidi kuhusiana na mkeo, lakini ni lazima upate mapumziko, hapo maumivu yataondoka, matafurani yatapungua kwenye akili, usiwe mwenye kupoteza (life Energy)yako kipuuzi kila siku iache ifanye kazi zengine kwenye mwili na napenda ukumbuke haya yote hi khiyari na huu wangu ni ushauri, usije ukamkimbia mumeo au mkeo ukasema mimi nimesema laa tupo katika kuelimishana tunapeana elimu,wale wengine walokua hawajui wapate kufahamu. Kazi yangu ni kukumbusha umuhimu wa maji ya uhai (life Energy)tulokua nayo katika miili yetu ikishuka chini(Creativeness)na ikipanda juu Vazi la Ucha Mungu(Holiness) na linalo subiri vazi hili ni vitendo vya kuelekea kwa Mollah wako. Nakumbusha tena Mzee wetu Nabii Adam a.s na Bi Hawa waliambiwa msiukaribie huu mti mkala tunda lake, na walipopinga ile amri wakafukuzwa peponi, na sisi Mollah wetu katupangia njia ya kurejea tena huko peponi, ndipo akatushushia (Vazi)la Ucha Mungu ndio iwe njia yetu, akatuwekea utaratibu wa kulivaa guo hili nao ni Saumu(Ramadhani)pia nguo hii ikipanda juu basi ina faida nyengine nayo inafanya(Repair)katika katika mwili inatibu maradhi mengi pasi nasi kujua,ndio maana tukaambiwa(Hakika ya hiyo Saumu ni kheri kwenu ikiwa mnajua), Kumbuka hapo mwanzoni (Shetani)Alituvua nguo hii na sasa tumepewa njia na Mollah wetu ili tuivae tena tupate kuwa kama hapo mwanzoni tuishi kwa salama na amani hapa ulimwenguni na huko akhera tuendapo. Naomba Mollah wetu atujaalie tuifunge Ramadhani kwa salama, tulipate hilo guo(Nguo)ya (Taqwa)wakati wa itikafu yetu, ikisha atudumishe katika hiyo (Taqwa)wala guo lisituvuke milele inshaallah, Mwisho naomba ukumbuke ukiwa utakula haramu japo kidogo hupati (Rehma)hii ya Vazi la Ucha Mungu. Mollah wangu anajua zaidi. Abdulla Baja