Asalaam aleiykum:
Mkipata hiyo Rehma mtapata mambo mawili kwa manne, leo kwanza nitayataja mawili nalo la kwanza ni:
Anasema Bwana Mtume s.a.w "atakuridhieni Mollah wenu katika kuipata hiyo shahada ya Laa-illah-illah-Allah na la pili itakua kwenu kuomba Maghfira"na hapo ndipo yanapatikana maneno ya Bwana Mtume s.a.w "hakika hii ndio Ramadhani, mwezi wenye Baraka,ni mwezi wa kumogopa Molla wenu, na katika mwezi huu ndipo anakuteremshieni hiyo Rehma, kakufanyieni hii funga akukingeni na makosa na kukubalieni dua zenu, na zinatizamwa nafsi zenu zinavoshinda katika mambo ya kheri.
Akasema Bwana Mtume s.a.w"Wamepewa umati wangu mambo matano hajapewa Mtume yoyote kabla yangu"(1)Katika usiku wa mwanzo huwatazama Mollah wako waja wake(Katika Ramadhan)na ambae alotizamwa na Mollah wake hato adhibiwa abadan"(2)"Malaika wanawaombea maghfira usiku na mchana"(3)Mwenye-enzi-Mungu anaiamrisha pepo kwa kuiambia,jipambe kwa ajili viumbe wangu walofunga ili waje kupumzika na tabu(walozipata)duniani"(4)Na harufu zao ziwe nzuri kuipita misk"(5)Na inapofika usiku Mwenye-enzi-Mungu ana ghufuria(Kusamehe)madhanbi yao yote.Iwe(Mfano kama kwamba vile wafanyakazi wanapomaliza kazi zao wakalipwa ujira wao)Na hili ndio kumi la mwanzo na hilo ndio kumi la Rehma maana yake ni nuru,maana yake sasa usha washa taa, sasa humo tena kizani, hukai tena katika himaya ya Iblis, umo katika (Awareness)kwani kumbuka mambo yote ya ufisadi huyafanyi ila uwe umelala katika akili(unconciousness)lakini ukiwa(Alert)hufanyi kabisa kama nilivosema katika darsa zilizopita yakua huwezi kutenda dhanbi hali ya kuwa unamkumbuka Mollah wako, basi fungeni ili mpate kufanya hiyo Taqwa. Tunamuomba Mollah wetu atujaalie tuipate (saum)kwa ukamilifu na Iman inshaallah.
Abdulla Baja
No comments:
Post a Comment