Monday, July 9, 2012
UMUHIMU WA DUA NA MAISHA YAKO(PART 1)
Asalaam-Aleiykum: Leo katika darsa hii nitazungumzia umuhimu wa dua na chanzo chake, kuna watu wengi tu hawajui nini dua na umuhimu wake,wamekua sasa wenye kuipuuza kabisa haitakiwi dua katika mkusanyiko wowote hata kwenye darsa siku hizi kitu hiki kimeondoka, Mara chache sana utakuta Darsa inaanza au kumalizwa na dua, sina haja ya kuzungumzia msiba siku hizi ukenda kwenye nyumba ilofikwa na msiba mazungumzo makubwa ni mambo ya mpira n.k. Katika maudhui hii nitagusa japo kidogo kwa undani ili upate kuijua nini Dua? na wapi imetokea, Halafu tena una hiyari yako kusoma au kuacha kama unavoshauriwa na Masheikh wako. Naam Nini Dua? Dua ni maombi ya (IBADA)au kwa msemo mwengine ni sawa sawa na (KUMKUMBUKA-MOLLAH-DHIKR)Ni kitendo cha kupeleka maombi kwa Mollah wako kwa unyenyekevu,heshima na matumaini makubwa ya kukubaliwa yawe maombi hayo ya furaha au huzuni.Sasa wapi na lini Dua ilpoanzia, Hapa itabidi Tuilize Qura'an kwa sababu ndio pekee itakayotupa yakinifu ya jambo hili, Na hapana pahala pengine pakuanzia ila pale Nabii Adam a.s alipofanya makosa na kuasi-Qura'an-sura-ya-Baqarah-aya-ya(37) فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَـٰتٍ۬ فَتَابَ عَلَيۡهِۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ "Ikisha Adam akapokea maneno kutoka kwa Mollah wake,Akatubu hakika (Mollah)wako ni mwingi wa kupokea Toba na mwingi wa kurehemu". Naam hiyo ndio Dua mwanzo inaanza na Toba ikisha Inamalizikia na Rehema, Na maneno haya katuletea, katupangia mwenyewe Mollah wetu ili tupate kitu cha kufungamana na yeye Mlezi wa viumbe vyote, Na kwanini isiwe hivyo wakati wewe Mollah wetu ndie ulikata, ukaamua baina yako na Mja (utadumu msamaha)vipi leo tuambiwe hata dua ina makosa. Nikizungumza Dua sina maana ile ya mchezo mchezo watu wamekaa na vichekesho vyao halafu anazuka mtu lete dua, laa ile sio dua ile wazungu wanaita (Lip-service)ninachozungumza hapa ni ile dua (sincere)itokayo moyoni, Inayotoka kwa utulivu na huku Moyo unatetemeka kwa Imani, siyo ile inayotoka mdomoni kwa ajili ya mazoea, Ndio maana Bwana Mtume s.a.w akawa anawfundisha Umma wake dua nyingi ili zipate kuendelezwa na wala hajaweka kikomo au muda au pahala maalumu. Nini Dua?.Akasema Tena Mollah wako kumwambia Mtume s.a.w-(Baqarah-aya-ya-186) وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِى عَنِّى فَإِنِّى قَرِيبٌۖ أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِۖ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لِى وَلۡيُؤۡمِنُواْ بِى لَعَلَّهُمۡ يَرۡشُدُونَ "Waja wangu watakapokuuliza (kuhusu mimi)mimi niko karibu nao,Naitikia maombi ya Muombaji(Talib wa Mattlub)anaponiomba, Basi na waniitikie na waniamini, ili wapate kuongoka". Hapo Bwana Mtume s.a.w hakuambiwa waambie,imetoka (Direct-line)mimi niko karibu nao naitikia maombi ya muombaji anaponiomba,"Ewe Mollah wetu unatupa pasi sisi kukuomba" lakini limewekwa shuruti kwanza uitikie halafu uamini,uitikie kwa kukubali au (surrender)na uamini sio bure unaomba lakini katika nafsi yako huamnini, iwe ukifanya kosa basi amini kama unatubu kwa moyo mkamilifu utasamehewa lakini utaamini vipi wakati wewe huishi na imani mtihani mkubwa huu. Katika maswala ya Dua itakiwayo Imani uwe umejitupa kikweli huna wasi wasi, uwe na tamaa ya kujiamini kuwa Mollah wako ni mwenye kukubali maombi yako,ukumbuke anakupa ulichoomba na hata usichoomba, na wala isikushike shaka katika kuomba huko anasema Mollah wako sura ya (Rahman-aya-ya-29) يَسۡـَٔلُهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ كُلَّ يَوۡمٍ هُوَ فِى شَأۡنٍ۬ "Vinamuomba yeye vilivyomo mbinguni na ardhini,na kila siku(Mollah wako)yumo katika mambo mengine(mapya)". Kwanini ukatazwe kumuomba Mollah wako wakati wewe Mollah wako kakuumba (Special-Unique)uko peke yako katika ulimwengu huu na ikisha akakupa Akili(Brain-Mental-capacitiy)ya kuwasiliana naye,Nini sasa kinachotakiwa hapo ni kuisafisha (Microphone)yako, rekebisha mitambo yako yakurushia hiyo dua ili ipate kufika huko unakoituma, vipi utafanya endelea sehemu ya pili upate kujua kuna siri gani ya dua yako kufika kwa aliyeumba Mbingu na Ardhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment