Asalaam Aleiykum:
Naam sasa kwanini likatajwa hili fungu la mwanzo kuwa la Rehma, Sababu kubwa hapa mwanzoni kuna mtihani(ule wa samaki mkunje yungali mbichi)ni mtihani mkubwa wa hicho kinachoitwa (Saum)ili upate hiyo (Taqwa).
Napenda kama unanifatilia kwa makini basi rejea tena ile aya inayo amrisha huku kufunga inasemaje katika hili neno linalosema(KUFUNGA)sio kama saum zetu ambazo tumezigeuza kujizuia,elewa chochote kile unachozuia kuna wakati utachoka lazima ukiwachie, Ndio maana utaona saum zetu tunajizuia mchana, ikisha usiku tunajiachia na hasara yako ukijiachia hakuna (Taqwa)muflis inakua kukaa kwako na njaa hakuna faida yoyote kwa sababu hujafunga kama ulivotakiwa ili upate kuipata hiyo (Taqwa)"Enyi mloamini nimekulazimisheni kufunga ili mpate kumcha Mungu". Unaingia katika Ustaadh wa kulea Roho soma taratibu na kwa makini ili upate kujua hii Rehma na Taqwa inapatikana vipi katiki hili kumi la mwanzo ili na wewe upate radhi za Mollah wako.
Naam sasa ufunge vipi upate hiyo Rehma ili ikupeleke kwenye Taqwa, umeijua taqwa japo kidogo basi pata japo kwa uchache uijue Rehma nayo ikoje.Rehma ziko za aina mbili zenye kuonekana na zisizo onekana(au zilofichika)wale walo karibu na Mollah wao sana wanapata bahati kuona na kuzijua japo kwa uchache na ndio wao wakapata kutuhadithia na sisi japo hatufahamu nini tunahadithiwa,Hizo rehma zipo bila ya idadi yaani nyingi sana na inatakiwa ujitupe kwa Mollah wako kupata fursa za kufahamu, kama nilivosema Rehma inakamatana na hii taqwa, kwa sababu lazima mwanzo upate hii Rehma halafu ndio upate hiyo taqwa,kama nilivotaja huko mwanzoni katika baadhi ya sifa zilobebwa na Rehma ndipo inapatikana katika tafsiri yake, Huruma,upole,imani na hii Rehma ndio njia ya kupita kwenda katika huo mlango wa Taqwa wa kurejea kwa Mollah wako.
Sasa vipi ufunge kuyapata hayo?
Kusudio la kuambiwa ufunge ni matarajio ya kutakiwa ufunge kila kitu unachojua au kudhani kitakunyima fursa ya kupata Rehma na Taqwa, ndio maana ukaambiwa jitahidi siku zenyewe chache usione taabu, sasa vitu gani hivo (uvifunge)au kama unavoita wewe ujizuie navyo sasa tega shikio nikujulishe nini hasa unatakiwa uvifunge.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment