Asalaam Aleiykum,
Kwenye hii (Vital Energy) inataka ufafanuzi wa ziada, sote tunaelewa kwa lugha ya sayansi wakati tunavuta hewa tunaambiwa tunavuta(Oxygen) huo ndio ufahamu wetu, lakini wale walo karibu na Mollah wao wanaelewa(Oxygen) ni gari tu ya kubeba na kukichukua hicho kilofichika ndani ya (Oxygen)kuna kitu maalum chenye kukufanya Uishi, hicho kinabebwa na hiyo (Oxygen) na kuingia katika Mwili wako, ukitaka kugundua hilo fanya ufike kujikurubisha na Mollah wako utapata kukijua nini hicho.
Naam kutoka kwa Roho ndugu zangu ni jambo kubwa na si la kufanyiwa maskhara kabisa, Nini habari yetu sisi tulozama kwenye maasi, itakuaje siku hii ikitukuta bado tumo kushughulika na dunia, vipi itakua tuje kutolewa Roho mbichi ilochafuka na madhanbi, ilokua ina ishi miaka nenda miaka rudi ikichuma na kufurahikia Maasi, vipi utakua utokaji wa Roho zetu.
Sasa ikiwa ndio Roho ishakata Tamaa, na matumaini hakuna tena na dhanbi ndio ushatenda na wala hazifutiki tena, nini cha kufanya? Jee kipo cha kufanya ili kupita katika daraja hili la Uhai na kwenda katika huo mji wa Mauti kwa salama. Naam la kufanya lipo na tena upande mmoja rahisi sana na upande wa pili mgumu sana, shauri ni kwako wewe kama utaweza, Jambo la kwanza ni lazima ukumbuke dhanbi zako zote ulofanya, kwanini nikakwambia ukumbuke kwa sababu nikikwambia ujute au utubu hutoweza kufanya hivyo, ndio itakua unakwenda na kurudi pale pale, unatubu unajuta uongo halafu unaendelea tena, lakini nikikwambia ukumbuke madhanbi yako yote wakati unayakumbuka moja baada ya moja yatakupeleka katika hisia za makosa na hisia hizo zitakupeleka kwenye kujuta na ukianza kujuta basi jua ushaanza kutubu, na ukianza kutubu kinakuteremkia kilotajwaa katika Sura ya Zumar aya ya 53
" قُلۡ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسۡرَفُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ لَا تَقۡنَطُواْ مِن رَّحۡمَةِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًاۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ"
"Sema Waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu, msikate tamaa na Rehma ya Mwenye-enzi-Mungu, Bila shaka Mwenye-enzi-Mungu husamehe dhanbi zote, hakika yeye mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu"
Hapo kwenye Moyo wako itaanza kuingia tamaa ya kusamehewa, anakutia Mollah wako Rehma zake na kukubadilisha kama ulikua unakwenda mwenendo wa kushoto unabadilika unaanza kwenda kulia, kama ulikua (Over-sex)itaanza kupungua na (Sex)matamanio yakipungua Taqwa(Ucha Mungu)unazidi na Taqwa ikizidi (Attachement)inapungua kama ulikua unapenda Mali, unakua hupendi tena, kama ulikua umezama katika mabiashara sasa unakua hupendi tena, kama ulikua unapenda watoto huwachukii lakini mapenzi yako yanahamia kwa Mollah wako, unapata kujijua kumbe mimi hapa Ulimwenguni(I belong to no one, and no one Belong to me)Nimekuja peke yangu, na nitaondoka peke yangu.
Na mapenzi yakihamia kwa Mollah wako hapo tena unapata kufahamu kwa undani kumbe mimi sitoguswa na Mauti, ila mauti yanatendeka kwenye kiwiliwili changu, hapo ndipo yanapokutana baina ya Mauti na Uhai, na tabu zote nazipata wakati wa kutoka Roho yangu sababu kubwa kungangania hivi vilivyomo ulimwenguni, Unatolewa Roho yako huku huzuni imekushika umeacha mapesa mengi Bank, nyumba zako tano atarithi nani, hivyo ile gari wataitunza, wewe unaitwa Akhera hutaki kwenda unakwenda shingo upande, kuna mambo hujamaliza ndio maana mnagombeana Roho na Malaika, lakini ukiacha (Attachement) ukaridhika nini kinatokezea siku hiyo. unatolewa Roho huku umeridhika hupati uchungu hata chembe na huku unaambiwa.Al fajr-27-30
"يَـٰٓأَيَّتُہَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَٮِٕنَّةُ"
"Ewe nafsi yenye kutua(Na matumaini)"
"ٱرۡجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً۬ مَّرۡضِيَّةً۬"
"Rudi kwa Mollah wako, hali ya kuwa umeridhika, na Mwenye-enzi-Mungu aridhike na wewe"
" فَٱدۡخُلِى فِى عِبَـٰدِى"
"Basi ingia katika (Kundi)la waja (Wema)
"وَٱدۡخُلِى جَنَّتِى"
"Uingie katika pepo yangu"
Hapo khofu inakutoka, unakua si moga tena wa kukabiliana na siku hiyo, nini woga? woga ni sehemu katika sehemu za Mauti, ndio maana unakua na khofu kubwa, nini Ushujaa? ushujaa ni sehemu katika sehemu za Uhai, na tafauti yake moga kajaa khofu, na shujaa hana khofu kabisa, ndio maana ukiumwa unaogopa kufa, na ukiwa mzima huogopi kutenda dhanbi.
Namuomba Mollah wangu atuweke katika utulivu wa kuikumbuka siku hii inayomkabili kila mmoja wetu, atupe takhfif itakapofika kila mmoja zamu yake, atukurubishe katika enzi yake ya kusubiri ili tupate shufaa ya tukio hili la siku ya kufa, atujaalie tupokewe kwa salama na amani katika Miliki yake ya Milele kama isemavyo aya hii ya Naziat" وَٱلنَّـٰشِطَـٰتِ نَشۡطً۬ا" Na kwa wale wanotoa Roho (Za watu wema)kwa taratibu. Amin
No comments:
Post a Comment