Asalaam Aleiykum,
Nini Imani?
Imani ni ukweli usokua na tafsiri, hakuna lugha yenye kuweza kufasiri nini Imani, njia moja tu inayoweza kukufahamisha maana ya Imani ni (Experience)kuishi katika hali hiyo ya Imani katika moyo wako, Hapo ndipo inapokaa Imani, na Imani au hali hiyo ya (Ukweli)ina sifa moja ikisha ingia moyoni haitoki tena, na chochote kiingiacho moyoni jua kimetokea kwa Mollah wako. Imani ni kitu kikubwa kisicho mwanzo wala mwisho, Imani ni mfano wa (Taa au Nuru) yenye kumurika yote yaliyomo kwenye ulimwengu huu, Imani ni taa popote penye giza inamurika ili vionekane vyote vilojificha, ndio utaona ukikaa na mwenye Imani aidha utamkimbia, kwanini unamkimbia kwa sababu woga unakua ushamtoka na anaweza kusema chochote kufanya chochote ambacho kinyume na matarajio yako, au utamfata kila anapo kwenda kwa sababu na wewe ushaanza kuonja ladha ya Imani.
Sasa nini faida za Imani?
Kitu cha mwanzo(1) kuanza kujua kuwa Imani inaingia katika nafsi yako ni pale kuondokewa na Tamaa, matamanio yanakatika kabisa, nisije kusema matamanio ukaruka na kudhani nakusudia tendo la (Ndoa)laa, kusudio hapo ni tamaa ya maisha, upate hiki au upate kile, hichi unataka na kile lazima upate, kwanini tamaa inakatika, sababu tamaa ni upungufu, Na imani ni yenye kuondosha upungufu inakujaza moyo wako, na moyo ukijaa lazima vile vyote vya nje vipungue(Inaitwa kukinai), huwezi kuwa na Imani na huku unatafuta utajiri, unataka ujenge jumba la ghorofa, huwezi kuwa na Imani ukawa unapokea Rushwa, huwezi kuwa na Imani ukawa unatesa wenzio, huwezi kuwa na Imani ukawa unapita kudhulumu wenzio, huwezi kuwa na Imani bado tamaa imekushika, huwezi kuwa na Imani ukawa unapita ukizini, Imani haikai pamoja na upungufu hilo likumbuke sana, kwani Imani ni kitu chenye kutosheleza yote pasi na kuacha hata jambo moja pembeni.
Kitu cha pili(2) kujua sasa Imani inaongezeka ni kujawa na Huruma, unaonea Huruma kila chenye kuishi, kuanzia wanyama,watu, maskini na matajiri kadhalika,wagonjwa ukenda kuwatembelea machozi yanakutoka, hakupiti kizee pasi kuwa na fikra za kumsaidia, huruma zako zinaenea katika kila chenye uhai aloumba Mollah wako.
Jambo la Tatu (3) Imani inakufunika kwa guo la upole wa tabia, mazungumzo, mpaka vitendo vyako.
Jambo la Nne (4)Imani ikifurika ndani ya moyo wako, uongo unatoweka, inakuwa huwezi kudanganya tena, huwezi kusengenya, inakua vigumu kwako kumlaghai yoyote, kila ulisemalo ni kweli tupu, wasiwasi unakuondoka, macho hayachezi tena kwa sababu uongo ushatoweka, sasa ni kweli tu ndio yenye kuishi katika moyo wako, hapo ndio mwanzo wa kuona kila mtu anakukimbia, wengine wanakuona sasa huyu anaumwa, ukimgusa tu anasema ukweli, marafiki wa uongo hawakai na wewe inakua mwiko kwako kukaa nao.
Jambo la tano (5)Imani ikifika katika daraja hii sasa wewe mwenyewe unageuka kuwa Imani, unakua taa au nuru yenye muangaza wa mfano kwa wale wenye kuisaka Imani. Na Imani ikijaa katika moyo wako inageuka (kuwa Mvuto) hapo kila mtu anataka kuwa awe pamoja na wewe na hapo ndipo jambo la sita linatokezea. Endelea part 3
No comments:
Post a Comment