Asalaam Aleiykum
Haitakiwi katika maisha haya kufanya jambo ukayumba upande mmoja kama vile baadhi yetu tunavo jilazimisha tuonekana Wacha Mungu, Mtu asivae (Joho)la Plastic ikawa yeye aonekana Mcha Mungu mkubwa kumbe akifanyiwa mtihani mdogo kayayuka, kipitie kisa cha Sheikh mmoja wa (Plastic)na mwenzie walivofanyiana mtihani "Masheikh hawa wawili walikua na kawaida ya kuvipitia vitabu vya wanazuoni, leo nyumba ya huyu kesho ya yule mwenzie, kwa bahati wote wawili wakajifunga hawana haja ya kuoa, ila wanashughulika na mambo ya kutafuta Ilmu, baada ya miaka michache kupita yule Sheikh mwenye kuaminika kwa Ucha Mungu akaamua kuajiri Msichana wa kufagia na kumpigia pasi nk, Yule mwenzie akamwambia mbona unajipa mtihani asije shetani akakushika ukaja kulala na huyu msichana, yule Sheikh akahamaki sana, akamwambia mwenzie mimi na heshimika katika jamii na sikudhani nitasikia maneno kama haya kutoka kwako, kuanzia leo urafiki wetu umekwisha na nakuomba uondoke kwenye nyumba yangu sasa hivi, natoka nje nikirudi uwe ushaondoka, baada ya muda Yule Sheikh akafunga vitabu vyake huyo akaondoka".
"Baada ya siku tatu akapokea barua kutoka kwa yule mwenzie anamwambia hivi""Sithubutu kusema kama wewe mwizi, ila ikiwa kwa bahati mbaya umeondoka na kitabu changu basi naomba unirudishie"Akakamata kalamu huyu mwenzie na yeye akaandika""Na mimi vile vile Sina dhamiri ya kukuita wewe Muongo, lakini ikiwa ungekua unalala kwenye chumba chako basi ungekiona kitabu chako" hiyo ndiyo Plastic ilivyo kuna wakati lazima inayayuka, kumbe Sheikh kafanyiwa mtihani kitabu kimewekwa kwenye kitanda chake, kumbe halali pale, ana lala chumbani kwa mfanyakazi wake, usivae juba la uongo, Ucha Mungu unakuja (Natural) huna haja ya kujilazimisha, usifanyie watu mfanyie Mollah wako na yeye atakuondoshea tabia ya kuyumba.
Mcha-Mungu ana tunongoneza tufungue Quraan sura ya Al-Hashir aya ya 18"
"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡتَنظُرۡ نَفۡسٌ۬ مَّا قَدَّمَتۡ لِغَدٍ۬ۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ "
"Enyi mloamini Mcheni Mwenye-enzi-Mungu na kila Mtu aangalie anayo tanguliza kwa ajili ya kesho(Akhera) Na Mcheni Mwenye-enzi-Mungu, hakika Mwenye-enzi-Mungu anazo habari mnayoyatenda"
Atizame Mja asiwe anayumba anapoteza muelekeo, yupo na kushughulika na mambo ya kipuuzi, umepewa (balance) ili uweze kushi katika ulimwengu huu katikati ya njia alokuwekea Mollah wako, ukianza kuyumba ushapoteza (Dira)na ukipoteza dira basi malipo yana anza hapa hapa Ulimwenguni, na kama unabisha hayo weye yumba ukione cha mtema-kuni. Tuna nongonezwa tena aya ya 19 " وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ نَسُواْ ٱللَّهَ فَأَنسَٮٰهُمۡ أَنفُسَہُمۡۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡفَـٰسِقُونَ"
"Wala msiwe kama wale walomsahau Mwenye-enzi-Mungu, na (Mollah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio maasi wakubwa"
Hii (Sense) ya sita ndio inokufanya usahau, ukipenda mali lazima umsahau Molla wako, ukiwa na kiburi lazima wakati wote ukumbuke kiburi chako, kama unapenda maharusi saa zote unafikiri sijui ntaalikwa au sialikwi, hivi ndivo ilivo hiyo hali ya kuyumba, kama mlevi asivo kumbuka sala kasahau na wewe vile vile, jipime wewe mchezo wako unaanza na wakati wa sala umefika, Jaalia ndio unakwenda kusali, tumekubali, basi sala yako mwanzo mpaka mwisho anatawala (Actor)na nini kitatokea katika hiyo story, au kama mfanya biashara ndio unahesabu faida au khofu ya kuibiwa imekujaa, hivyo ndio maana ya kusahaulishwa nafsi zao, ikiwa wewe unamsahau Mungu na yeye anakusahaulisha kabisa, na huko kusahau ndio huku kuyumba, kwanini ikawa kuyumba, kwa sababu kuna wakati unakumbuka kumbuka mara moja moja.
"Basi nyinyi waumini msiwe kama wale walosahahu, usiwaonee choyo wale walokwenda kwenye Taarab, ila waonee huruma, usiwaone wanafaida walokwenda vilabu vya pombe, ila waombee dua wawache kumuasi Mollah wao, na wewe unaambiwa usiwe kama wao, kwani hao ni maasi makubwa wanayofanya, wewe kuwa tafauti nao, na ukiwa tafauti basi jambo la mwanzo unasita kuyumba, na ukisita kuyumba hapo unaanza safari ya Ucha-Mungu.
Ananongoneza tena Mcha-Mungu tizameni aya ya 20:Endelea-part-3
No comments:
Post a Comment