Asalaam Aleiykum,
Vipi kifo hichi kinatokea, safiri namie ili nikushike mkono tupate kuhudhuria Mauti haya ya (Final Death) Kwanza kabisa napenda uelewe Mwanaadamu ni muungano wa vitu viwili, unacho kitu cha kwanza nacho kutokana na hii ardhi(Sura ya Taha aya ya 55)
" مِنۡہَا خَلَقۡنَـٰكُمۡ وَفِيہَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡہَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ"
"katika(Kutokana na) hii ardhi, Tumekuumbeni, na Humo tutakurejesheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine tena"
Hiyo ndio sehemu ya kwanza ya mwanaadamu (Pande la Ardhi) lakini kumbuka uzuri una kitu kilotokea (Mbinguni) nayo hiyo Roho ilo Tukufu, iliyo muhimu, yenye usafi ambayo ndio yenye kushereheka siku ya kuzaliwa na kuhuzunika au kufurahika siku ya kufa kwako, hiyo ndiyo (Roho) ilotoka mbinguni ikiwa safi haina doa, hiyo ndio yenye kutizamwa itafanya amali gani, hiyo ndio itakayo sutwa na ardhi kama ilivotajwa kwenye sura ya (Yaasin aya ya 65)
"ٱلۡيَوۡمَ نَخۡتِمُ عَلَىٰٓ أَفۡوَٲهِهِمۡ وَتُكَلِّمُنَآ أَيۡدِيہِمۡ وَتَشۡہَدُ أَرۡجُلُهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ"
"Siku hiyo tutaziba vinywa vyao,itazungumza mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokua wakiyachuma"
Naam hiyo ndio Roho inayo tajwa katika sura ya (Al-Maarij aya ya 4) "تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕڪَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِى يَوۡمٍ۬ كَانَ مِقۡدَارُهُ ۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٍ۬"
"Malaika na Roho hupanda kwake katika siku ambayo muda wake (Kwa makadirio)ni miaka elfu hamsini."
Sasa ikiwa hii ardhi na hiyo Roho zinapotaka kutenganishwa ndio linatokea hilo tukio zito(Ambalo nimelifafanua kwa urefu katika darsa yangu ya kukabiliwa na Mauti) hapa pana kazi kubwa sana , na hapa ndipo anapohudhuria yule (Surgeon Specilist)Malaika wa kutoa Roho, cha mwanzo kabisa kinachfanyika ni kukata mawasiliano inaondoshwa Sauti na macho vinakua havifanyi kazi tena, kama afanyavo operesheni Daktari wa kawaida, ila tafauti inayopatikana hii operesheni ya Kufa, inakua wale walokuzunguka wao hawaoni nini kinaendelea, lakini wewe mwenye kutolewa Roho umacho na unahisi kila kitu kinachotendeka.
Wanakwambia Malaika leo ni siku ya kutenganishwa na mwili wako uloishi nao miaka 60 mpaka 70 na machungu ya kutenganishwa huku ni makubwa sana hayana mfano, utatamani upewe Bahari yote ili ikate kiu yako, ikiwa mgonjwa wa saratani anaumwa anapewa dawa za usingizi hazifai, anapigwa shindano machungu hayaondoki nini habari yetu sisi kuja kutolewa Roho na huku una Mabegi ya Dhanbi, inapatikana nafuu kama utakua katika hawa walotajwa katika aya ya hizi ya sura ya Waqiah,
"فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ"
"Na kama akiwa (Mtu huyo anaye kufa) ni miongoni mwa wale walokaribishwa(Na Mwenye-enzi-Mungu)"
"فَرَوۡحٌ۬ وَرَيۡحَانٌ۬ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ۬"
"Basi ni Raha(Tupu wakati wa kutoka Roho)na Manukato(Harufu nzuri) na Mabustani yenye neema"
Na kama utakua katika kundi la Muumin wa kawaida umemtii Mollah wako, imekuingia khofu ukaanza kutenda mema basi unaambiwa,
"وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَـٰبِ ٱلۡيَمِينِ"
"Na kama akiwa ni miongoni mwa watu wa kheri(Muumin)"
"فَسَلَـٰمٌ۬ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَـٰبِ ٱلۡيَمِينِ"
"Ataambiwa ni Salama kwako, (wewe)miongoni mwa watu wa kheri"
Hapo unapata Nafuu ya kuondoshewa machungu na dhiki za utokaji wa Roho, unapewa ganzi ya kuondoshewa fahamu na unakua kama vile mtoto anavozaliwa. Lakini kama ulikua umeishi maisha yako kwa njia ya ufisadi na una mizigo ya Dhuluma, basi unaachiwa kushuhudia mambo yote (Live).
" وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ "
"Na kama akiwa ni miongoni mwa walokadhibisha, wapotofu"
"فَنُزُلٌ۬ مِّنۡ حَمِيمٍ۬"
"Basi karamu(Yako) ni maji ya moto yachemkayo(ili ukate kiu).
" وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ"
"Na kuwaka (Katika)moto"
Na kama unahisi utayaweza hayo hebu jaribu japo dakika moja kuzuia pumzi uone vipi unakua, hali hiyo unokua nayo sasa igeuze mara elfu moja ndio utapata kwa uchache vipi Roho yako itatoka, kwa sababu katika kutoka Roho kuna (Vital Energy) lazima ikatwe. kutaka kuijua hiyo Energy Endelea-Part-3
No comments:
Post a Comment