Asalaam Aleiykum,
Nakukaribisheni kwenye darsa hii "Enyi" wacheza (Birthday) Na wewe mkumbukaji wa siku yako ya harusi(Anniversery) na hata yule mpiga mayowe ya kuzaliwa kwa chama chako, Mbona umeisahau Siku ya kufa kwako, wakati unajua ipo, inakuja na ishakaribia. Nikisema ipo maana yake imetuzunguka kila siku inatokezea, lakini kusudio langu ni ile mnayoifahamu ya mtoto mdogo(Kichanga), Na hii ya pili yakuja, hiyo inawahusu vijana kuwa japo mmesahau lakini mgeni yuko karibu au pengine keshafika, anasubiri umkaribishe au yupo kwa jirani akitoka hapo anakuja kwako. Na ama hii ishakaribia, hii ni ya watu wazima kifo kishatoa taarifa, kimeshagonga mlango, tayari kimeshatanguliza dalili, Viungo vyote sasa vinaelekea kusini, kwa sababu ulivokua mdogo vilikua vinaelekea kaskazini, ulipofika ujanani vikarejea katikati, na sasa umekua mzee vinataka kurejea vilipotoka.
Vimeshaleta ishara labda una magonjwa ambayo hayaponi tena, pengine nywele zishapiga weupe zimekua rangi ya kitambaa cha sanda, na mpaka nguvu za kukimbia zishatoweka, kutembea pia kwa mashaka, Mauti yashahudhuria na wewe huna tena amri ya kuzuia tukio hilo.
Sasa nini cha kufanya? Ukitaka kujua cha kufanya ili upate (Tahfif)siku hiyo itakapo dhihiri, basi niazime macho yako ili iwe (Tochi)yetu nikutoe kwenye kiza nikupeleke kwenye(Mwanga)Taa ya kufahamu vipi siku hiyo upate nafuu ya vishindo vyake, Na kabla hatujenda huko wacha nikujulishe nini Mauti?, Mauti ni jambo moja na Uhai vina uhusiano wa karibu, ni vitu venye kushirikiana sana katika kazi zao, najua utashangaa, ni wajibu wako kushangaa, ila kumbuka mwenye kushangaa ndie anaefahamu vizuri, mfano wa wa mtoto mwenye kuuliza hichi nini na hichi nini.
Sasa na tuanze na kuitupia macho aya inayotujulisha nini Mauti na nini Uhai, Aya ya 1-2 sura ya Mulk.
"تَبَـٰرَكَ ٱلَّذِى بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ"
"Ametukuka yule ambaye mkononi mwake umo ufalme(Uwezo wake)Na yeye ni mwenye uwezo wa kila kitu(Yeye ndiye alomiliki haya maisha)"
"ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلاً۬ۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ"
"Ambaye ameumba Mauti na Uhai ili akujaribuni(kukufanyieni mtihani) ni yupi miongoni mwenu atakae tenda vitendo vizuri, Naye ni mwenye nguvu na mwenye kusamehe"
Naam: Aya ya pili imeanza mwanzo kwa kutaja mauti, unajua sababu gani ikawa hivyo, kwa sababu Mauti ndio mlango unaopita ukatokezea kwenye Uhai, mwanzo ulikua hupo katika maisha haya, na mfano wa hayo tizama Mti, kabla mti haujawa mkubwa inakuwepo mbegu, na hiyo mbegu lazima ife chini ya ardhi ili mti upate kuzaliwa, na wewe vile vile mfano wako ni kama huo, maumbile yako yanaanzia tokea tumboni, lazima Mauti yashirikiane na Uhai, kwa wale wenye Elimu ya (Ukunga)au uzazi wanafahamu hilo vipi (Cells)hizi zinavofanya kazi na kufa na kujitoa (Copy) ili wengine waendelee na kazi.
Inaendelea kawaida hii katika umri mzima wa mwanaadamu mashirikiano ya Mauti na Uhai bila ya kuleta maumivu kwako, inafanyika (Process) hii ukiwa hai , hichi lazima kife ili kile kizaliwe , yanakutokezea Mauti yakenda sambamba na uhai ndio maana unaona tafauti ulipokua mtoto, na ukawa kijana na mpaka sasa mtu mzima hiyo ni (Biological death) nilikua naitaja japo kwa ufupi kuonesha taathira za mauti, katika vazi la Umbile, Sasa hapa itabidi mnistahamilie niingie upande wa pili wa kusudio la hiyo aya ya pili sura ya Mulk, ambayo munasaba wake ni kutujulisha(Spritual Death)Kutoka kwa Roho. kutaka kuyajua hayo Endelea Part-2
No comments:
Post a Comment