Asalaam Aleiykum,
Leo pokea bahasha ndani yake utaikuta Barua Adhimu ya Ukumbusho, fungua uisome Barua hii kwa utaratibu wa fikra ili umalizapo kusoma na wewe upate kuijibu kwa shauku na hamu kubwa, na ipe umuhimu wa pekee kwani utaulizwa jee hukuisoma Barua ya Ukumbusho?. Jee kwani wewe ilikua haikuhusu barua hiyo? mbona basi mliachia watu wachache kuandika barua hiyo.
Barua hii inatoka wapi na inakwenda kwa nani? Barua hii Inatoka kwa Mpenzi Mollah wako kwenda kwa vipenzi waja wake wakiwemo mimi na wewe, Anakuagiza Mollah wako wapelekee vipenzi vyako wote wakaribu ujumbe huu wakiwemo, wa kwanza mkeo au mumeo, kama kweli unampenda, ikisha wanao damu yako unayo ionea huruma, halafu tena wazazi wako wawili, na baada ya hapo wote walo karibu katika familia yako.
Anza kwa kuwaandikia barua hii au wasomee njia zote mbili zinafaa, na wa mwanzo muanze mkeo au mumeo na hao wawili imewahusu sana kwa sababu wao wako karibu sana mpaka malazi yao yako pamoja. Halafu tena wanafatia watoto wako au wazazi wako wawili, yaweza kuwa makaka zako au madada zako na pamoja wote walio karibu yako katika mahusiano ya kiroho, wote hao wasomee barua hii.
Naanza Barua hii kwa Jina la Mwenye enzi Mungu mwingi wa Rehma Mwenye kurehemu, Naandika Barua hii nikiwa na hisia za mapenzi kifuani mwangu,(Kwanini zikawa hisia?)kwa sababu mapenzi ushayamaliza kabla hayajaanza katika hiyo(Ndoa)ndio maana kutwa mnaparurana, imekuaje hali hiyo, imekua hivi, unampenda Sharbanu unamuoa Shabira, umeolewa na Abdulla unampenda Baja, hizo ndio hali zetu tulivyo, mume au mke anakua (Mfano)tu uko naye lakini unamungunyika ukimuona yule ulomtia moyoni, vipi leo utaruhusu mapenzi yatokezee kwenye moyo wako, wakati moyo wenyewe ushaufunga, na ungekua wazi moyo wako na mapenzi yametokezea basi (Wallahi)ungekua ushaandika Barua hii siku nyingi au ushaisoma maneno yake tokea kitambo huko nyuma, na kama hujaandika basi pia hujachelewa anza leo, Vipi?.
Naam: Mimi zimenijia hisia za mapenzi kifuani mwangu, halafu nikafunikwa na khofu kichwani mwangu ya kwamba mimi nimo hasarani ya kukukosa wewe hapa Ulimwengu na kesho huko Akhera, na nimekubali kustahamili kukukosa hapa Ulimwenguni, kwani unaishi katika jumba la damu, jumba la usaha, jumba la wadudu, mkusanyiko wa mifupa na nyama na ndio maana unapokufa naufanyia ukarimu mwili wako kwa heshima ya kukuzika haraka sana, mpelekeni ataharibika, atatoa harufu msimweke muda mrefu, yote hayo nayasema mimi mwenyewe, na nimekubali kuyavumilia hapa Ulimwenguni, Lakini nisichoweza kukisubiri na kukinyamazia kimya ni ile hukumu ya Roho yako itakapoamuliwa sasa ikaishi na kuteseka Motoni, ama kwa hilo nimeshindwa kuvumilia ndio maana hii leo nakuletea Barua hii nikitumai utaipa zingatio la umuhimu wa kipekee ikiwa wewe ni mwenye kumogopa Allah na kufahamu umeumbwa na leo au kesho unaweza kuondoka katika Ulimwengu huu bila ya taarifa yoyote ile.
Kwanini nikayasema hayo?Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment