Asalaam Aleiykum,
Nani huyu Mwenye kuuliza kama atakwenda Peponi au Motoni, Nani Muulizaji wa Swali hili, yaweza kuwa mimi au wewe, sote tuna shaka, sote tunakiu yakutaka kujua, kwanini tukauliza? lazima (Deep) katika hiyo (Being) yetu kuna (Jawabu)linaelea lakini hatujui tulijibu vipi, Muulizaji kajaa mashaka, wasiwasi unamjia kila mara, woga unamgubika kila akisikia mwenzie (Kafariki) anaendelea kuuliza Muulizaji, Huyu fulani kenda wapi, na sasa hamu inamjia anataka kujijua yeye nani na atakwenda wapi wakati wake ukimalizika hapa Ulimwenguni, swali hili linawasumbua wengi na kuwatia mashaka makubwa katika Imani.
Nani Muulizaji? Huyu Mwenye kuuliza Daima yeye anauliza Nje na hata siku moja hajapata kujiuliza Ndani kwake, Na wakati kaambiwa wewe Mwenye mashaka, wewe mwenye Imani hafifu, Adh-Dhariyat 21"وَفِىٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ"
"Na katika Nafsi zenu Je Hamuoni"
Ushawahi kujiuliza mbona kuna mambo Mtu wa nje yoyote hayajui, si Mkeo wala wanao, si wazazi wako au ndugu zako, Bali ni wewe Mwenyewe unaeuliza ndie unayeijua siri hiyo, sasa Nani Muulizaji huyo? Nani Mwenye kujua sasa hivi Kichwa kinaniuma, Nani Mwenye kujua njaa imenishika, Nani Mwenye kujua sasa hivi Sikio linaniwasha, Nani Mwenye Kujua jana niliota Nini, Nani Mwenye kujua sasa hivi nishashiba nisiendelee kula, hayo mambo yote na mengine chungu nzima ni lazima uyaseme Mwenyewe ndio watu wa Nje wayajue, (Narejea tena wayajue)hakuna yoyote awezaye kuyahisi, (Unaweza kuwa uongo au kweli)shahid wa hilo ni wewe Mwenyewe, kwani kuhisi ni wewe peke yako huna mshirika katika hilo.
Napenda Uelewe hapo unapohisi ndio Jirani yako wa (Ufalme wa Nafsi yako)Ndio karibu yakaapo Mamlaka ya hiyo Roho yako, Sasa ikiwa ushagundua hilo kuwa mimi na hili Jumba langu ninalo ishi ni tafauti, kwanini ikawa Tafauti, kwa sababu kuna (Gap)baina ya kuhisi na kugundua wewe fanya uchunguzi utafahamu hilo(Leo si sehemu yake ya kulifahamisha hilo, ndio maana ukaambiwa katika nafsi zenu hamuoni, hapo ishapatikana Separation)hapo utajua ikiwa ipo hiyo tafauti baina yako na jumba lako la udongo, basi hicho chenye kutafautisha ndio mimi Muulizaji, Na utapata uyakinifu kitu hichi kinachoitwa mimi lazima kina pahala kilipotokea, na ukisha kulijua hilo basi moja kwa moja unaelewa lazima kuna siku na muda maalumu ya kurejea huko kilipotokea, Na baada ya kupata hakika hiyo, Lazima utafute (Source) ya mapenzi ya kurejea utokako, na ujitaarishe kuchukua zawadi gani, na hapo tena unakubali yupo aloniumba mpaka akanifikisha katika Ulimwengu huu, lazima iko safari mimi nilifanya mpaka nikafika hapa, na lazima nitarejea tena huko nitokako, ni bure kujenga kwangu majumba, ni bure kujilimbikizia mali, ni bure kufanya fisadi na chuk,i vyote hivi nitaviacha na nitarudi peke yangu kama nilivyokuja mwanzo.
Nani Muulizaji? Muulizaji kumbe ni mie ambaye sasa nakubali, sio kuamini tena, bali sasa imekua kukubali, na kukubali ndio hiyo (Surrender-Islam)na uki (Surrender) tu unafungukiwa na ufahamu wa mambo vyengine kabisa, sasa unakwenda (Beyond)unahama kwenye (Knowledge)unatupa elimu yote unaishi kwenye (Understanding) na ukipata huko kufahamu ndio hekima, na hapo Muulizaji unageuka kuwa mwenye kujibu kama inavoendelea aya ya 22 ya sura hiyo hiyo ya Adh-Dhariyat.
Endelea part 2
Sunday, January 26, 2014
JAWABU LA ROHO PART 2
Asalaam Aleiykum,
"وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ"
Na katika Mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa(Promise)
Sikiliza "Ewe"Muulizaji ahadi zote zipo na kuwa na uhakika zitatekelezwa kwa Amri ya Mollah wako, Na katika Mbingu kuna Riziki zenu, Makusudio yake uwe unajua kila unacho chuma hapa Ulimwenguni, ikiwa wewe Mkulima au Mfanya Biashara, au uwe Mtu wa kawaida, Basi Elewa kila ukiamka Riziki yako ishapangwa Mbinguni kiwango chake Maalumu, Na hata ukifanya nini huwezi kuzidisha wala kupunguza, ila uamue Mwenyewe, Na unaruhusiwa kuamua , Unaruhusiwa kufanya vita na Mwenye Enzi Mungu, kwa Kuwanyanganya wenzio Riziki zao kwa Nguvu, Unaruhusiwa kufanya (Booking)yako ya mateso ya Moto kwa mkono wako mwenyewe, kuchukua mali za watu, kudhulumu majumba ya watu, kudhulumu maskini, kuwatia katika dhiki walochini kwa kujilimbikizia mali, kwa hilo unapewa ruhusa ili ukaribishe matatizo yatakayo kukuta Milele na hilo halina Shaka.
Kwa hiyo huku kuhangaika kwenu ni Bure kabisa mtowaji yupo na kajitaja kwenye sura ya (Banii-Israel-aya ya 30)
إِنَّ رَبَّكَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ إِنَّهُ ۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرً۬ا
Hakika Mollah wako Mlezi humkunjulia Riziki amtakaye, na humpimia amtakaye, Na yeye kwa Waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona.
Na kawaida Yake Mfalme wa hiyo Riziki yako kuwa ukizidisha kwa kutoa Sadaka, Na yeye anakuongezea kwa njia unazo zifahamu na usizozifahamu. Na kila kitu kinapangwa huko Mbinguni, upande wako wewe unatakiwa upige hatua ya kukielekea hicho kitu, na hapo utaona milango inafunguka bila ya wewe kutarajia, ikiwa umepangiwa uende University utakwenda, ukiwa umepangiwa uwe Tajiri utakuwa, Ikiwa umepangiwa uwe Rais utakuwa, ukipangiwa uwe chochote unakuwa na wala hili usilitilie shaka, ukitakiwa uwe Mwalimu utasomesha tu, kila pato lako limepangwa na yeye Mwenye kuwajua viumbe vyake, Na ndio athari yake utaiona tukiomba Dua unaelekeza mikono Mbinguni (Juu) kwa ishara ya kuomba, Unajua kwanini? Kwa sababu Roho inajua ilipotokea na inaelewa wapi hizo Riziki zinapopangwa.
Nyanyua macho upatazame uzuri Mbinguni kuna mambo ambayo huyaoni, halafu wacha zikujie fikra kuwa kuna siku na wewe utafanya safari ya kwenda huko mbinguni muda wako wa kuishi ukimalizika, lakini kabla ya kusafiri kuna (Interview)mahojiano lazima yafanyike hapa hapa Ulimwenguni, Na yanafanyika mahojiano haya wapi?
Endelea part 3

JAWABU LA ROHO PART 3
Asalaam Aleiykum,
Yanafanyika mahojiano hayo chini ya ardhi au juu ya ardhi, inategemea wewe wa Dini gani, hapo havuki mtu, usione labda utakimbia kwa kuchomwa moto au kucheleweshwa kuzikwa, ni lazima mahojiano hayo yafanyike kwa muda usiozidi siku tatu, ndio maana mkaambiwa msiba siku tatu, Nabii Isa a.s anasema kwenye Injili(Biblia)Ntakaa kwenye tumbo la Ardhi siku tatu, (Mfano wangu kama Mfano wa Yunus, kukaa ndani ya tumbo la samaki chewa siku tatu)Na wewe Ardhini lazima ukae siku tatu kabla ya kuanza safari yako, ukimaliza kufukiwa tu wanatokezea watu usowahi kuwaona, viumbe wa aina nyengine, Nuru zao zinakuunguza, wanafanya nini? wanakupiga Begani fungua sanda tushafika sisi tuna mazungumzo na wewe, na hao wenzio wenye kuishi huko juu ya Ardhi wametufanyia hisani kubwa ya kukutia manukato ili huu mwili kabla ya kutoa harufu tuelewane uzuri kwa haya tutakayo kuuliza, Sasa ikiwa hapa Duniani unaulizwa (Confirmed Date of Birth)Chini ya Ardhi kuna Maswala matatu muhimu ya mwanzo, (Hapa ndio Bwana Mtume s.a.w )alikua akisha kumzika mtu anawaambia Masahaba muombeeni ndugu yenu hivi sasa anaulizwa.
Anaulizwa nini? Siku hii sote itatukabili na siku nzito ambayo ishasemwa na huko Mbinguni yapo yalee tuliyokua tunakupeni ahadi nayo, kuwa mtayakuta. Swali la Kwanza nani uliyekua Unamuabudu?, Ndugu zangu ikiwa umekufa hujarudi kwa Mollah wako, basi hapo Roho inakaa kimya inajibu (Mind) Akili yako Muimbaji fulani, Kinacho kufika hapo mimi sikisemi ila fikiria mwenyewe ile mbao na dongo ulofunikwa nalo futi 6 hali inakuwaje huko chini.
Swali la pili nani huyu uliyekua unamfata aliyekuletea ujumbe, tena hapo kama ulikua hutoki kwenye Computer unajibu (Face book), Na swali la tatu ulikua ukifata dini gani, unajibu kwa haraka haraka (Wassup) hapo watu hawaendelei tena na maswali hakuna faida wanajua umejaa mambo ya mjini, kila utakachoulizwa utatoa Story za mjini, kiza kinachokua hapo hata ukitaka kukumbuka labda imekujia duh nishafuja unataka kusema Allah, wapi ulimi ushatiwa Nanga nzito, ee una vidonda vya mdomo huwezi kula na tafran tele vipi leo ufungwe Nanga ya Meli nzima kwenye Ulimi huo hali inakuaje?. Hali inatisha katika Giza la kaburi ndugu zangu, ndio maana tukiomba tunasema mtilie kaburi lake Nuru. Hiyo ni (Interview) ya ile Roho ilosahau ikagubikwa na maasi, fitina, choyo na unyanganyi katika Ulimwengu huu.
Ama Yule Mwenye kukumbuka akawa anafanya yalo mema na kila saa kumtaja Mollah wake yeye kashushiwa Aya anaondoshwa wasiwasi, anaambiwa asiogope kaburi wala hiyo (Interview)Mahojiano, ikiwa wewe ulikuwa Muumin wa kweli basi soma aya ya 27 Surat Ibrahiim ili ikupoze na kadhia ya siku hiyo,
"يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِى ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِى ٱلۡأَخِرَةِۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّـٰلِمِينَۚ وَيَفۡعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ"
"Mwenye Enzi Mungu huwathibitishia waloamini kwa kauli thabit, Katika Maisha ya Dunia na katika Akhera, Na Mwenye Enzi Mungu huwaacha kupotea hao Wenye kudhulumu, Na Mwenye Enzi Mungu hufanya apendavyo"
Hiyo ndio kawaida ya Ahadi ikiwa umeishi vyema kwenye Ulimwengu huu basi wewe utakua mwepesi na huko chini ya Ardhi kuijibu hiyo (Interview), Utatoa Jawabu Mollah wangu ni Mlezi aliyeniumba kutokana na Udongo huu nilolalia, akaufanyia ujuzi wa hali ya juu katika maumbile mpaka sasa nikawa nakujibuni kutumia huu Ulimi aloniumba nao Mollah wangu. Na huyo niliyekua namfata ni mjumbe wake aliyemtuma kwetu sisi waja wake, namie nikayaamini aliyotuletea, Na nikaifata hii Dini ya Kiislam kwa ukamilifu kama ilivotakiwa, Na sasa najisalimisha kwake Muweza wa kila jambo, Na Naridhia kila alonipangia Mollah wangu ambaye anafanya mambo yake kwa haki na anavotaka yeye, Napia nataraji atanisamehe kwa yote nilomkosea kwa kuwa mimi sikua mkamilifu kama alivonitaraji, Na hili ni jawabu la Roho yangu na yako siku hiyo itakapowadia.
Namuomba Mollah mwenye kuyajua ya Siri na ya Dhahiri, niloyafanya na ninayokusudia kuyafanya, anipe ridhaa ya kusamehewa na kuishi katika Enzi yake ya Utukufu wa Ulimwengu huu bila ya kumkera yeye ama viumbe wenzangu, aisafishe Roho yangu niwe Nampenda kila Mtu na kila Mtu awe ananipenda mimi kwa kadiri ya Uweza wa Roho hiyo. Amin.

Sunday, January 19, 2014
MSIBA WA NDOA PART 1
Asalaam Aleiykum,
Unazijua Nyumba zilofikwa na Msiba huu wa Ndoa, Umeshawahi kuhudhuria makaburi hayo ukaona vipi wana Ndoa wanavyoteseka, Na kwanini nikaita msiba kwa sababu wanandoa hao wanaishi ndani ya kifo cha Mapenzi, Wamefikia mpaka kutoka katika Rehma za Mollah wao, Watu hao ni wale wenye kuishi katika Ndoa isiyokua na Mapenzi wala masikilizano, Na Ndoa kama hiyo Mwenye Enzi Mungu anaiondoshea Rehma zake kabisa, Na ikiondoshwa Rehma katika hiyo ndoa utaona kila mmoja anatafuta mvinyo wake wa kumlaza, utaona Wanaume watakua wanazama kutafuta na kuthamini Marafiki kuliko Mke, Au anakwenda nje kufuga (Kimada)au anatafuta (Uraibu) wa aina yake ili ajisahaulishe huku akidhani mambo yatakaa sawa yenyewe.
Na Mwanamke Ima atabaki na huzuni, pamoja na malalamiko, au atatafuta Mashoga apate kujisahaulisha na (Kadhia)yake ya kuharibika kwa ndoa yake, au na yeye atatafuta kipoza Moyo(barobaro)afanye urafiki nalo. Sasa Jiulize kwanini Ndoa yako imefikia Hali kama hiyo, Na kwanini unaichia iendelee na kufanya kama jambo la kawaida.
Katika Darsa ya leo nadondosha Siri iokote upate kuitumia, ifanyie kazi upate kurekebisha Ndoa yako, Usikubali tena kuishi ndani ya kaburi la Mapenzi, Nia yangu sio kukutenganisha au kuvunja Ndoa yako, Dhumuni langu ni kuuhisha au kuirejesha kama zamani ilivyokua, na wala usione labda nishazeeka Ndoa ya nini, laa Ndoa ni ngazi ya Mapenzi ya Mume na Mke, Na Mapenzi hayo yakikamilika mkaungana kikweli basi yana kupelekeni moja kwa moja kwa Mollah wenu, Mnageuka baada ya kupendana nyinyi mnampenda Mollah wenu na hilo ndio dhumuni la Ndoa.
Anasema Mwenye Enzi Mungu katika Quraan sura ya Rumi aya 21.
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ
"Na katika Alama zake,Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila shaka katika haya kuna ishara kwa watu wanofikiri"
Wewe mwenye kumtesa huyo mwenzio, Napenda uelewe hizo unazozitesa na kuzipiga vita na kumkimbia mwenzio basi unazipinga na kuzikanusha Alama za Mwenye Enzi Mungu"
"Ewe Mja ametajwa Mke ili kwa kuambiwa wewe Mwanamme kuwa huyo ni jinsi yako, Imekua jinsi hiyo ya Maumbile mpaka kufanana naye, hebu angalia kwa pembeni hivyo jee mimi na Mke wangu tunafanana, Jee sisi ni (Soul Mate) Hebu kuwa Mja wa Fikira kwanini namtesa Mwenzangu, Nilipomuoa mwenzangu huyu Mollah wangu alichukua ahadi ya kutujaalia Mapenzi na Huruma, viwili hivi leo vipo wapi, nani kaviondosha? Na kwanini vimeondoka, mbona mimi nakimbilia nje? Jee hii ni Ishara ya mwanzo wa Adhabu yangu.
Mollah alipopanga waishi Mke na Mume ilikua Dhumuni lake wapeane (Company) Awe Mbize Uwe Mboza, Awe Laila Uwe Majnu, awe Habiba uwe Habib, vipi leo unakwenda kufurahisha watu wa nje, nini kimekusibu Mja wewe, au haya yalokusibu kwa sababu ya kwenda kinyume na maneno ya Bwana Mtume s.a.w "aliposema" Yoyote yule atakae muoa Mwanamke kwa ajili ya kuyatunza macho yake, kuwa na tahadhari (Katika maisha yake) Na kuwatunza familia yake kwa Huruma, Basi Mwenye Enzi Mungu humtilia Baraka mwanamke huyo kwa mumewe, Na Mume kwa Mkewe, Tizama leo vipi unaifanyia familia yako, hivyo unafikiri Mlipaji hayupo? au unadhani hizo sio Dhanbi? Na kama ukigundua hayo makosa basi fanya haraka uyarekebishe ili ufanye (Tahfif)siku yako ya kutolewa Roho.

MSIBA WA NDOA PART 2
Asalaam Aleiykum,
Mwenye Enzi Mungu kasema kama utaona Mambo yameharibika, An-Nisai aya ya 128,
وَإِنِ ٱمۡرَأَةٌ خَافَتۡ مِنۢ بَعۡلِهَا نُشُوزًا أَوۡ إِعۡرَاضً۬ا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡہِمَآ أَن يُصۡلِحَا بَيۡنَہُمَا صُلۡحً۬اۚ وَٱلصُّلۡحُ خَيۡرٌ۬ۗ
"Na kama Mke akiona Mume wake (Anamfanyia)magonvi au kutengana, basi si vibaya kwao wakitengeneza baina yao suluhu, Maana suluhu ni kitu bora(Chenye kheri)"
Napenda uelewe suluhu si ushindi na kama huyo mwenzio haitaki suluhu basi kuna mambo mawili lazima uyaangalie, na ikisha yafanyie uchunguzi wa kina mambo hayo mawili la kwanza ni(1)Kubadilika, Mfumo wa Tabia uloandamana na mazoea ya Akili, Kama litafanyiwa kazi hili lipasavyo mtu anaweza kubadilika, kumbuka huyo mwenzio mwanzo hakua hivyo ndio maana unaita kabadilika, kinachotakiwa kufanywa ni kwenda kwenye mizizi ya Mbadiliko wenyewe na kuanza kuufanyia kazi, (Mfano)wa kwanza labda Mume anapenda (Vimada)Muulize kwanini? Tatizo liko kwako au kwake sisitiza lazima upewe sababu, kwani hao walo nje na wewe hamna tafauti, isipokua kuna sababu itafute uifanyie kazi, labda kuna vitafunio hapati, vitafute mwenyewe utajua kama chakula au vitu vyengine.
Pengine yaweza kuwa mwenzio anapenda kutumia Ulevi wa aina fulani chunguza sababu zake nini kufanya hivyo, kuna mambo mengi yanasababisha hali kama hizo, yaweza kuwa anataka kuilaza akili yake labda asikumbuke madeni, au biashara imekwenda vibaya, au mtu kaondokewa na alo wake na sasa matafran yamemshika hajui afanyeje, hayo yote yanachangia kuanzisha misukosuko katika majumba na ndoa zikawa kama misiba, kila mtu anaingia na hamsini zake.
Sasa nini kinatakiwa mmoja katika nyinyi awe mvumbuzi wa mambo, na mambo yapo mengi ya kuifanya nyumba iwe na (Surprise) mpaka wageni wakiingia wanashikwa na mshangao na kusema (Haya Mambo)ikiwezekana chezeni (Foliti)Mchezo wa kujificha, Mwanamke ifanye Nyumba yako kama (Nursery)kwani Mwanamme ni kama mtoto na kila siku anataka (Kitu kipya cha kuchezea) Isiwe kazi yako umekaa kwenye Sofa na (Big G)mdomoni unaangalia kipindi chako cha TV, Kwa hilo hakai mtu ndani atakimbia.
Na la pili(2) ni hili la kusamehe, (Waingereza)wametumia neno zuri sana waliposema (Forgive)unaweza kuyafasiri hivi (Kwa wewe na Kupa)hiyo ndio (Forgive) hiyo ndio kwa wewe nakupa, unampa nini? Inaweza kuwa (Second Chance)Unampa kwa maana hutaki malipo, Unampa hutomuadhibu kichini chini wala hutomlipia kisasi, Unampa nafasi ajirekebishe sababu unampenda, Na mapenzi hayajui kuadhibu, Mapenzi ni yenye kutoa na hayajui kuchukua, Na hiyo ndio (For give) kusamehe na ukichambua sana mwisho utaikuta inasema (For love) kwanini? Kwa sababu mwenye chuki hasamehe, hana sifa hiyo. Ikiwa wewe unaweza kusamehe basi jijue kwenye moyo wako kuna Mapenzi, na Mapenzi mwenzie Subira, Ndio maana baada ya kusubiri sana alipopona nabii Ayoub a.s akaambiwa Mkeo kafanya utundu basi Msamehe kwa kufanya nini?
endelea part 3

MSIBA WA NDOA PART 3
Asalaam Aleiykum,
وَخُذۡ بِيَدِكَ ضِغۡثً۬ا فَٱضۡرِب بِّهِۦ وَلَا تَحۡنَثۡۗ إِنَّا وَجَدۡنَـٰهُ صَابِرً۬اۚ نِّعۡمَ ٱلۡعَبۡدُۖ إِنَّهُ ۥۤ أَوَّابٌ۬
"Na Chukua majani mkononi mwako, kisha mpige nayo(Mkeo kwa kiapo ulichoapa kuwa utampiga kwa mabaya alofanya)wala usivunje kiapo, Hakika tulimkuta ni mwenye subira, Mja mwema, kwa hakika alikua mnyenyekevu sana".
Ewe wa (Ayoub)chukua jani umchape mkeo, hapa walovamia tafsiri wakadhani wapigeni wanawake, vipi Mollah wako aagize wanawake waonewe, itakuaje habari hii kuwa watu wamepewa amri ndani ya Quraan wawapige wake zao, Wanashindwa kufahamu Ujumbe uliomo kwenye aya hiyo, Ujumbe unasemaje?
Kwanza kabisa zinavunjwa dasturi zenu za viapo, kwamba ukimwambia mkeo naapa ukenda kwenu ndio itakua (Talaka)yako, Maskini na yule Mke akitoka akenda kwao inakua Balaa, wewe bado unampenda na mke bado anakupenda, lakini katikati mnamkuta Sheikh kavaa (Juba)lake bila ya fikira yoyote anasema Talaka imesihi, Talaka itasihi vipi wakati katikati kuna (Kiapo)na kiapo kinavunjwa kwa kafara, na hiyo ni zawadi ya kuweza kuzitunza ndoa pengine watu wamezaa, au wanapenda kwa ajili ya Mollah wao, wewe unaingia kati na kuwaachisha, nani alokwambia (Talaka)imesihi, itasihi kama wakitaka, na itavunjika ikiwa watatoa kafara, hakuna ukenda harusini ndio Talaka yako, msifanye mchezo huo mnawatia watu matatizoni na kusababisha vizazi kusambaratika na watoto kukulia katika makaazi ya mama peke yake. Naam na la pili chukua Jani umpige nalo ili ukivunje hicho kiapo, kwani kiapo kina mashaka, kiapo kinakutia maradhi, kiapo kinatoka na (Energy)maalumu na ni lazima kivunjwe ili ipatikane salama, Basi "Ewe" Ayoub, chukua jani, kwanini majani, si mnajua majani ni dawa, na yapo ya aina nyingi, unaambiwa hii saga ujipake utapona, hii chemsha unywe utapona, na kwa kuwa Nabii Ayoub a.s anampenda Mke wake basi kwanini achishwe nae, kwa hiyo mpige kwa Jani, unajua kuna nini katika Jani lile, mbali ya kuvunja kiapo? kuna (Transformation)imepatikana kwenye Jani lile, Mke wa Ayoub kapigwa na Mapenzi ya (Nature), Kapigwa kwa Ishara ya kusamehewa, (Chemical)zimemuingia zikambadilisha akarudi kwa Mumewe kwa mapenzi makubwa, Na hayo hayo Majani ndio kitu cha mwanzo Nabii Adam a.s na Bibi Hawa walipogundua (Sehemu zao za Siri)waliyachukua na kujifunika, na hayo hayo majani mpaka hii leo ndio tunavaa nguo zetu.
Na wewe katafute majani yako umpige nayo mwenzako ili upate kumsamehe mpate kuanza tena kama Nabii Ayoub, Pata subira ya Nabii Ayoub, kuwa na wema kama alokua nao Nabii Ayoub, kuwa mnyenyekevu upate kuzidi kupendwa,(Natoa Tahadhari usende ukatafute Jani la Mirungi Utamkosa mwenzio)
Naam Unapata njia ya kusamehe ili uitunze ndoa yako, Na jambo la tatu ni hilo la kujiuliza kwanini visa vyote, na magonvi yote bado mko pamoja, Jawabu kuwa hiyo ndoa yenu imefungana moyoni, bado mnapendana, lakini Akili zenu zimetafautiana, nyoyoni nyote baridi, lakini kichwani kila mtu anamuua mwenzie kwenye ndoto, lakini moyoni kuna kitu kwako na kwake bado hakijatoka ndio maana mpaka leo mko pamoja, sasa mkikigundua hicho kitu mnakua hamna haja ya magonvi, ama kama hamjakigundua kikatoka chenyewe basi hamkai hata dakika moja pamoja, na hivyo ndio inatokea kila siku kwenye mdomo mnagombana kwenye moyo mnapendana, Na moyo ndio wenye nguvu kwa hiyo unaamua kustahamili labda atabadilika, vituko vinaendelea, adhabu zinazidi na hapo unakua unaishi kwenye msiba wa ndoa, na unasahau kama unaweza kustahamili visa vyote, na adhabu zote, kinakushinda nini kuondoka ukafanya majaribio kuona jee huyu atanimiss, jee atanitafuta, Na kama huyawezi yote basi nyanyuka Umshtakie Mungu , Useme nakuomba Mollah wangu uwezo wa kuondoka sina, na Kukaa sasa nishachoka Madhila haya , sasa na nyamaza kimya nijengee jumba langu peponi, na sasa nayabadilisha mapenzi haya kugeukia kwako Mollah wangu naomba nipokee, Na huyu Mume wangu akiingia basi nimuone kama kabati. Amin.

Sunday, January 12, 2014
UCHUNGU WA MAMA PART 1
Asalaam Aleiykum,
Nani awezaye kuujua Uchungu wa Mama pale anapo ondokewa na Mwanawe kwa ajili ya Fardhi ya (Kifo)Pengine anafariki Mtoto huyo kwa Ghafla, au unapata habari mwanao keshatangulia mbele ya haki, au unamshuhudia mwenyewe yanamkuta umauti. Yupo atakayeweza kuelezea japo kidogo hali anayokua Mama huyo wakati hukumu hii ya haki inapitishwa, Mwenye Enzi Mungu kashapitisha amri yake anahitaji kiumbe chake kirejee, na sisi hatujui siku gani kiumbe hicho kitahitajiwa, desturi yetu tunaridhia ikiwa mtu (kesha kula chumvi) au anaumwa hapo tunakiri, tunasema bora kapumzika, lakini nini habari yetu sisi ikiwa huyo alotangulia mbele ya haki ni mtoto mdogo, vipi tunaupokea msiba kama huu, hususan kitoto kishakuja Ulimwenguni na kimepata mahusiano na sasa kinaitwa mtoto wa fulani, vipi inakua hali ya wazee wake hususan Mama mtu?.
Mama Mwenyewe anaweza kueleza Uchungu wa kuzaa kwa ukamilifu, lakini akashindwa kuyazungumzia Machungu ya kuondokewa na Mtoto wake, Mambo hayasemeki ni mazito sana, Sasa kwanini inakua hali kama hiyo na Uchungu usoelezeka, leo tunafanya uchambuzi wa hali hiyo ili mtu ikimkuta atambue anaikabili vipi. Inatakiwa ukumbuke Binaadamu sote hatuko sawa na kila mmoja wetu ataukabili mtihani huo kwa jinsi ya uweza wake.
Sasa kwanini ikawa Mama ndiye Mwenye Uchungu zaidi, Napenda kukujulisha katika Ulimwengu huu kila kitu kina Ndani(Inner)Na Nje(Outer).Na Mapenzi pia yana hali kama hiyo, si unaona vipi anavopenda Baba anaonesha kwa kununua hichi na kile,Baba ni mwenye kuonesha Mapenzi yake kwa wanawe kwa njia ya nje, Na Mama yeye Penzi lake liko Moyoni, Imekua hivyo sababu mwanzo wake huyo Mtoto kaumbwa ndani ya Tumbo la mama yake na kwa ajili hiyo zimepatikana (Connections) za kimaumbile baina ya Mama na mtoto. Anakua Mama huyo ni msimamizi wa kila kitu kinachomuhusu huyo mtoto, anaumbwa mtoto huyo katika tumbo la mama yake katika viza vitatu, ndani ya viza hivyo tunakuja kumuona kwa kushuhudia kitu cha mwanzo nacho hicho kinyama cha moyo kinachopiga kwa kutiwa Nuru na kuanza kuwaka na huku kinadunda, hapo tena inakua mioyo miwili inapiga kwenye mwili mmoja wa Mama alobeba mimba hiyo na hapo ndio inapoanza hiyo (Communion)ya Milele baina ya Mama na Mtoto.
Na Mfano wa (Communion) ni kama vile wa (Lover na Beloved) endelea part 2

UCHUNGU WA MAMA PART 2
Asalaam Aleiykum,
Na (Communion) Utaigundua pale labda Mtoto wako kapotea, au Mgonjwa wako kaingia chumba cha Operesheni na hujui kama atatoka yuhai, au Au mfano mwengine una Mume au Mke anakuacha bado unampenda, na yeye sasa hataki tena hiyo Ndoa, Machungu unayoyapata hapo basi kwa Mama alofiwa na Mwanae ni mara 99.
Nini Kinatokea, tukio linalotokea hapo ni kama umo ndani ya chumba unaanza kusoma Barua ya mafanikio au ya kupanda cheo, au umetumiwa cheki ya mapesa na ghafla taa ikazimwa, na huyo mama maskini na yeye Taa yake ya Moyoni imezimika, kabaki anapapasa hajui kwanini, Anaweza Mtu kwa wakati huo akapeleka lawama zake kwa Mungu, Na kuuliza kwanini Mimi? Jee hii ndio Haki, Nahisi mimi nimeonewa, Mollah wako anamjibu nini huyo Mja kupitia katika Kitabu chake cha Ukweli usio na shaka, Quraan 156 Baqarah. ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَـٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٌ۬ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٲجِعُونَ
"Na wale ambao uwapatapo msiba husema, Hakika sisi(tumetokea)kwa Mwenye Enzi Mungu, Na kwake yeye Tutarejea".
Hapo inafutwa Dhana ya uchungu wako wa kuona eti Mungu kakuonea, hakufanya huruma yoyote akamuacha mtoto wako, Ndio anakujulisha kuwa nyote viumbe vyake, na kuja na kuondoka kwako anapanga yeye kwa sababu zake anazozijua, pengine huyo mtoto atakua kiombezi chako hiyo siku ya siku, Pengine anafanya hivyo kwa kuyataka Mapenzi yako yageukie kwake yeye na ujisogeze karibu, pengine umechaguliwa wewe mtihani huu ili Mollah wako akupeleke katika pepo yake kwa ajili ya kuridhia kwako tu, na hakuna jengine.
Leo itakuaje kitoto kilichopita ndani ya Matumbo yangu kimeondoka bila ya kuniaga Mollah wangu mimi nimekukosa nini? kwa tukio hili, bora ingekua mimi, bora ungenichukua mimi nikatangulia, hayo ni mayoe ya Mama aloondokewa na Mwanawe, Na huo ni Uchungu anohisi wakati ule, Huzuni imemshika hajui akimbilie wapi, hajafanya makosa mama huyo kwani hata pale Firauni alipoamuru watoto wote wa kiume wauliwe Mama yake Nabii Musa a.s aliambiwa nini? Kitie kitoto kwenye (Kisusu)halafu ukiwache kwenye Mto, (Atalelewa huyo na Adui wangu Firauni)Halafu kikafatia nini? Tizama Mollah anavoipoza Roho ya Mzazi (Quraan-Taha aya ya 40)
فَرَجَعۡنَـٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَىۡ تَقَرَّ عَيۡنُہَا وَلَا تَحۡزَنَۚ
"Tukakurejesha kwa Mama yako ili macho yake yaburudike (Na)Wala asihuzunike"
Huzunika Mollah wako anajua nini kinatokea katika Moyo wako kwa mapenzi ya Mwanao, Na anajua kuwa huyo alowako harejei tena na wewe macho yako hayatoburudika kwa wakati huu, kwa hiyo omboleza, Ikiwa Mama wa Mtume wa Mwenye Enzi Mungu kapewa na (Wahyi)alikua katika hali hiyo, nini hali ya Mama wa kawaida. Endelea Part 3

UCHUNGU WA MAMA PART 3
Asalaam Aleiykum,
Nini Hali ya Mzazi wa kawaida aliyeondokewa na Mwanawe, ili Na wewe usije ukahuzunika sana, na usije ukadhurika na sumu za machozi, na maumivu ya mapenzi kwa Mwanao, Ndio Mollah anakumbusha kuwa kila Nafsi itakufa(Kuonja Mauti)Na kila nafsi imewekewa muda wake wa kupita katika Ulimwengu huu, na wakati wake mahususi na sababu zake. Na vile vile unakumbushwa Mzazi ukiondokewa na mtoto mdogo basi ujue ule Uchungu na shida unazozipata Mwenye Enzi Mungu anakuzindua uelewe yeye ndiye aliyetoa na sasa amechukua, unachotakiwa wewe uridhie msiba huo, pia ujue huna la kufanya katika amri ya Mwenye Enzi Mungu, Na kama utaridhika kweli ukawa hukufuru, Nini kinatokea?Mollah wako anakuteremshia Shufaa itokayo kwake(Na hakuna uponesho ulo bora isipokua ule ulotoka kwa Mollah wako).
Na kuna Shufaa za kila aina huenda Mollah wako akakupa zawadi nyengine ya kiumbe chake, au akakufanya hayo mapenzi ya mwanao kuyageuzia kwake Mollah wako, na kaa ukijua huyo mtoto yaweza kuwa akawa wa kukuombea siku hiyo ya siku (Siku ya Hukumu)Na wakati huu "Ewe" Mama ulofikwa na msiba, usiyafuge machungu, wala usiwe shujaa kwa kujizuia na huzuni yako, pata dawa yako kwa kuyaondoa machungu hayo, ikiwa unahisi kulia, basi lia, kama unahisi kucheka, cheka, ukihisi kuhamaki, hamaki, chochote kinachokuja moyoni mwako kitoe wala usihisi haya au kujizuia, ukiona unataka kuzungumza, zungumza, ukiona unataka kukaa kimya, kaa kimya, ukiona unataka kumkumbuka Mtoto wako mkumbuke, usizuie kitu, ila kumbuka kitu kimoja tu hizo fikira ndizo zenye kukuumiza basi nakushauri kitu kimoja zikija fikira zikumbuke hizoo zinakuja, na ukiweza kuzikumbuka zinapokuja hiyo ndio dawa yako ya kuondokewa na huzuni, na hapo utakua ushaushinda moyo na sasa hutopata maumivu tena, na kidogo kidogo machungu yataanza kutoweka.
"Ewe Mollah wetu tupe subira sisi na wazee waloondokewa na watoto wao""Ewe Mollah wetu tuteremshie huruma zako tupate kukubali amri yako" "Ewe Mollah wetu tupe kheri zako sisi na watoto wetu walo hai na walotangulia kuja kwako, Na utukutanishe tena katika Pepo yako ya Firdaus kwa salama na Amani Mollah wetu" "Ewe Mollah wetu wape shufaa Ndugu zetu na Waislam kwa Jumla walofikwa na Misiba itokayo kwako. Amin.

Sunday, January 5, 2014
KIPIMO CHA DINI PART 1
Asalaam Aleiykum
Ingia kwenye Darsa hii kwa Utulivu ili upate kufahamu yanokusudiwa, Nakuchukua katika chumba cha Upimaji ili uweze kujua na kuchambua Maswali kadhaa kuhusiana na Imani yako na kile Unachokifata, Kipimo hichi kitakusaidia pengine kupata ufafanuzi wa Mambo na ukaweza kuyarekebisha Masuala ya Dini yako na Imani kwa Jumla.
Nini Uislam? Swali hili unalikwepa sana kujiuliza na kulisikiliza sababu litakuumbua, hutaki lizungumzwe, unataka lisemwe, litamkwe kwenye Ulimi tu, lakini Mtu akitaka kwenda (Deep)unaona mambo hayoo yanaanza. Jawabu lake ni Ku(Surrender)Kujisalimisha, Nini (Surrender)? (Ni kujisalimisha kwa Ukamilifu, hupigani tena, unamuachia yule ulokua unapigana nae aamue kila kitu, kama kukufunga au kukunyonga. mikono juu sasa huna la kufanya tena)hiyo ni (Surrender)kwa Binaadamu mwenzio, Lakini kwa Mollah wako kujisalimisha unatakiwa uwe mkamilifu kwa Matendo yako yote,(Nothing less). Na ukiweza kufanya hivyo basi unakua wewe Muislam.
Sasa vipi kunakua kujisalimisha huku? Kujisalimisha huku ni kugumu sana kwani unatakiwa kufilisika kwa kila kitu, Na wakati huo huo kutajirika na kila kitu, Utaona mbona kauli zinatafautiana, mbona anajikanyaga mwenyewe, vipi ufilisike na hapo hapo utajirike, yanakuwaje mambo haya, Mbona sifahamu, ndio mambo ya Vipimo yanavokua unakua hufahamu mpaka upewe (Result)au uzijue mwenyewe, kazi yangu mimi ni kukusogezea (Kipimo)na kukuonesha vipi utajipima halafu majawabu utapata mwenyewe.
Kitu cha kwanza napenda kukujulisha kuwa Muislam ni jambo rahisi sana, kazi ipo kwenye kuingia na kuishi Kiislam, hilo ni jambo zito na si wengi wenye kulitekeleza. Kama nilivoeleza Kuishi Kiislam ni Ku(Lose of Many things) halafu wakati huo huo ni Ku(Gains Everythings)huko ni kuishi, ama kuwa Muislam inaweza kua umezaliwa au umesilimishwa au umewakuta wazazi wako wanasema(Kumbuka wanasema hawatendi)sisi Waislam na wewe umelelewa hivyo unafata unaingia kundini mpaka kufa kwako na wewe unasema mimi Muislam, Lakini kamwe mwiko kwako kuishi Kiislam, Uislam wako unaendelea kubaki kwenye Ulimi, ndio unautaja kwa mbwembwe lakini maskini huujui.
Sasa unapata nafasi ya kuujua na una shauku vipi uta (Surrender)ili uwe Muislam kamili.Quraan Al Baqarah aya ya 2-3
ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدً۬ى لِّلۡمُتَّقِينَ
"Hichi ni kitabu kisichokua na shaka ndani yake,ni uongozi kwa Wamchao Mungu"
Nini kitabu, kitabu ni maneno yaloandikwa, usije kubaki kwenye maneno utakosa maana yake, utashindwa ku (Surrender)ingia ndani ya maneno utizame ujumbe uliomo ndani ya hayo maneno,(na ndio wengi tumepata hasara ya kubaki ndani ya maneno)ndio maana Uislam wetu unaishia kwenye Ulimi, ukiingia ndani ya ujumbe hukutani na mashaka kabisa, unaogelea kwa Raha ya kujua kuwa huu ni uongozi ulotoka kwa Mollah wangu mlezi,lakini kujua huku si kwa wote isipokua kwa wale wenye mapenzi na Mwenye enzi Mungu ambao wanamcha na kutekeleza maamrisho yake.
Endelea part2 upate kujua vipi uta (Surrender)

KIPIMO CHA DINI PART 2
Asalaam Aleiykum
ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَـٰهُمۡ يُنفِقُونَ
"Ambao huyaamini yasionekana, na kusimamisha Sala na hutoa katika yale tuliyowapa"
Hapa ndipo penye hiyo (Surrender)"Wale ambao wana amini"yasio onekana, Rahisi kuamini chenye kuonekana, mkipigana vita ukishindwa unaona silaha ile na wewe ushashindwa una nyanyua mikono, vipi leo utanyanyua mikono silaha hujaiona, ndio nikasema vigumu kwako ku (Surrender) kwa jambo usiloliona, unakubali shingo upande, mashaka yamekushika, (surrender)yako si ya ukamilifu kabisa, Sasa kama kweli Ume (Surrender)umekua unaishi ndani ya Uislam jipime halafu jawabu kaa nalo mwenyewe, Anasema yule alokuumba, (Wewe si Umeamini)Basi kama umemuamini, anakuamrisha Usiseme Uongo, Usizini,Usisikilize mambo ya kipuuzi, usitukane, usipokee Rushwa,usidhulumu,usile haramu,usihusudu,usichukie,usishuhudie ushaidi wa uongo,usisengeye,usikere viumbe wenzio,usile Riba,usifanye Biashara ya haramu,usigombane na ndugu zako.
Waangalie wazazi wako,ndugu zako mayatima,maskini,waloharibikiwa njiani, ikisha ondosha Kiburi jione wewe Mtu wa kawaida, ondosha mimi Shk Fulani,ondosha mimi kabila fulani, ondosha mimi mkubwa Fulani yatupe majoho yakujipa, ondosha cheo chako kumbuka(Cheo kipo)lakini hakikuvai ndani ya Moyo ukawa unajivuna na cheo hicho, ondosha majivuno, na kila wakati jione mimi (Nothing)na najikabidhi kwa yule asoonekana kwa mapenzi na utiifu,mimi naamini yupo na yeye ndiye mlezi wangu, na kwake na (Surrender)yeye ndie awe muamuzi wa kila kitu changu, na mimi naishi kama alivyoamrisha yeye kwa kadir ya uwezo wangu.
Ukifikia Daraja hiyo wewe usha (Surrender)ushakua Muislam kamili na ukiwa Muislam kamili tu, sasa Sala haitokei mdomoni tena, bali inatokea moyoni na unakuwa katika wale wenye kusimamisha Sala, Sala yako inakua sio ya kawaida, siyo ya kwenye Ulimi, inatoka kwa mapenzi ya kweli kweli kwa ajili ya Mollah wako usiyemuona lakini umeridhika na uhakika ulokua nao, na muongozo wa Nuru alokupa katika Moyo wako, unakua sio tena (Wanoamini yasionekana, bali unakua unaamini yenye kuonekana) Na ukifikia Daraja hiyo tena hapo kila ulichopewa unakitoa, hutaki kukaa nacho, kwani ushaona visivyooneka na unajua kuwa nikitoa ntaongezewa, vipi utaongezewa? endelea part 3

KIPIMO CHA DINI PART 3
Asalaam Aleiykum
Vipi utaongezewa? Utaongezwa ukionekana unafata Dini ya Mwenye enzi Mungu kama inavosema aya ya 208 sura ya Baqarah
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِى ٱلسِّلۡمِ ڪَآفَّةً۬ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٲتِ ٱلشَّيۡطَـٰنِۚ إِنَّهُ ۥ لَڪُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬
"Enyi Mloamini Ingieni katika hukumu(Dini)za Uislam zote(Kikamilifu)Wala msifate nyayo za Shetani, Hakika yeye kwenu ni Adui (Aliye)dhahir"
Nzuri umeamini, hiyo ni hatua ya mwanzo, sasa piga hatua ya pili kwa ukamilifu, mwache mkono Shetani ili uingie ndani, kumbuka kakufunga pingu zikate umkimbie, kumbuka anakuzuia usiipate (Dini)wala hiyo (Surrender) Mambo yako wazi, unajijua mwenyewe shetani alivokutawala inawezakuwa kwenye Biashara, au kwenye siasa, au katika mambo mengine ambayo yanakuzuia usiishi Kiislam. Unajiuliza kwanini nifilisike halafu nitajirike, unaogopa vipi nitapewa nikishafilisika kumbuka hiyo ndio kazi ya Shetani.
Leo wewe umesahau umekuja katika Ulimwengu huu bila hata nguo, Unasahau unavoendelea kupewa hivyo ulivo navyo na zaidi, unapewa muda wa kuishi, unapewa Afya nzuri, unapewa furaha ya ko moyoni, unapewa familia uishi nayo, unapewa vicheko na faraja, basi kwa mtoaji huyo wewe mfano wako unakua kwenye Bank tu, na Nyumba kubwa, na gari la fahari, na vyote hivyo kaa ujiulize, nani alokupa maarifa hayo ukavipata, ni yule yule (Unaye Muamini)bila ya kumuona, Yeye ndiye Mwenye kukuletea hayo maarifa, ikisha akakuonesha njia, akakupa sababu na nyenzo za kupata hayo uliyoyapata, kumbuka anaweza kukunyanganya wakati wowote ima iwe kwa kukupa maradhi au kukuondosha Ulimwenguni, uwezo wake Yeye, na Yeye ndie Mlezi wa viumbe vyote.(Baqarah 267)
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا ڪَسَبۡتُمۡ وَمِمَّآ أَخۡرَجۡنَا لَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِۖ وَلَا تَيَمَّمُواْ ٱلۡخَبِيثَ مِنۡهُ تُنفِقُونَ وَلَسۡتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغۡمِضُواْ فِيهِۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ
"Enyi Mloamini Toeni katika Vile Vizuri mlivyovichuma, Na katika Vile tulivyo kutoleeni katika Ardhi, Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea isipokua kwa kuto viangalia, Basi Jueni Mwenye Enzi Mungu ni Mkwasi asifiwaye(Kwa Shukurani)"
Kwanini Utoe, sababu kutoa ni sehemu katika mambo ya (Surrender) Kutoa ni sifa katika Uislam, Bila ya kutoa wewe hujawa Muislam, na Sababu Kubwa ya kuwa sifa ndani ya Dini hii ni kuwa huyo alokuumba Mollah wako, Yeye Daima yumo katika kutoa, Na sio kama wewe unatoa usivovitaka, Yeye ni mwenye kutoa mazuri usiku na mchana, sio kama wewe hutoi mpaka liwepo kundi la watu linakutizama, hutoi mpaka nyuma yake iwepo sababu ima utalipwa au utapongezwa, huko si kutoa hiyo ni biashara, kutoa kwa (Muislam)kwa ku (surrender)unatoa kwa siri, unafata Maskini hawakujui, huwajui unawapa vile vizuri hasa, ambavyo kama watakuona watu wako wanakukamata mkono,wanaona labda unaumwa au umekosea hujui unalolifanya, huko ndio ku(Surrender)huo ndio Uislam. (Surrender)kwa kile kisicho onekana, anza mazoezi ya kuacha vyeo vyako, ukikaa peke yako hebu japo mara chache kumbuka kama ulivokua mdogo, huna majukumu yoyote ulikua vipi, Baharini unachupa bila ya kujali, mbio unakwenda bila hata ya kutizama gari, popote unaingia hujali hata hatari yake, unashika mpaka moto huogopi, rejea kama vile lakini sasa kwa njia nyengine, ipi ukikaa ondoa vyeo vyako, mimi nani, mimi Baba, mimi mume, mimi mwalimu,mimi kiongozi, mimi hivi mimi vile, Jijue mimi nimekuja katika Ulimwengu huu bila ya hata Jina, sikuja wala na nguo, sina wala address,sina Rafiki, jiulize wapi nilipotokea, kuwa na hamu huko ulipotokea ufunguliwe siri zake upajue ili upate kupakamata kwa ku(Surrender)Na ukisha yajua hayo wewe ushabadilika, huwi Muislam Jina tena, unakua Muislam wa Matendo, mpaka sala yako inakua ya aina nyengine, hapo unagundua mimi ni (Kinyama)niliyeumbwa nikapewa Utukufu wa kujitambua, uwezo wa kugundua yupo aliyeniumba na kwake yeye na (Surrender)Nasilimu, nabadilika nakua Mtu mwengine kabisa, Mimi namuamini Mollah wangu asiye onekana kwa Dhati ya uwepo wake, na nazifata Sheria zake zote kwa ukamilifu, na Iwapo nitateleza basi Mollah wangu atanisamehe kwa hilo.Kuanzia leo nakua Muislam kamili na sitaki tena kipimo.

Subscribe to:
Posts (Atom)