Asalaam Aleiykum,
Yanafanyika mahojiano hayo chini ya ardhi au juu ya ardhi, inategemea wewe wa Dini gani, hapo havuki mtu, usione labda utakimbia kwa kuchomwa moto au kucheleweshwa kuzikwa, ni lazima mahojiano hayo yafanyike kwa muda usiozidi siku tatu, ndio maana mkaambiwa msiba siku tatu, Nabii Isa a.s anasema kwenye Injili(Biblia)Ntakaa kwenye tumbo la Ardhi siku tatu, (Mfano wangu kama Mfano wa Yunus, kukaa ndani ya tumbo la samaki chewa siku tatu)Na wewe Ardhini lazima ukae siku tatu kabla ya kuanza safari yako, ukimaliza kufukiwa tu wanatokezea watu usowahi kuwaona, viumbe wa aina nyengine, Nuru zao zinakuunguza, wanafanya nini? wanakupiga Begani fungua sanda tushafika sisi tuna mazungumzo na wewe, na hao wenzio wenye kuishi huko juu ya Ardhi wametufanyia hisani kubwa ya kukutia manukato ili huu mwili kabla ya kutoa harufu tuelewane uzuri kwa haya tutakayo kuuliza, Sasa ikiwa hapa Duniani unaulizwa (Confirmed Date of Birth)Chini ya Ardhi kuna Maswala matatu muhimu ya mwanzo, (Hapa ndio Bwana Mtume s.a.w )alikua akisha kumzika mtu anawaambia Masahaba muombeeni ndugu yenu hivi sasa anaulizwa.
Anaulizwa nini? Siku hii sote itatukabili na siku nzito ambayo ishasemwa na huko Mbinguni yapo yalee tuliyokua tunakupeni ahadi nayo, kuwa mtayakuta. Swali la Kwanza nani uliyekua Unamuabudu?, Ndugu zangu ikiwa umekufa hujarudi kwa Mollah wako, basi hapo Roho inakaa kimya inajibu (Mind) Akili yako Muimbaji fulani, Kinacho kufika hapo mimi sikisemi ila fikiria mwenyewe ile mbao na dongo ulofunikwa nalo futi 6 hali inakuwaje huko chini.
Swali la pili nani huyu uliyekua unamfata aliyekuletea ujumbe, tena hapo kama ulikua hutoki kwenye Computer unajibu (Face book), Na swali la tatu ulikua ukifata dini gani, unajibu kwa haraka haraka (Wassup) hapo watu hawaendelei tena na maswali hakuna faida wanajua umejaa mambo ya mjini, kila utakachoulizwa utatoa Story za mjini, kiza kinachokua hapo hata ukitaka kukumbuka labda imekujia duh nishafuja unataka kusema Allah, wapi ulimi ushatiwa Nanga nzito, ee una vidonda vya mdomo huwezi kula na tafran tele vipi leo ufungwe Nanga ya Meli nzima kwenye Ulimi huo hali inakuaje?. Hali inatisha katika Giza la kaburi ndugu zangu, ndio maana tukiomba tunasema mtilie kaburi lake Nuru. Hiyo ni (Interview) ya ile Roho ilosahau ikagubikwa na maasi, fitina, choyo na unyanganyi katika Ulimwengu huu.
Ama Yule Mwenye kukumbuka akawa anafanya yalo mema na kila saa kumtaja Mollah wake yeye kashushiwa Aya anaondoshwa wasiwasi, anaambiwa asiogope kaburi wala hiyo (Interview)Mahojiano, ikiwa wewe ulikuwa Muumin wa kweli basi soma aya ya 27 Surat Ibrahiim ili ikupoze na kadhia ya siku hiyo,
"يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِى ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِى ٱلۡأَخِرَةِۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّـٰلِمِينَۚ وَيَفۡعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ"
"Mwenye Enzi Mungu huwathibitishia waloamini kwa kauli thabit, Katika Maisha ya Dunia na katika Akhera, Na Mwenye Enzi Mungu huwaacha kupotea hao Wenye kudhulumu, Na Mwenye Enzi Mungu hufanya apendavyo"
Hiyo ndio kawaida ya Ahadi ikiwa umeishi vyema kwenye Ulimwengu huu basi wewe utakua mwepesi na huko chini ya Ardhi kuijibu hiyo (Interview), Utatoa Jawabu Mollah wangu ni Mlezi aliyeniumba kutokana na Udongo huu nilolalia, akaufanyia ujuzi wa hali ya juu katika maumbile mpaka sasa nikawa nakujibuni kutumia huu Ulimi aloniumba nao Mollah wangu. Na huyo niliyekua namfata ni mjumbe wake aliyemtuma kwetu sisi waja wake, namie nikayaamini aliyotuletea, Na nikaifata hii Dini ya Kiislam kwa ukamilifu kama ilivotakiwa, Na sasa najisalimisha kwake Muweza wa kila jambo, Na Naridhia kila alonipangia Mollah wangu ambaye anafanya mambo yake kwa haki na anavotaka yeye, Napia nataraji atanisamehe kwa yote nilomkosea kwa kuwa mimi sikua mkamilifu kama alivonitaraji, Na hili ni jawabu la Roho yangu na yako siku hiyo itakapowadia.
Namuomba Mollah mwenye kuyajua ya Siri na ya Dhahiri, niloyafanya na ninayokusudia kuyafanya, anipe ridhaa ya kusamehewa na kuishi katika Enzi yake ya Utukufu wa Ulimwengu huu bila ya kumkera yeye ama viumbe wenzangu, aisafishe Roho yangu niwe Nampenda kila Mtu na kila Mtu awe ananipenda mimi kwa kadiri ya Uweza wa Roho hiyo. Amin.
No comments:
Post a Comment