"وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ"
Na katika Mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa(Promise)
Sikiliza "Ewe"Muulizaji ahadi zote zipo na kuwa na uhakika zitatekelezwa kwa Amri ya Mollah wako, Na katika Mbingu kuna Riziki zenu, Makusudio yake uwe unajua kila unacho chuma hapa Ulimwenguni, ikiwa wewe Mkulima au Mfanya Biashara, au uwe Mtu wa kawaida, Basi Elewa kila ukiamka Riziki yako ishapangwa Mbinguni kiwango chake Maalumu, Na hata ukifanya nini huwezi kuzidisha wala kupunguza, ila uamue Mwenyewe, Na unaruhusiwa kuamua , Unaruhusiwa kufanya vita na Mwenye Enzi Mungu, kwa Kuwanyanganya wenzio Riziki zao kwa Nguvu, Unaruhusiwa kufanya (Booking)yako ya mateso ya Moto kwa mkono wako mwenyewe, kuchukua mali za watu, kudhulumu majumba ya watu, kudhulumu maskini, kuwatia katika dhiki walochini kwa kujilimbikizia mali, kwa hilo unapewa ruhusa ili ukaribishe matatizo yatakayo kukuta Milele na hilo halina Shaka.
Kwa hiyo huku kuhangaika kwenu ni Bure kabisa mtowaji yupo na kajitaja kwenye sura ya (Banii-Israel-aya ya 30)
إِنَّ رَبَّكَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ إِنَّهُ ۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرً۬ا
Hakika Mollah wako Mlezi humkunjulia Riziki amtakaye, na humpimia amtakaye, Na yeye kwa Waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona.
Na kawaida Yake Mfalme wa hiyo Riziki yako kuwa ukizidisha kwa kutoa Sadaka, Na yeye anakuongezea kwa njia unazo zifahamu na usizozifahamu. Na kila kitu kinapangwa huko Mbinguni, upande wako wewe unatakiwa upige hatua ya kukielekea hicho kitu, na hapo utaona milango inafunguka bila ya wewe kutarajia, ikiwa umepangiwa uende University utakwenda, ukiwa umepangiwa uwe Tajiri utakuwa, Ikiwa umepangiwa uwe Rais utakuwa, ukipangiwa uwe chochote unakuwa na wala hili usilitilie shaka, ukitakiwa uwe Mwalimu utasomesha tu, kila pato lako limepangwa na yeye Mwenye kuwajua viumbe vyake, Na ndio athari yake utaiona tukiomba Dua unaelekeza mikono Mbinguni (Juu) kwa ishara ya kuomba, Unajua kwanini? Kwa sababu Roho inajua ilipotokea na inaelewa wapi hizo Riziki zinapopangwa.
Nyanyua macho upatazame uzuri Mbinguni kuna mambo ambayo huyaoni, halafu wacha zikujie fikra kuwa kuna siku na wewe utafanya safari ya kwenda huko mbinguni muda wako wa kuishi ukimalizika, lakini kabla ya kusafiri kuna (Interview)mahojiano lazima yafanyike hapa hapa Ulimwenguni, Na yanafanyika mahojiano haya wapi?
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment