Asalaam Aleiykum,
Nani huyu Mwenye kuuliza kama atakwenda Peponi au Motoni, Nani Muulizaji wa Swali hili, yaweza kuwa mimi au wewe, sote tuna shaka, sote tunakiu yakutaka kujua, kwanini tukauliza? lazima (Deep) katika hiyo (Being) yetu kuna (Jawabu)linaelea lakini hatujui tulijibu vipi, Muulizaji kajaa mashaka, wasiwasi unamjia kila mara, woga unamgubika kila akisikia mwenzie (Kafariki) anaendelea kuuliza Muulizaji, Huyu fulani kenda wapi, na sasa hamu inamjia anataka kujijua yeye nani na atakwenda wapi wakati wake ukimalizika hapa Ulimwenguni, swali hili linawasumbua wengi na kuwatia mashaka makubwa katika Imani.
Nani Muulizaji? Huyu Mwenye kuuliza Daima yeye anauliza Nje na hata siku moja hajapata kujiuliza Ndani kwake, Na wakati kaambiwa wewe Mwenye mashaka, wewe mwenye Imani hafifu, Adh-Dhariyat 21"وَفِىٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ"
"Na katika Nafsi zenu Je Hamuoni"
Ushawahi kujiuliza mbona kuna mambo Mtu wa nje yoyote hayajui, si Mkeo wala wanao, si wazazi wako au ndugu zako, Bali ni wewe Mwenyewe unaeuliza ndie unayeijua siri hiyo, sasa Nani Muulizaji huyo? Nani Mwenye kujua sasa hivi Kichwa kinaniuma, Nani Mwenye kujua njaa imenishika, Nani Mwenye kujua sasa hivi Sikio linaniwasha, Nani Mwenye Kujua jana niliota Nini, Nani Mwenye kujua sasa hivi nishashiba nisiendelee kula, hayo mambo yote na mengine chungu nzima ni lazima uyaseme Mwenyewe ndio watu wa Nje wayajue, (Narejea tena wayajue)hakuna yoyote awezaye kuyahisi, (Unaweza kuwa uongo au kweli)shahid wa hilo ni wewe Mwenyewe, kwani kuhisi ni wewe peke yako huna mshirika katika hilo.
Napenda Uelewe hapo unapohisi ndio Jirani yako wa (Ufalme wa Nafsi yako)Ndio karibu yakaapo Mamlaka ya hiyo Roho yako, Sasa ikiwa ushagundua hilo kuwa mimi na hili Jumba langu ninalo ishi ni tafauti, kwanini ikawa Tafauti, kwa sababu kuna (Gap)baina ya kuhisi na kugundua wewe fanya uchunguzi utafahamu hilo(Leo si sehemu yake ya kulifahamisha hilo, ndio maana ukaambiwa katika nafsi zenu hamuoni, hapo ishapatikana Separation)hapo utajua ikiwa ipo hiyo tafauti baina yako na jumba lako la udongo, basi hicho chenye kutafautisha ndio mimi Muulizaji, Na utapata uyakinifu kitu hichi kinachoitwa mimi lazima kina pahala kilipotokea, na ukisha kulijua hilo basi moja kwa moja unaelewa lazima kuna siku na muda maalumu ya kurejea huko kilipotokea, Na baada ya kupata hakika hiyo, Lazima utafute (Source) ya mapenzi ya kurejea utokako, na ujitaarishe kuchukua zawadi gani, na hapo tena unakubali yupo aloniumba mpaka akanifikisha katika Ulimwengu huu, lazima iko safari mimi nilifanya mpaka nikafika hapa, na lazima nitarejea tena huko nitokako, ni bure kujenga kwangu majumba, ni bure kujilimbikizia mali, ni bure kufanya fisadi na chuk,i vyote hivi nitaviacha na nitarudi peke yangu kama nilivyokuja mwanzo.
Nani Muulizaji? Muulizaji kumbe ni mie ambaye sasa nakubali, sio kuamini tena, bali sasa imekua kukubali, na kukubali ndio hiyo (Surrender-Islam)na uki (Surrender) tu unafungukiwa na ufahamu wa mambo vyengine kabisa, sasa unakwenda (Beyond)unahama kwenye (Knowledge)unatupa elimu yote unaishi kwenye (Understanding) na ukipata huko kufahamu ndio hekima, na hapo Muulizaji unageuka kuwa mwenye kujibu kama inavoendelea aya ya 22 ya sura hiyo hiyo ya Adh-Dhariyat.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment