Asalaam Aleiykum,
Unazijua Nyumba zilofikwa na Msiba huu wa Ndoa, Umeshawahi kuhudhuria makaburi hayo ukaona vipi wana Ndoa wanavyoteseka, Na kwanini nikaita msiba kwa sababu wanandoa hao wanaishi ndani ya kifo cha Mapenzi, Wamefikia mpaka kutoka katika Rehma za Mollah wao, Watu hao ni wale wenye kuishi katika Ndoa isiyokua na Mapenzi wala masikilizano, Na Ndoa kama hiyo Mwenye Enzi Mungu anaiondoshea Rehma zake kabisa, Na ikiondoshwa Rehma katika hiyo ndoa utaona kila mmoja anatafuta mvinyo wake wa kumlaza, utaona Wanaume watakua wanazama kutafuta na kuthamini Marafiki kuliko Mke, Au anakwenda nje kufuga (Kimada)au anatafuta (Uraibu) wa aina yake ili ajisahaulishe huku akidhani mambo yatakaa sawa yenyewe.
Na Mwanamke Ima atabaki na huzuni, pamoja na malalamiko, au atatafuta Mashoga apate kujisahaulisha na (Kadhia)yake ya kuharibika kwa ndoa yake, au na yeye atatafuta kipoza Moyo(barobaro)afanye urafiki nalo. Sasa Jiulize kwanini Ndoa yako imefikia Hali kama hiyo, Na kwanini unaichia iendelee na kufanya kama jambo la kawaida.
Katika Darsa ya leo nadondosha Siri iokote upate kuitumia, ifanyie kazi upate kurekebisha Ndoa yako, Usikubali tena kuishi ndani ya kaburi la Mapenzi, Nia yangu sio kukutenganisha au kuvunja Ndoa yako, Dhumuni langu ni kuuhisha au kuirejesha kama zamani ilivyokua, na wala usione labda nishazeeka Ndoa ya nini, laa Ndoa ni ngazi ya Mapenzi ya Mume na Mke, Na Mapenzi hayo yakikamilika mkaungana kikweli basi yana kupelekeni moja kwa moja kwa Mollah wenu, Mnageuka baada ya kupendana nyinyi mnampenda Mollah wenu na hilo ndio dhumuni la Ndoa.
Anasema Mwenye Enzi Mungu katika Quraan sura ya Rumi aya 21.
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ
"Na katika Alama zake,Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila shaka katika haya kuna ishara kwa watu wanofikiri"
Wewe mwenye kumtesa huyo mwenzio, Napenda uelewe hizo unazozitesa na kuzipiga vita na kumkimbia mwenzio basi unazipinga na kuzikanusha Alama za Mwenye Enzi Mungu"
"Ewe Mja ametajwa Mke ili kwa kuambiwa wewe Mwanamme kuwa huyo ni jinsi yako, Imekua jinsi hiyo ya Maumbile mpaka kufanana naye, hebu angalia kwa pembeni hivyo jee mimi na Mke wangu tunafanana, Jee sisi ni (Soul Mate) Hebu kuwa Mja wa Fikira kwanini namtesa Mwenzangu, Nilipomuoa mwenzangu huyu Mollah wangu alichukua ahadi ya kutujaalia Mapenzi na Huruma, viwili hivi leo vipo wapi, nani kaviondosha? Na kwanini vimeondoka, mbona mimi nakimbilia nje? Jee hii ni Ishara ya mwanzo wa Adhabu yangu.
Mollah alipopanga waishi Mke na Mume ilikua Dhumuni lake wapeane (Company) Awe Mbize Uwe Mboza, Awe Laila Uwe Majnu, awe Habiba uwe Habib, vipi leo unakwenda kufurahisha watu wa nje, nini kimekusibu Mja wewe, au haya yalokusibu kwa sababu ya kwenda kinyume na maneno ya Bwana Mtume s.a.w "aliposema" Yoyote yule atakae muoa Mwanamke kwa ajili ya kuyatunza macho yake, kuwa na tahadhari (Katika maisha yake) Na kuwatunza familia yake kwa Huruma, Basi Mwenye Enzi Mungu humtilia Baraka mwanamke huyo kwa mumewe, Na Mume kwa Mkewe, Tizama leo vipi unaifanyia familia yako, hivyo unafikiri Mlipaji hayupo? au unadhani hizo sio Dhanbi? Na kama ukigundua hayo makosa basi fanya haraka uyarekebishe ili ufanye (Tahfif)siku yako ya kutolewa Roho.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment