Sunday, January 12, 2014

UCHUNGU WA MAMA PART 1

Asalaam Aleiykum,

Nani awezaye kuujua Uchungu wa Mama pale anapo ondokewa na Mwanawe kwa ajili ya Fardhi ya (Kifo)Pengine anafariki Mtoto huyo kwa Ghafla, au unapata habari mwanao keshatangulia mbele ya haki, au unamshuhudia mwenyewe yanamkuta umauti. Yupo atakayeweza kuelezea japo kidogo hali anayokua Mama huyo wakati hukumu hii ya haki inapitishwa, Mwenye Enzi Mungu kashapitisha amri yake anahitaji kiumbe chake kirejee, na sisi hatujui siku gani kiumbe hicho kitahitajiwa, desturi yetu tunaridhia ikiwa mtu (kesha kula chumvi) au anaumwa hapo tunakiri, tunasema bora kapumzika, lakini nini habari yetu sisi ikiwa huyo alotangulia mbele ya haki ni mtoto mdogo, vipi tunaupokea msiba kama huu, hususan kitoto kishakuja Ulimwenguni na kimepata mahusiano na sasa kinaitwa mtoto wa fulani, vipi inakua hali ya wazee wake hususan Mama mtu?.
Mama Mwenyewe anaweza kueleza Uchungu wa kuzaa kwa ukamilifu, lakini akashindwa kuyazungumzia Machungu ya kuondokewa na Mtoto wake, Mambo hayasemeki ni mazito sana, Sasa kwanini inakua hali kama hiyo na Uchungu usoelezeka, leo tunafanya uchambuzi wa hali hiyo ili mtu ikimkuta atambue anaikabili vipi. Inatakiwa ukumbuke Binaadamu sote hatuko sawa na kila mmoja wetu ataukabili mtihani huo kwa jinsi ya uweza wake.
Sasa kwanini ikawa Mama ndiye Mwenye Uchungu zaidi, Napenda kukujulisha katika Ulimwengu huu kila kitu kina Ndani(Inner)Na Nje(Outer).Na Mapenzi pia yana hali kama hiyo, si unaona vipi anavopenda Baba anaonesha kwa kununua hichi na kile,Baba ni mwenye kuonesha Mapenzi yake kwa wanawe kwa njia ya nje, Na Mama yeye Penzi lake liko Moyoni, Imekua hivyo sababu mwanzo wake huyo Mtoto kaumbwa ndani ya Tumbo la mama yake na kwa ajili hiyo zimepatikana (Connections) za kimaumbile baina ya Mama na mtoto. Anakua Mama huyo ni msimamizi wa kila kitu kinachomuhusu huyo mtoto, anaumbwa mtoto huyo katika tumbo la mama yake katika viza vitatu, ndani ya viza hivyo tunakuja kumuona kwa kushuhudia kitu cha mwanzo nacho hicho kinyama cha moyo kinachopiga kwa kutiwa Nuru na kuanza kuwaka na huku kinadunda, hapo tena inakua mioyo miwili inapiga kwenye mwili mmoja wa Mama alobeba mimba hiyo na hapo ndio inapoanza hiyo (Communion)ya Milele baina ya Mama na Mtoto.
Na Mfano wa (Communion) ni kama vile wa (Lover na Beloved) endelea part 2

No comments:

Post a Comment