Sunday, January 5, 2014

KIPIMO CHA DINI PART 3

Asalaam Aleiykum

Vipi utaongezewa? Utaongezwa ukionekana unafata Dini ya Mwenye enzi Mungu kama inavosema aya ya 208 sura ya Baqarah
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِى ٱلسِّلۡمِ ڪَآفَّةً۬ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٲتِ ٱلشَّيۡطَـٰنِ‌ۚ إِنَّهُ ۥ لَڪُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬ 
"Enyi Mloamini Ingieni katika hukumu(Dini)za Uislam zote(Kikamilifu)Wala msifate nyayo za Shetani, Hakika yeye kwenu ni Adui (Aliye)dhahir"
Nzuri umeamini, hiyo ni hatua ya mwanzo, sasa piga hatua ya pili kwa ukamilifu, mwache mkono Shetani ili uingie ndani, kumbuka kakufunga pingu zikate umkimbie, kumbuka anakuzuia usiipate (Dini)wala hiyo (Surrender) Mambo yako wazi, unajijua mwenyewe shetani alivokutawala inawezakuwa kwenye Biashara, au kwenye siasa, au katika mambo mengine ambayo yanakuzuia usiishi Kiislam. Unajiuliza kwanini nifilisike halafu nitajirike, unaogopa vipi nitapewa nikishafilisika kumbuka hiyo ndio kazi ya Shetani.
Leo wewe umesahau umekuja katika Ulimwengu huu bila hata nguo, Unasahau unavoendelea kupewa hivyo ulivo navyo na zaidi, unapewa muda wa kuishi, unapewa Afya nzuri, unapewa furaha ya ko moyoni, unapewa familia uishi nayo, unapewa vicheko na faraja, basi kwa mtoaji huyo wewe mfano wako unakua kwenye Bank tu, na Nyumba kubwa, na gari la fahari, na vyote hivyo kaa ujiulize, nani alokupa maarifa hayo ukavipata, ni yule yule (Unaye Muamini)bila ya kumuona, Yeye ndiye Mwenye kukuletea hayo maarifa, ikisha akakuonesha njia, akakupa  sababu na nyenzo za kupata hayo uliyoyapata, kumbuka anaweza kukunyanganya wakati wowote ima iwe kwa kukupa maradhi au kukuondosha Ulimwenguni, uwezo wake Yeye, na Yeye ndie Mlezi wa viumbe vyote.(Baqarah 267)


يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا ڪَسَبۡتُمۡ وَمِمَّآ أَخۡرَجۡنَا لَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ‌ۖ وَلَا تَيَمَّمُواْ ٱلۡخَبِيثَ مِنۡهُ تُنفِقُونَ وَلَسۡتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغۡمِضُواْ فِيهِ‌ۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ 
"Enyi Mloamini Toeni katika Vile Vizuri mlivyovichuma, Na katika Vile tulivyo kutoleeni katika Ardhi, Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali  nyinyi wenyewe msinge vipokea isipokua kwa kuto viangalia, Basi Jueni Mwenye Enzi Mungu ni Mkwasi  asifiwaye(Kwa Shukurani)"
Kwanini Utoe, sababu kutoa ni sehemu katika mambo ya (Surrender) Kutoa ni sifa katika Uislam, Bila ya kutoa wewe hujawa Muislam, na Sababu Kubwa ya kuwa sifa ndani ya Dini hii ni kuwa huyo alokuumba Mollah wako, Yeye Daima yumo katika kutoa, Na sio kama wewe unatoa usivovitaka, Yeye ni mwenye kutoa mazuri usiku na mchana, sio kama wewe hutoi mpaka liwepo kundi la watu linakutizama, hutoi mpaka nyuma yake iwepo sababu ima utalipwa au utapongezwa, huko si kutoa hiyo ni biashara, kutoa kwa (Muislam)kwa ku (surrender)unatoa kwa siri, unafata Maskini hawakujui, huwajui unawapa vile vizuri hasa, ambavyo kama watakuona watu wako wanakukamata mkono,wanaona labda unaumwa au umekosea hujui unalolifanya, huko ndio ku(Surrender)huo ndio Uislam. (Surrender)kwa kile kisicho onekana, anza mazoezi ya kuacha vyeo vyako, ukikaa peke yako hebu japo mara chache kumbuka kama ulivokua mdogo, huna majukumu yoyote ulikua vipi, Baharini unachupa bila ya kujali, mbio unakwenda bila hata ya kutizama gari, popote unaingia hujali hata hatari yake, unashika mpaka moto huogopi, rejea kama vile lakini sasa kwa njia nyengine, ipi ukikaa ondoa vyeo vyako, mimi nani, mimi Baba, mimi mume, mimi mwalimu,mimi kiongozi, mimi hivi mimi vile, Jijue mimi nimekuja katika Ulimwengu huu bila ya hata Jina, sikuja wala na nguo, sina wala address,sina Rafiki, jiulize wapi nilipotokea, kuwa na hamu huko ulipotokea ufunguliwe siri zake upajue ili upate kupakamata kwa ku(Surrender)Na ukisha yajua hayo wewe ushabadilika, huwi Muislam Jina tena, unakua Muislam wa Matendo, mpaka sala yako inakua ya aina nyengine, hapo unagundua mimi ni (Kinyama)niliyeumbwa nikapewa Utukufu wa kujitambua, uwezo wa kugundua yupo aliyeniumba na kwake yeye na (Surrender)Nasilimu, nabadilika nakua Mtu mwengine kabisa, Mimi namuamini Mollah wangu asiye onekana kwa Dhati ya uwepo wake, na nazifata Sheria zake zote kwa ukamilifu, na Iwapo nitateleza basi Mollah wangu atanisamehe kwa hilo.Kuanzia leo nakua Muislam kamili na sitaki tena kipimo.

No comments:

Post a Comment