Sunday, January 12, 2014

UCHUNGU WA MAMA PART 2

Asalaam Aleiykum,

Na (Communion) Utaigundua pale labda Mtoto wako kapotea, au Mgonjwa wako kaingia chumba cha Operesheni na hujui kama atatoka yuhai, au Au mfano mwengine una Mume au Mke anakuacha bado unampenda, na yeye sasa hataki tena hiyo Ndoa, Machungu unayoyapata hapo basi kwa Mama alofiwa na Mwanae ni mara 99.
Nini Kinatokea, tukio linalotokea hapo ni kama umo ndani ya chumba unaanza kusoma Barua ya mafanikio au ya kupanda cheo, au umetumiwa cheki ya mapesa na ghafla taa ikazimwa, na huyo mama maskini na yeye Taa yake ya Moyoni imezimika, kabaki anapapasa hajui kwanini, Anaweza Mtu kwa wakati huo akapeleka lawama zake kwa Mungu, Na kuuliza kwanini Mimi? Jee hii ndio Haki, Nahisi mimi nimeonewa, Mollah wako anamjibu nini huyo Mja kupitia katika Kitabu chake cha Ukweli usio na shaka, Quraan 156 Baqarah. ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَـٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٌ۬ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٲجِعُونَ
"Na wale ambao uwapatapo msiba husema, Hakika sisi(tumetokea)kwa Mwenye Enzi Mungu, Na kwake yeye Tutarejea".
Hapo inafutwa Dhana ya uchungu wako wa kuona eti Mungu kakuonea, hakufanya huruma yoyote akamuacha mtoto wako, Ndio anakujulisha kuwa nyote viumbe vyake, na kuja na kuondoka kwako anapanga yeye kwa sababu zake anazozijua, pengine huyo mtoto atakua kiombezi chako hiyo siku ya siku, Pengine anafanya hivyo kwa kuyataka Mapenzi yako yageukie kwake yeye na ujisogeze karibu, pengine umechaguliwa wewe mtihani huu ili Mollah wako akupeleke katika pepo yake kwa ajili ya kuridhia kwako tu, na hakuna jengine.
Leo itakuaje kitoto kilichopita ndani ya Matumbo yangu kimeondoka bila ya kuniaga Mollah wangu mimi nimekukosa nini? kwa tukio hili, bora ingekua mimi, bora ungenichukua mimi nikatangulia, hayo ni mayoe ya Mama aloondokewa na Mwanawe, Na huo ni Uchungu anohisi wakati ule, Huzuni imemshika hajui akimbilie wapi, hajafanya makosa mama huyo kwani hata pale Firauni alipoamuru watoto wote wa kiume wauliwe Mama yake Nabii Musa a.s aliambiwa nini? Kitie kitoto kwenye (Kisusu)halafu ukiwache kwenye Mto, (Atalelewa huyo na Adui wangu Firauni)Halafu kikafatia nini? Tizama Mollah anavoipoza Roho ya Mzazi (Quraan-Taha aya ya 40)
فَرَجَعۡنَـٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَىۡ تَقَرَّ عَيۡنُہَا وَلَا تَحۡزَنَ‌ۚ
"Tukakurejesha kwa Mama yako ili macho yake yaburudike (Na)Wala asihuzunike"
Huzunika Mollah wako anajua nini kinatokea katika Moyo wako kwa mapenzi ya Mwanao, Na anajua kuwa huyo alowako harejei tena na wewe macho yako hayatoburudika kwa wakati huu, kwa hiyo omboleza, Ikiwa Mama wa Mtume wa Mwenye Enzi Mungu kapewa na (Wahyi)alikua katika hali hiyo, nini hali ya Mama wa kawaida. Endelea Part 3

No comments:

Post a Comment