Sunday, January 5, 2014

KIPIMO CHA DINI PART 1

Asalaam Aleiykum

Ingia kwenye Darsa hii kwa Utulivu ili upate kufahamu yanokusudiwa, Nakuchukua katika chumba cha Upimaji ili uweze kujua na kuchambua Maswali kadhaa kuhusiana na Imani yako na kile Unachokifata, Kipimo hichi kitakusaidia pengine kupata ufafanuzi wa Mambo na ukaweza kuyarekebisha Masuala ya Dini yako na Imani kwa Jumla.
Nini Uislam? Swali hili unalikwepa sana kujiuliza na kulisikiliza sababu litakuumbua, hutaki lizungumzwe, unataka lisemwe, litamkwe kwenye Ulimi tu, lakini Mtu akitaka kwenda (Deep)unaona mambo hayoo yanaanza. Jawabu lake ni Ku(Surrender)Kujisalimisha, Nini (Surrender)? (Ni kujisalimisha kwa Ukamilifu, hupigani tena, unamuachia yule ulokua unapigana nae aamue kila kitu, kama kukufunga au kukunyonga. mikono juu sasa huna la kufanya tena)hiyo ni (Surrender)kwa Binaadamu mwenzio, Lakini kwa Mollah wako kujisalimisha unatakiwa uwe mkamilifu kwa Matendo yako yote,(Nothing less). Na ukiweza kufanya hivyo basi unakua wewe Muislam.
Sasa vipi kunakua kujisalimisha huku? Kujisalimisha huku ni kugumu sana kwani unatakiwa kufilisika kwa kila kitu, Na wakati huo huo kutajirika na kila kitu, Utaona mbona kauli zinatafautiana, mbona anajikanyaga mwenyewe, vipi ufilisike na hapo hapo utajirike, yanakuwaje mambo haya, Mbona sifahamu, ndio mambo ya Vipimo yanavokua unakua hufahamu mpaka upewe (Result)au uzijue mwenyewe, kazi yangu mimi ni kukusogezea (Kipimo)na kukuonesha vipi utajipima halafu majawabu utapata mwenyewe.
Kitu cha kwanza napenda kukujulisha kuwa Muislam ni jambo rahisi sana, kazi ipo kwenye kuingia na kuishi Kiislam, hilo ni jambo zito na si wengi wenye kulitekeleza. Kama nilivoeleza Kuishi Kiislam ni Ku(Lose of Many things) halafu wakati huo huo ni Ku(Gains Everythings)huko ni kuishi, ama kuwa Muislam inaweza kua umezaliwa au umesilimishwa au umewakuta wazazi wako wanasema(Kumbuka wanasema hawatendi)sisi Waislam na wewe umelelewa hivyo unafata unaingia kundini mpaka kufa kwako na wewe unasema mimi Muislam, Lakini kamwe mwiko kwako kuishi Kiislam, Uislam wako unaendelea kubaki kwenye Ulimi, ndio unautaja kwa mbwembwe lakini maskini huujui.
Sasa unapata nafasi ya kuujua na una shauku vipi uta (Surrender)ili uwe Muislam kamili.Quraan Al Baqarah aya ya 2-3
ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَ‌ۛ فِيهِ‌ۛ هُدً۬ى لِّلۡمُتَّقِينَ
"Hichi ni kitabu kisichokua na shaka ndani yake,ni uongozi kwa Wamchao Mungu"
Nini kitabu, kitabu ni maneno yaloandikwa, usije kubaki kwenye maneno utakosa maana yake, utashindwa ku (Surrender)ingia ndani ya maneno utizame ujumbe uliomo ndani ya hayo maneno,(na ndio wengi tumepata hasara ya kubaki ndani ya maneno)ndio maana Uislam wetu unaishia kwenye Ulimi, ukiingia ndani ya ujumbe hukutani na mashaka kabisa, unaogelea kwa Raha ya kujua kuwa huu ni uongozi ulotoka kwa Mollah wangu mlezi,lakini kujua huku si kwa wote isipokua kwa wale wenye mapenzi na Mwenye enzi Mungu ambao wanamcha na kutekeleza maamrisho yake.
Endelea part2 upate kujua vipi uta (Surrender)

No comments:

Post a Comment