Sunday, January 5, 2014

KIPIMO CHA DINI PART 2

Asalaam Aleiykum

ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَـٰهُمۡ يُنفِقُونَ
"Ambao huyaamini yasionekana, na kusimamisha Sala na hutoa katika yale tuliyowapa"
Hapa ndipo penye hiyo (Surrender)"Wale ambao wana amini"yasio onekana, Rahisi kuamini chenye kuonekana, mkipigana vita ukishindwa unaona silaha ile na wewe ushashindwa una nyanyua mikono, vipi leo utanyanyua mikono silaha hujaiona, ndio nikasema vigumu kwako ku (Surrender) kwa jambo usiloliona, unakubali shingo upande, mashaka yamekushika, (surrender)yako si ya ukamilifu kabisa, Sasa kama kweli Ume (Surrender)umekua unaishi ndani ya Uislam jipime halafu jawabu kaa nalo mwenyewe, Anasema yule alokuumba, (Wewe si Umeamini)Basi kama umemuamini, anakuamrisha Usiseme Uongo, Usizini,Usisikilize mambo ya kipuuzi, usitukane, usipokee Rushwa,usidhulumu,usile haramu,usihusudu,usichukie,usishuhudie ushaidi wa uongo,usisengeye,usikere viumbe wenzio,usile Riba,usifanye Biashara ya haramu,usigombane na ndugu zako.
Waangalie wazazi wako,ndugu zako mayatima,maskini,waloharibikiwa njiani, ikisha ondosha Kiburi jione wewe Mtu wa kawaida, ondosha mimi Shk Fulani,ondosha mimi kabila fulani, ondosha mimi mkubwa Fulani yatupe majoho yakujipa, ondosha cheo chako kumbuka(Cheo kipo)lakini hakikuvai ndani ya Moyo ukawa unajivuna na cheo hicho, ondosha majivuno, na kila wakati jione mimi (Nothing)na najikabidhi kwa yule asoonekana kwa mapenzi na utiifu,mimi naamini yupo na yeye ndiye mlezi wangu, na kwake na (Surrender)yeye ndie awe muamuzi wa kila kitu changu, na mimi naishi kama alivyoamrisha yeye kwa kadir ya uwezo wangu.
Ukifikia Daraja hiyo wewe usha (Surrender)ushakua Muislam kamili na ukiwa Muislam kamili tu, sasa Sala haitokei mdomoni tena, bali inatokea moyoni na unakuwa katika wale wenye kusimamisha Sala, Sala yako inakua sio ya kawaida, siyo ya kwenye Ulimi, inatoka kwa mapenzi ya kweli kweli kwa ajili ya Mollah wako usiyemuona lakini umeridhika na uhakika ulokua nao, na muongozo wa Nuru alokupa katika Moyo wako, unakua sio tena (Wanoamini yasionekana, bali unakua unaamini yenye kuonekana) Na ukifikia Daraja hiyo tena hapo kila ulichopewa unakitoa, hutaki kukaa nacho, kwani ushaona visivyooneka na unajua kuwa nikitoa ntaongezewa, vipi utaongezewa? endelea part 3

No comments:

Post a Comment