Sunday, January 19, 2014

MSIBA WA NDOA PART 2

Asalaam Aleiykum,

Mwenye Enzi Mungu kasema kama utaona Mambo yameharibika, An-Nisai aya ya 128,
وَإِنِ ٱمۡرَأَةٌ خَافَتۡ مِنۢ بَعۡلِهَا نُشُوزًا أَوۡ إِعۡرَاضً۬ا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡہِمَآ أَن يُصۡلِحَا بَيۡنَہُمَا صُلۡحً۬ا‌ۚ وَٱلصُّلۡحُ خَيۡرٌ۬‌ۗ 
"Na kama Mke akiona Mume wake (Anamfanyia)magonvi au kutengana, basi si vibaya kwao wakitengeneza baina yao suluhu, Maana suluhu ni kitu bora(Chenye kheri)"
Napenda uelewe suluhu si ushindi na kama huyo mwenzio haitaki suluhu basi kuna mambo mawili lazima uyaangalie, na ikisha yafanyie uchunguzi wa kina mambo hayo mawili la kwanza ni(1)Kubadilika, Mfumo wa Tabia uloandamana na mazoea ya Akili, Kama litafanyiwa kazi hili lipasavyo mtu anaweza kubadilika, kumbuka huyo mwenzio mwanzo hakua hivyo ndio maana unaita kabadilika, kinachotakiwa kufanywa ni kwenda kwenye mizizi ya Mbadiliko wenyewe na kuanza kuufanyia kazi, (Mfano)wa kwanza labda Mume anapenda (Vimada)Muulize kwanini? Tatizo liko kwako au kwake sisitiza lazima upewe sababu, kwani hao walo nje na wewe hamna tafauti, isipokua kuna sababu itafute uifanyie kazi, labda kuna vitafunio hapati, vitafute mwenyewe utajua kama chakula au vitu vyengine.
Pengine yaweza kuwa mwenzio anapenda kutumia Ulevi wa aina fulani chunguza sababu zake nini kufanya hivyo, kuna mambo mengi yanasababisha hali kama hizo, yaweza kuwa anataka kuilaza akili yake labda asikumbuke madeni, au biashara imekwenda vibaya, au mtu kaondokewa na alo wake na sasa matafran yamemshika hajui afanyeje, hayo yote yanachangia kuanzisha misukosuko katika majumba na ndoa zikawa kama misiba, kila mtu anaingia na hamsini zake.
Sasa nini kinatakiwa mmoja katika nyinyi awe mvumbuzi wa mambo, na mambo yapo mengi ya kuifanya nyumba iwe na (Surprise) mpaka wageni wakiingia wanashikwa na mshangao na kusema (Haya Mambo)ikiwezekana chezeni (Foliti)Mchezo wa kujificha, Mwanamke ifanye Nyumba yako kama (Nursery)kwani Mwanamme ni kama mtoto na kila siku anataka (Kitu kipya cha kuchezea) Isiwe kazi yako umekaa kwenye Sofa na (Big G)mdomoni unaangalia kipindi chako cha TV, Kwa hilo hakai mtu ndani atakimbia.
Na la pili(2) ni hili la kusamehe, (Waingereza)wametumia neno zuri sana waliposema (Forgive)unaweza kuyafasiri hivi (Kwa wewe na Kupa)hiyo ndio (Forgive) hiyo ndio kwa wewe nakupa, unampa nini? Inaweza kuwa (Second Chance)Unampa kwa maana hutaki malipo, Unampa hutomuadhibu kichini chini wala hutomlipia kisasi, Unampa nafasi ajirekebishe sababu unampenda, Na mapenzi hayajui kuadhibu, Mapenzi ni yenye kutoa na hayajui kuchukua, Na hiyo ndio (For give) kusamehe na ukichambua sana mwisho utaikuta inasema (For love) kwanini? Kwa sababu mwenye chuki hasamehe, hana sifa hiyo. Ikiwa wewe unaweza kusamehe basi jijue kwenye moyo wako kuna Mapenzi, na Mapenzi mwenzie Subira, Ndio maana baada ya kusubiri sana alipopona nabii Ayoub a.s akaambiwa Mkeo kafanya utundu basi Msamehe kwa kufanya nini?
endelea part 3

No comments:

Post a Comment