Asalaam Aleiykum,
Nini Hali ya Mzazi wa kawaida aliyeondokewa na Mwanawe, ili Na wewe usije ukahuzunika sana, na usije ukadhurika na sumu za machozi, na maumivu ya mapenzi kwa Mwanao, Ndio Mollah anakumbusha kuwa kila Nafsi itakufa(Kuonja Mauti)Na kila nafsi imewekewa muda wake wa kupita katika Ulimwengu huu, na wakati wake mahususi na sababu zake. Na vile vile unakumbushwa Mzazi ukiondokewa na mtoto mdogo basi ujue ule Uchungu na shida unazozipata Mwenye Enzi Mungu anakuzindua uelewe yeye ndiye aliyetoa na sasa amechukua, unachotakiwa wewe uridhie msiba huo, pia ujue huna la kufanya katika amri ya Mwenye Enzi Mungu, Na kama utaridhika kweli ukawa hukufuru, Nini kinatokea?Mollah wako anakuteremshia Shufaa itokayo kwake(Na hakuna uponesho ulo bora isipokua ule ulotoka kwa Mollah wako).
Na kuna Shufaa za kila aina huenda Mollah wako akakupa zawadi nyengine ya kiumbe chake, au akakufanya hayo mapenzi ya mwanao kuyageuzia kwake Mollah wako, na kaa ukijua huyo mtoto yaweza kuwa akawa wa kukuombea siku hiyo ya siku (Siku ya Hukumu)Na wakati huu "Ewe" Mama ulofikwa na msiba, usiyafuge machungu, wala usiwe shujaa kwa kujizuia na huzuni yako, pata dawa yako kwa kuyaondoa machungu hayo, ikiwa unahisi kulia, basi lia, kama unahisi kucheka, cheka, ukihisi kuhamaki, hamaki, chochote kinachokuja moyoni mwako kitoe wala usihisi haya au kujizuia, ukiona unataka kuzungumza, zungumza, ukiona unataka kukaa kimya, kaa kimya, ukiona unataka kumkumbuka Mtoto wako mkumbuke, usizuie kitu, ila kumbuka kitu kimoja tu hizo fikira ndizo zenye kukuumiza basi nakushauri kitu kimoja zikija fikira zikumbuke hizoo zinakuja, na ukiweza kuzikumbuka zinapokuja hiyo ndio dawa yako ya kuondokewa na huzuni, na hapo utakua ushaushinda moyo na sasa hutopata maumivu tena, na kidogo kidogo machungu yataanza kutoweka.
"Ewe Mollah wetu tupe subira sisi na wazee waloondokewa na watoto wao""Ewe Mollah wetu tuteremshie huruma zako tupate kukubali amri yako" "Ewe Mollah wetu tupe kheri zako sisi na watoto wetu walo hai na walotangulia kuja kwako, Na utukutanishe tena katika Pepo yako ya Firdaus kwa salama na Amani Mollah wetu" "Ewe Mollah wetu wape shufaa Ndugu zetu na Waislam kwa Jumla walofikwa na Misiba itokayo kwako. Amin.
No comments:
Post a Comment