Asalaam Aleiykum,
Mwanzo kabisa Bwana Mtume s.a.w katoa Dirham 7 ili ende kwa Mollah wake Msafi,, Sasa na wewe kama unataka kuyapata mapenzi na huo Ucha Mungu wa Ghafla, Unaambiwa Toa kama unaweza. Utoe Nini?(Al-Imran 92) لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ
"Hamtoweza kuufikia(Kuupata)Wema mpaka mtoe katika vile mnavovipenda".
Nini Wema? Wema ni Mapenzi, Nini Mapenzi, Mapenzi ndio hiyo Taqwa, hamtoweza kuifikia hiyo Taqwa au Mapenzi mpaka mtoe vile mnavovipenda, (Wengine wanauliza Wema unauzwa wapi na mimi nikanunue) Leo ninakujulisha panapo uzwa Wema, wacha nikuoneshe duka linalouzwa huo Wema unalo Mwenyewe, (Shop keeper)Ni wewe bado hujagundua vipi Wema utaweza kuupata, Wewe na Mcha Mungu hamna tafauti, vile vote alokua navyo Mcha Mungu na wewe unavyo, Tafauti yake wewe hujui kuvifikia hivyo alonavyo Mcha Mungu, Ndio Maana unaambiwa ukitaka uvipate basi (Shuruti)lake toa katika kile unachokipenda, Sababu katika hicho unachokipenda nyuma yake kumejificha hiyo Taqwa, hicho unachokipenda ndio kizuizi baina yako na huo Wema, sasa unaambiwa Toa hicho unachokipenda uone (Result) yake, na (Result)yake ni hayo hayo Mapenzi, unatoa unachokipenda unapewa kinachokupenda, (Give n Take) Na kinachokupenda kina utajiri Mkubwa, kinachokupenda ndio chenye utajiri usokatika, kinachokupenda ndio kilokupa hayo unayoyapenda na mengi mengine ambayo yamo kwenye Ulimwengu huu, Kinachokupenda kinaendelea kutoa kila leo, kinachokupenda kwa mapenzi yake kimekupa mpaka huu Uhai na uwezo wa kuyapata hayo unayoyapenda, Yule ambaye anakupenda anakwambia kunifikia mimi, kuwa karibu na mimi, basi toa utengane na hicho unachokipenda, Na utakapo kitoa tu, basi mimi na wewe tunakutana na unakuwa Kipenzi changu, madhila na dhiki yanakuondoka, shida na matatizo zinatoweka, lakini lazima utoe unachokipenda, hiyo ndio (Thamani unayotakiwa ulipie Penzi la Taqwa).
Katika kutoa kuna Raha fulani inapatikana kwa anaepewa na mwenye kutoa, lakini ukiona umehisi raha fulani katika kutoa huko basi hiyo inakua bado hujatoa, kutoa ili uupate Ucha Mungu inatakiwa Mtowaji hayupo na nafasi yake kabaki Mwenye Enzi Mungu, "Ewe"Mwenye Mali au Mapesa unajiuliza kutoa huku kuna kuwaje ili nipate Ucha Mungu(Mfano)Una Million 20(Au Kidani chako chako cha Almasi), watafute Maskini kumi waambie nimeamrishwa na Mollah wangu hizi Million 10 kumi nikupeni nyinyi ili muanze biashara na hizi sikupeni mimi ila Amri ya Mollah wangu na mimi nimo katika kuitekeleza, Au una nyumba tatu unatoa moja kuwapa wasiokuwa na uwezo iwe yao mali yao, tena iwe ili nzuri unayoipenda, unawapa hii kakupeni Mollah wangu kaeni familia nzima.
Na "Ewe" Mwenye Mshahara mkubwa zikimbilie kheri za kuwalisha viumbe wenzio unaowajua wana shida. nyumba ina watoto 7 mzee wao ana hangaika kutafuta Riziki, sema kuanzia leo mimi nitakua naleta chakula mpaka mtakapopata uwezo, nusu mshahara wangu utakua haki yenu, nachukua dhamana hiyo kwa kutafuta Radhi za Mollah wangu.
Na "Ewe" Maskini msokitu wewe unakikubwa zaidi cha kujitolea, sema Mollah wangu najikabidhi kwako kwa haki ya uhai wangu niwe Mtumwa wako katika kukuabudu wewe, katika kuwatumikia viumbe vyako kama utavyoniamrisha, "Ewe"Mollah wangu unaujua udhaifu wangu mimi sina cha kutoa na wala sina ninachokipenda isipokua dhati yako yenye Uweza, basi nipe mimi Ridhaa yako ya kuupata huo Wema ulojaa Neema zako, wewe Mollah wangu ni mwenye kujaalia Mapenzi, basi naomba nichague katika wale viumbe vyako uloviongoza katika hayo Mapenzi yako ya Taqwa.
وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَىۡءٍ۬ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ۬
"Na chochote mnachokitoa, Basi Mwenye Enzi Mungu anakijua"
usije ukajifanya mjanja unatoa nyumba yako mbovu, inayotakiwa ni ile mpya yenye (swimming Pool), au ukawapa pesa huku unawanongoneza ukipata utanirudishia, au unaomba dua Mollah nipe utajiri nishachoka kusubiri, toka nimenyanyukia nahangaika na maisha basi nipe na mimi ikisha ntafanya Ibada kwa wingi, Mollah ni mwenye kujua kila mipango yako ilofichika kwenye kifua chako.
Usiwe mwenye kutoa kama mwana siasa au mfanya biashara mpaka Wapiga picha wawepo, au watu wajue katoa, huko sikutoa kwa (Ikhlas) ni shirk ya kujionesha, kutoa kwa kweli ni kule unajua wewe tu na mpokeaji kama umetoa, huna haja ya matangazo au picha au usikike redioni, na ukitoa kama alivoamrisha Mollah wako basi kwa hakika yanaanza kukushukia mapenzi hiyo ni (Gurantee) wewe toa, utakuja nikumbuka ukitoa kile unachokipenda kweli katika moyo wako basi na huku (Something happen)katika moyo ikisha inaanza ku (Grow slowly) na kikisha ota kwa ukamilifu wewe Mcha Mungu, wewe ushaupata huo wema, na ni Bora kuishi na Wema kuliko kuwa Millionea. Sasa jitizame ukimpenda Mtu unakuwaje, sasa yapime mapenzi hayo hayo lakini yameongezeka mara million unapenda kitu usichokiona, na kila siku zikizidi unashauku ya kukisogelea karibu kutaka kukijua, na kila ukisogea mapenzi yanazidi, na maajabu yanaongezeka na huo ndio Ucha Mungu ambao tunamuomba Mollah atujaalie kwa sote. Amin.
No comments:
Post a Comment