Sunday, February 23, 2014

NGAZI SABA ZA ROHO PART 1(NGAZI 1)

Asalaam Aleiykum, 

Leo nimetamani kukupeni zawadi hii nikiwa na Imani na kuamini kama Mtu atayafahamu haya ninayo andika basi atapata faida ya kujua mambo kwa upeo mwengine kabisa, Atatumia mtu somo hili ndio iwe njia ya kumbadilisha au kubadilika kama atavotaka. Tukijaaliwa tutazipanda ngazi hizi moja baada ya nyengine kwa utaratibu ili tupate kujua katika kila ngazi kuna hazina gani na kama kuna faida na hazina hizo.
Pia napenda ufahamu inayopanda hizo ngazi ni (Roho)na wala sio Mtu ana madevu meupe, Na nikisema (Roho) wengine watataka kuitafuta waone inapanda vipi, hivyo ndio Binaadamu alivyo, lakini kama utasoma kwa makini utakujia ufunuo wa kufahamu kusudio la ngazi zenyewe na utapata kujua vipi hiyo (Roho)inavopanda. Ili kufahamu kwa undani zaidi itabidi tuanze na aya ya mwanzo iloteremka katika kitabu kitukufu Quraan, ili ituoneshe hizo ngazi zenyewe  ziko wapi.Sura ya Alaq aya ya 3
 ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ 
Soma Mollah wako ni Karim(Mkarimu)
Umepatikana Ukarimu mkubwa kama utazingatia kwa makini, Amehadithia "Anas kasema Bwana Mtume s.a.w hakika ya Malaika wanasema"Mwenye enzi Mungu katuumba sisi, Ikisha kamuumba Mwanaadamu""Akamjaalia kula Chakula, akaweza kunywa vinywaji, akawa mwenye kuvaa nguo, Akawapa Wanawake, wakawa wanapanda wanyama,Wakawa wanalala na kuamka," Na wala hatukujaaliwa sisi chochote katika hayo, Akawajaalia Dunia ikisha baada yake kuna Akhera. Akajibu Mollah wako "Nimemjaalia yule niliyemuumba kwa mikono (Uwezo wangu)Ikisha nikampulizia (Roho)inayotokana na Mimi, kama alivosema Kuwa ikisha Ikawa".
Basi soma kwa ajili ya Mollah wako aliye Mkarimu, katika hadith hiyo Malaika wanaanza kukuonesha njia wanakumurikia (Torch)zione fadhila za Mollah wako kwenye ngazi hii ya kwanza, unaweza kuzingatia hayo, yanaingia akilini moja baada ya jengine, basi ikiwa ushaona njia soma aya ya 4 ya sura hiyo hiyo ili tuanze kupanda ngazi.
 ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ 
Ambaye amemfundisha kwa Kalamu(Akili)
Nani Mfundishaji ? Mollah wako, Nani anae fundishwa Mwanaadamu, mafundisho hayo yanapita au kuingia kwenye hiyo Akili, kwa hiyo utagundua mafundisho yanatokea ndani, hapa itabidi tufahamu tafauti ya mafundisho(Understanding) na Elimu (Knowledge) utagundua (Understanding) inatokea ndani na Elimu (Knowledge) inatokea nje lakini pia ni matunda ya (Understanding)lakini naita ni (Dead Memory)(Understanding)ni (New Memory)mambo ya nje ni yenye kupandikizwa katika hiyo Akili, ndio utakuta unaambiwa kwa Mollah inapatikana (Hekima) na kwenye hizo (School, College, na Uni)zinapatikana hiyo Elimu ambayo ni Mamillion ya copy za Akili za watu ziloandikwa kwenye vitabu.
Lakini Ufahamu sahihi unatoka kwa Mollah ambaye kasema katika sura ya Taha aya ya 98.
إِنَّمَآ إِلَـٰهُكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ‌ۚ وَسِعَ ڪُلَّ شَىۡءٍ عِلۡمً٨
Hakika Muabudiwa wenu ni Mwenye enzi Mungu tu, ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye, Amekienea kila kitu kwa Elimu.
Ukiweza kulijua hilo kuwa Mwenye enzi Mungu amekienea kila kitu kwa Elimu, ndio sasa utaingia na kuifahamu uzuri aya inofatia ya sura ya Alaq aya ya 5 ili tupate kujitaarisha kuipanda hiyo ngazi ya kwanza. Endelea part 2

No comments:

Post a Comment