Asalaam Aleiykum,
Ajiangalie Mwanaadamu nani alokufundisha kutambaa, akakufundisha kutembea, akakufundisha kuzungumza,akakufundisha hichi na kile, akakuonesha maajabu haya na yale, ukawa kila leo utotoni unagundua hichi na kile ukakifahamu bila ya kuwepo Mwalim mbele yako, na mengi mengineyo na ukisha ulipotimia miaka 14 akakufungulia ukurasa mpya wa (Sex Energy)au kumi na mitatu kwa Wanawake, Ukawa tayari sasa umeingia katika Ulimwengu wa Fahamu, Unaendelea kuishi katika ngazi hii ukiwa unapata mazoea ya kila kitu na mafundisho na baadhi ya elimu zinaendelea kumiminika samba samba katika Akili yako, hapo tena unafanya maamuzi nini unataka, nani unataka kuwa(Japo kwa wengi maamuzi hayo yanafanywa na wazazi)unachagua njia zako za kila aina, elewa katika kipindi hicho chote kuna (Group)tatu , mbili zinapigana kukusomesha na moja imetulia inakufundisha taratibu.
Ama (Group) ya mwanzo ya Kilimwengu inapigana kukusomesha mambo ya Kidunia, kukupa (Gossip)kukupa habari za maendeleo, zengine mpya zengine za zamani, wanakuhimiza nunua gari mpya, jenga nyumba mpya, oa mke huyu, olewa na mume yule, mambo yako yote ya Ulimwengu, na ile (Group)ya Pili ambayo ni ya watu wa dini nayo inajitahidi wewe funga, usiwache kusali, huko kuna pepo, huko kuna moto, kuna mateso makubwa, na hivi na vile.
Halafu linasalia hili lenye ukweli, lenye kukujulisha taratibu tena kwa uyakinifu, lenye kukufundisha kuijua haki kwa dalili na kukuonesha kwa uwazi uso shaka kuwa upande wa pili kuna hivi na vile, unaambiwa kwa utaratibu hivyo usifanye ni (Kosa)utadhurika,na unajua kweli hili ni kosa (Lakini wapi)unaambiwa unaona Moyo wako sasa hauchukui usije ukenda mbio huziwezi tena, sasa acha (Disco) na kwenda vilabu vya pombe ushakua mtu mzima, lakini husikilizi kabisa taarifa za ndani huna haja nazo kabisa, ukiona kero unafungua nyimbo, ukiona kina zidi sana unafungua senema(TV)ukiona maelezo yanazidi huyo unatoka kwenda Barazani kwenye mazungumzo, lakini kwa kuwa ni haki yako upande huo wa pili unaendelea kukufundisha na kukupa taaluma. Hii wewe hujachoka huoni marafiki wamepungua, huoni kama unapitwa na wakati, mbona hivi umeshughulika na mambo yaso maana katika umri wako ulo Adhimu, hebu kumbuka umefanyiwa Ukarimu, jee umelipa nini katika Ukarimu huo?
Nini kitu hicho?
Hiyo ni Roho yako ambayo iko ngazi ya kwanza inakufundisha kuwa zipo zengine sita, lakini hutaki kabisa kuisikiliza.(Mara moja moja ndio unaisikiliza ikisha unasema kweli Roho yangu ilikua nzito sikwenda pahala pal au sikusafiri ndio ajali imetokea unaona). Na kwanini tusifundishwe wakati (Baba yetu Adam a.s)alifundishwa, na wewe mpaka leo mafunzo hayo yanaendelea, lakini umekua mtoro, unayakimbia huyataki, hutaki kusikia habari hii, inakutia dhiki.
Ndio maana utakuta watu wengi habari za upande wa pili zinawafika lakini wameshughulika na Ulimwengu.
Sasa nakupa kidogo mfano wa mafundisho yenyewe ili usije ukaona labda mazinga ombwe, (Unapokua na Njaa unajuaje, hakuna chengine ila fahamu zinakujia kuwa sasa tumbo lina njaa, na sio tumbo mwili unapeleka taarifa tumboni ili uambiwe utafute chakula)
Unaposhikwa na usingizi mwili pia unakwambia tushachoka kalale, mwenyewe unasema usingizi umenishika, sasa hayo ni machache tu katika ngazi hii,sasa upo kwenye(Ghorofa ya fahamu hizo) lakini (Massage)zinakuja kutoka upande wa Pili lakini huzisikilizi, hutaki kufahamu, unazidi kushughulika na dunia, unagombea hichi na kile, Unamkuta mtu mzima bado anagombea vyeo, kama hapati cha siasa basi mpaka cha msikitini lazima awe Imam, kama haupati Uimam awe japo mkuu wa karata, awe msimamizi wa sadaka, awe chifu, au mjumbe wa nyumba kumi, kila kitu (Ambitions)za Ulimwengu huu, na utawakuta wengi wamebaki katika Umri uleule wa (Baleghe)bado wako kwenye maisha ya utotoni (Teens)bado wanatafuta (Boyfriend na Girlfriend)(Vimada)bado wametawaliwa na Ulimwengu wa anasa, bado anataka gari mpya, bado anataka nyumba nyengine, anashughulika Mja katika ngazi hii kutaka kujulikana, kutafuta cheo, na mambo mengi ya kipuuzi katika maisha haya huku akisahau kabisa sauti ya ukimya inayomfundisha "Ewe Mwanaadamu"kipo kitu chengine kwenye ngazi zengine"usibakie kwenye ngazi hiyo utakua hasarani, zipo sita hebu zitafute ukamilishe maisha yako, mbona umecharuka kulimbikiza mali, kuonea wenzio, kudhulumu haki za watu, hebu wacha uje kwenye ngazi ya pili uone kuna nini, njoo uchungulie ghorofa hii labda utazinduka usingizini ujue kumbe kuna zaidi ya haya.Na ukipanda Ngazi ya pili unapata (Shock)unakutana na kitu cha kustaajabisha kitu gani hicho?
Inshaallah tutaendelea wiki ijayo hiyo ngazi ya Pili
No comments:
Post a Comment