Sunday, February 9, 2014

KUFA HUKU UMEFURAHI PART 1

Asalaam Aleiykum,

Tunaingia katika ile Darsa ambayo sote tunaiogopa, Maudhui ambayo yakitajwa Mtu anasema huyoo keshanza kututia dhiki, lakini ni wajibu wangu kukumbusha na kufundisha vipi utaikabili siku hii Adhimu, yenye vishindo na machungu makubwa ambayo mwanaadamu anakumbana nayo, Imekua siku hii kila Mtu anaiogopa na yuko tayari anywe madonge kama Mlima kuepukana nayo, au kama kuna vidonge vya kuweza kuisahau basi atakunywa ili asikumbuke, lakini vidonge hakuna ila kuna Milima ya Dhanmbi ambayo Mwanaadamu ndio kaamua kujificha ili Kifo kikija kimjie ghafla, hataki kukijua hataki kukikumbuka na akikumbushwa anakua mkali. Sasa kwanini wakati wa Mauti unakua na hofu kubwa?.
Khofu inakuja sababu kubwa ni ile ya kumsahau Mollah wako Muumba, Ni kwa ajili ya kujua sasa unakwenda kukutana naye, Na hujui nini kitakukuta, Na kwa wakati huo wa Mauti unakua wewe mweupe, safi, huna cha kukukera akili imeshasimama haitumiki tena, Inakua Baina ya Roho na wale walokuzunguka viumbe wasiri(Malaika)Unazinduka wakati huo ukitokea usingizini wa Uhai na kuingia kwenye mzinduko wa Mauti, Hapo tena unayaona yote ulokua unaambiwa ukawa unayatilia mashaka yanatokea (Live)na wewe ukiwa Shahidi wake, unaanza kuonja Uchungu wa kutolewa (Roho)Unaanza kujua vipi Maumivu ya kukosa (Oxygen) na balaa yake, jasho linakumiminika huku ukiwaza lau wangejua wangenipa (Pipa)zima la (Oxygen). Hivo ndio inavotokea wakati wa kufa, pale (Body)Ishaanza Ku(Shut Down)taratibu, na huku unashangaa Nani hawa walonizunguka mbona hawacheki, na hii Operesheni wanonifanyia ya nini? hapo ndipo unaposomewa aya ya 92mpaka93. "Kwani situlikwambia kama utakua hivo ulivo sasa na sisi tutakutana na wewe tukujulishe".
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّين
"Na kama akiwa ni miongoni mwa waliokadhibisha, wapotofu" Hiyo ndio hali unayokutana nayo, Mauti yanakua shida tupu,

فَنُزُلٌ۬ مِّنۡ حَمِيمٍ۬
Basi karamu (yako)ni maji ya moto yachemkayo, Vuke lenye kukata (Oxygen), basi ikiwa wewe Mwenye kujiwa na hofu na siku hii ya miadi, au ikiwa unaghafilika nayo siku hii basi inapasa ujiulize Mwenyewe kwa Mwenyewe "Ewe Moyo Wangu" Nihadithie kwani kuna Jambo gani kubwa umefanya hata nikawa nina hofu mimi ya siku hii? Mbona naogopa sana, lazima iko sababu pengine kwa haya ninayoyatenda, na kama unaendelea kuyatenda (Ushauri utokao kwangu nakushauri ili uweze kuacha basi fanya uone Maiti japo tatu, itakusaidia sana kuchenji mwenendo wako, utabadilika uwe Mtu mwengine kabisa) Naam, utapata mateso makubwa siku yako ya kutoka Roho ikiwa una maradhi ya Mali au cheo, Au umebakisha chuki moyoni, Tahadhari sana kuweka hamaki na ghadhabu utakua hasarani siku hiyo ya siku, ondosha sasa hivi kama una husda au wivu na choyo kwa Binaadamu wenzio usije ukateseka siku ya kutolewa Roho yako, kwani ukiyaweka Rohoni ni lazima (Malaika)waanze kuyakumta hayo kwanza halafu ndio waanze kuifanyia kazi Roho, huku watu wanaulizana vipi hali yake, wanajibiwa siku ya tatu leo yumo kwenye msukosuko mkubwa, huku wewe umelala kwenye tandiko la Mauti, na visasi vyako, unaondoka na magonvi umeyashikilia Rohoni, weka mbali na zile Dhanmbi ulizokua hujatubu kumbuka vitakupa uzito mkubwa siku yako ya kutolewa Roho.
Sasa Ufanye nini uondokane na hali hiyo?
Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment